Loading...

Monday, April 7, 2008

Mwekezaji Anapowezeshwa!

Kwa mujibuwa Vyombo vya Habari Mheshimiwa Waziri Mkuu, ametatua mgogoro uliopelekea wafanyakazi wa Shirika la Reli lililobinafsishwa kwa kampuni kutoka India Kugoma. Sio siri ni jambo la kufurahisha kuona kuwa wafanyakazi hao watalipwa mishahara yao. Ila swali la kujiuliza ni iweje mwekezaji ashindwe kuhudumia wafanyakazi wake mpaka Serikali imkope shilingi bilioni 3.6? Yaani ule uwezeshaji wote wa vivutio wanavyopewa na TIC havitoshi?

Na hizo dalili za wingu la ufisadi ambazo zinajidhihirisha zitachunguzwa au yaliyopita si ndwele tugange yajayo? Naam yajayo yatatokea baada ya hiyo miezi 5 ambapo hizo bilioni 3.6 zitakuwa zimekwisha. Je, mwekezaji atakuwa amejizatiti au atataka kuwezeshwa tena na Serikali yetu iliyoelemewa na mizigo mingi ya madeni ya uwekezaji mbovu na inayowezeshwa na wafadhili?

Hakika ndio maana Mwalimu Nyerere alilalamika kuwa mbona wanatuambia tubinafsishe vya kwetu wakati vyao hawabinafsishi. Ndio maana alisisitiza kuwa 'you cannot nationalize nothing' yaani huwezi kubinafsisha kisichopo. Kumbe tulikuwa navyo na fedha tunazo. Kuifadhili TRL kunadhihirisha kuwa bongo tambarare kama anavyouliza kwa bezo mtoa maoni wa blogu ya Michuzi?

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP