Loading...

Wednesday, June 11, 2008

Ardhi isiyo ya Mtu - 'No Man's Land'?

Dhana tete inayodai kuwa ardhi fulani, mahali fulani, wakati fulani haina mwenyewe ilitumiwa sana wakati wa enzi za walowezi wa kikoloni kuhalalisha unyang'anyi wa ardhi ya wafugaji na wakulima wa Afrika. Mgogoro wa ardhi unaoendelea katika kijiji cha Vilima Vitatu (pichani) wilayani Babati ambapo mwekezaji amepewa eneo kubwa la ardhi pembezoni mwa Ziwa Manyara ili ajenge kambi/loji ya kitalii unadhihirisha kuwa dhana hii bado inatumiwa kujipatia ardhi nzuri ya jamii hata leo. Dhana, kama ilivyo maneno, huumba. Je, ni dhana za aina gani ambazo jamii yetu inazienzi? Je, dhana hizi zinaumba jamii inayojali haki na usawa au inajenga jamii ya kibeberu na kinyang'anyi?


0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP