Loading...

Friday, January 25, 2008

Maji ya Kumwaga Umeme Kiduchu!

Sijui haya nayo ni maporomoko ya kudumu au la ila hapa ni Rusumo, kwenye mpaka wetu na Rwanda. Huo ni mto Kagera. Naona hayo maji ni ya nguvu na yanaweza kuzalisha umeme. Je, wataalamu wetu wanajua kwa nini hatuyatumii kuongezea umeme kwenye gridi ya taifa ambayo haitoshelezi mahitaji yetu?

Je, maji haya hayatumiki kwa kuwa hatuna uwezo wa kujenga mitambo?Au hayatumiki kwa sababu hayana nguvukasi ya kutosha kutoa kiwango cha kutosha cha umeme? 'Kwa nini?'

Kuna umuhimu wa kuendelea kudadisi maana bei ya umeme inazidi kupanda. Nasikia mwezi huu imepanda kwa zaidi ya 20% japokuwa nishati hii inafikia takribani 10% tu ya wananchi!Umeme ni bidhaa adimu Tanzania, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe n.k, kwa nini hatuuzalishi kwa wingi?

1 comments:

Anonymous January 28, 2008 at 12:04 PM  

Mimi bado natatizwa na mantiki ya Serikali kuachana na mradi wa Stiegler's Gorge. Kwa wasiojua habari ya mradi huu kuna dondoo chache katika http://www.bongotz.com/bongoyetu10_%2029_06.htm

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP