Loading...

Monday, June 30, 2008

Ufisadi ni Siri ya Serikali?

Mvutano mkali kati ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Dk. Wilbroad Slaa, na Waziri wa Utawala Bora, Philip Marmo, unazidi kupamba moto. Hoja ya Marmo ni kuwa Slaa anakiuka taratibu na Kisheria kwa kuwa na nyaraka za siri za Serikali. Kwa upande wake, Slaa anasema Marmo ndio anakiuka sheria kwa kuficha nyaraka za kifisadi.

Mgongano wa hoja zao unadhihirisha kuwa haki ya ya Kikatiba ya wananchi kupata taarifa muhimu zinazohusu masuala muhimu kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 18 bado ina tafsiri tete. Hii inatokana na ukweli ni vigumu kujenga hoja kuwa Slaa anavunja sheria kwa kuwa hakuna sheria inayosema ufisadi ni siri za Serikali - au ipo?

Mjadala uliozuka kuhusiana na suala hili ni vyema ukaendelea ili kupanua wigo wa uelewa wetu kuhusu haki yetu ya kupata taarifa. Maswali ya kujiuliza ni kuhusu uzito wa Kisheria wa hoja hizi:

"Sisi tulimuonya [Slaa] kuwa asiendelee kuchukua nyaraka bila kufuata utaratibu ili asije kupata matatizo mbeleni. Huwezi kujitetea kuwa umevunja nyumba na kuiba kwa sababu una njaa, kwa hiyo ufisadi isiwe sababu ya kutofuata Sheria za nchi...Dk. Slaa ni Mbunge ambaye anafahamu Sheria na yeye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa hivyo ni rahisi akafuata taratibu zilizopo na akapata nyaraka anazohitaji kuliko kutumia njia zisizo halali... Sote tunapinga ufisadi lakini lazima tufuate sheria" - Philip Marmo

"Wanataka kunikamata mimi eti kwa kupata nyaraka za Serikali lakini anayestahili kukamatwa ni Waziri Marmo ambaye anaficha wizi na ubadhirifu kwa kisingizio cha siri za Serikali. Mimi nimetoa vielelezo vya wizi, hivi wizi na ubadhirifu vinahusiana vipi na Sheria ya siri za Serikali?`" - Dk. Wilbroad Slaa

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP