Mwamko wa Kizazi Kipya!
Wakati kizazi cha zamani kikizidi kutopea katika usingizi mzito wa usahaulifu wa historia, kizazi kipya kinazidi kupata mwamko wa kifikra wa hali ya juu kuhusu historia ya mapambano ya kudai haki na usawa. Kizazi hiki kinachojulikana kama kizazi cha 'doti komu' kina fursa ya kupata ufahamu na taarifa kwa kasi ya ajabu kutoka katika vyanzo mbalimbali. Wadadisi wa mambo wanaamini kuwa hiki ndicho kizazi kitakachotuletea ukombozi wa tatu kama alivyopenda kuuita Mwalimu Julius Nyerere. Kwenye picha ni baadhi wa watoto na vijana wa kizazi hiki walioandamana jana kupinga kupanda kwa nauli ya wanafunzi kwenye vidaladala kwa 100%.
Kulikoni? Lo! Ule msemo wa 'asili huchukia ombwe' sasa unadhihirika waziwazi! Ombwe la madaraka ndio hili linaanza kuzibwa na utashi wa asili wa mwanadamu aliyesongwa na kuchoshwa na hali iliyopo! Tuikumbuke Sharpeville! Ole wetu tusipozisoma nyakati hizi za wakati! Mungu ibariki Tanzania! Wabariki na watoto wake!

0 comments:
Post a Comment