Loading...

Wednesday, July 9, 2008

Utaalamu Mbadala Upo Umejaa Tele

Mchakato huu wa kuzalisha mkaa utokanao na uchafu/takataka kwa kutumia mtambo uliotengenezwa hapa nchini ulinivutia sana katika maonyesho ya Saba Saba 2008. Mtambo huu umetengenezwa na taasisi ya teknolojia inayofaa kutumika vijijini (Appropriate Rural Technology Institute). Mwaka 2002 taasisi hii ya ARTI-TZ ilishinda Tuzo ya Nishati Endelevu ya Ashden. Jitihada zake za kuvumbua nishati mbadala zinazoendana na mazingira yetu ni kielelezo tosha kuwa uwezo/utaalamu wa kujifanyia mambo yetu wenyewe tunao. Hii ndio ilikuwa njozi ya Muasisi wa Siasa na Elimu ya Kujitegemea.
Hatua ya 1: Kukusanya Takataka
Hatua ya 2: Kuchoma Takataka

Hatua ya 3: Kufinyanga Mkaa

Hatua ya 4: Kutumia Mkaa

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP