Loading...

Wednesday, December 19, 2007

Kulikoni kizazi cha MMEM/PEDP?

Matokeo ya darasa la 7 ya wale wanafunzi waliojiunga na darasa la kwanza mwaka ambao MMEM/PEDP ilianza rasmi, yaani 2001, yametolewa rasmi jana. Vyombo vya habari vimemkariri Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akitoa takwimu za matokeo hayo. Kwa kweli zinasikitisha. 54.18% ya wanafunzi 419,198 waliofanya mtihani ndio 'wamefaulu'. Inasemekana kuwa kiwango hiki kimeshuka kwa 16.3% kutoka kwenye kiwango cha 70.4% kilichorekodiwa mwaka jana.

Bila shaka wadadisi wa masuala ya elimu wameshaanza kugonganisha vichwa vyao kuhusu matokeo haya. Itakumbukwa kuwa kwa kipindi kirefu wadau wa Elimu kama vile TEN/MET na HAKIELIMU wamekuwa wakilivalia njuga suala la kuhakikisha kuwa 'Wingi wa wanafunzi'(Quantity)unaendana na 'Ubora wa Elimu '(Quality). Ni dhahiri kuwa matokeo haya ni uthibitisho tosha kuwa 'Elimu bora' ni muhimu kuliko 'Bora Elimu'.

Kwa uchambuzi wa changamoto/uwiano/ukinzani wa 'wingi na ubora' kwenye nyanja ya elimu soma makala ya 'Shall we address Mwalimu Nyerere's unanswered question' kwenye hifadhi ya blogu hii.

1 comments:

Anonymous December 21, 2007 at 9:54 PM  

Chambi
Tanzania tuna ugonjwa wa ubishi. Kila mtawala anakabiliwa na ugonjwa wa kubisha. Mpaka watawala hawa watakapoachana na tabia hii na kutofautisha utawala na siasa, mambo yatakwenda. Ila kwa sasa, tunatawaliwa na wajinga wengi wasio na uchungu na nchi hii

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP