Loading...

Wednesday, December 12, 2007

Heri Mkoloni wa Nyamagana?

Hayawi hayawi sasa tunaambiwa yamekuwa. Kwa mujibu wa gazeti la leo la The Citizen, uamuzi wa kuvunja uwanja wa kihistoria wa Nyamagana uliopo mjini Mwanza ili kuwapisha wawekezaji umekwishafikiwa. Uwanja huo ulisanifiwa enzi za mkoloni na Dokta John Thoburn Williamson wa Williamson Diamonds Limited. Uwanja huo ulijengwa mahsusi kwa ajili ya wakazi wa Mwanza ambao mababu na mabibi zao walipoteza maisha yao kwa ajili ya wakoloni kwenye Vita Kuu ya Pili. Hivyo, kwa kipindi kirefu wakazi wa mji huo, wakiwamo watoto, walikuwa na uhuru wa kuutumia uwanja huu. Je, sasa wataipata fursa hiyo lini, wapi, na vipi?

Katika dunia ya leo ya 'utandawazi' ambayo inahubiri kuwa wawekezaji wana wajibu kwa jamii (corporate social responsibility) kunakuwa na utata pale wawekezaji wanapowezeshwa kwa nguvu za dola kutoiwajibikia jamii. Mkoloni mmoja aliwahi kusisitiza kuwa hakuna kitu chochote kinachoweza kumfidia mwafrika aliyenyang'anywa ardhi yake. Kama wakoloni na ubaya wao wote waliweza kufikiria walau kidogo kuhusu wajibu kwa jamii waliyoitawala je tunapata picha gani kuhusu ukoloni mamboleo pale tunaposhuhudia ukikiuka hata misingi ya huduma kwa jamii iliyoachwa na ukoloni wa kale? Je, 'Heri Mkoloni kuliko Mkoloni Mamboleo'?

1 comments:

mkimbizi ktk nchi yake December 12, 2007 at 4:27 PM  

mmh nadhani sasa hivi hata Muhimbili watabinafsisha kwa wawekezaji wajenge apartments au mnaonaje wanablog? Manake si mchezo rushwa mpaka kwa mahujaji wallah tena tumeshauzwa bila kujijua! Bora Enzi za ukoloni kwani reli walizoacha hazijabadilishwa hadi leo, miundombinu ya umeme na simu mabadiliko yamefanyika miaka ya tisini. Sasa wasingekuja jeeee? TWAFWAAA

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP