Loading...

Sunday, November 16, 2008

Buriani Ben Mtobwa

Nimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha mwandishi maarufu, Ben Mtobwa ama 'Joram Kiango'. Taifa limepoteza kinara mwingine wa kutumia fasihi andishi kufichua masuala mazito yaliyoigubika jamii yetu. Hivi karibuni nilimwona gwiji Ben pale kwenye Mkahawa wa Vitabu wa Soma akipanga mikakati ya uandishi na uchapishaji.

Nilidhani huo ni mwendelezo wa kumwona mpiganaji huyu akiwa katika harakati za kutumia 'mtutu wa kalamu' kufichua uzandiki na ufisadi katika jamii. Lakini upeo wa mwanadamu una kikomo. Hivyo, sikujua kuwa hiyo ilikuwa mara ya pili na ya mwisho kumwona mwanaharakati huyo ambaye pia alijitosa katika fani ya uhariri wa gazeti la Heko na uchapishaji kupitia kampuni yake ya Heko Publishers.

Nawasihi tumpe mtunzi huyu 'Zawadi ya Ushindi' kwa kusoma kwa undani vitabu vyake ili tutambue ni nini hasa amejaribu kutufunulia 'Nyuma ya Mapazia' ya jamii yetu iliyozingirwa na 'Malaika wa Shetani' na mafisadi wenye 'Roho ya Paka' wanaomsulubisha 'Mhariri Msalabani' na kudiriki kusema 'Najisikia Kuua Tena' kupitia mikataba mibovu wanayoisaini 'Dar-es-Salaam Usiku' pasipo kumwambia mwekezaji uchwara 'Peza Zako Zinanuka' na tena bila kuogopa 'Salamu Kutoka Kuzimu' au kilio chetu cha 'Tutarudi na Roho Zetu?' Buriani Ben Mtobwa!

3 comments:

Anonymous November 16, 2008 at 7:54 PM  

Kweli hizi ni habari za kusikitisha sana. Bw. Mtobwa alikuwa mwandishi mahiri sana wa riwaya. Nakumbuka riwaya yake ya Dar es Salaam Usiku ilinifanya nichelewe kwenda shule wakati niko shule ya msingi nikaishia kuchapwa viboko. Mbali ya kwamba nilikuwa shule ya msingi, lakini nilitafuat hela na kuweza kununua riwaya zake nyingine kama Salamu kutoka Kuzimu na Pesa zako zinanuka.
Ni vizuri kumuenzi kwa kuendeleza yale mema aliyoyaacha.

MBOGELA, Jackson November 17, 2008 at 3:27 AM  

Salaam zangu za pole ziwafikie Familia ya Ben Mtobwa na Watanzania kwa ujumlaa kupotelewa na mpiganaji mwanafasihi maridhawa Ben Mtobwa. Bwana ametoa na Bwana ametwa jina la Bwana libarikiwe.

Mathew A.Ngwahi March 4, 2018 at 9:09 PM  

Riwaya za Ben R. Mtobwa, Zilikuza sana Fikra zangu wakati ningali shule ya msingi. Zilinijenga sana kiakili na kifasihi, nikaishia kuwa Kijana mwenye Upeo sana katika Umri ule. Nimenunua upya vitabu vyake vyote kwa Ajiri ya wanangu ambao Tayari wameanza kuwa mahiri sana katika usomaji.

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP