Loading...

Sunday, October 25, 2009

Tujikumbushe: Alichosema Waziri wa Fedha & Uchumi kuhusu Bajeti ya Nishati 2009/2010!

"Nishati na madini imetengewa shilingi bilioni 285.5 ikilinganishwa na shilingi bilioni 378.8 zilizotengwa mwaka 2008/09, sawa na upungufu wa asilimia 24.6. Hali hii imesababishwa na kumalizika mikataba ya kuzalisha umeme kwa makampuni ya kukodi ya Dowans, APR na Aggrekko. Hatua nyingine zinachukuliwa katika mwaka 2009/10 kutafuta mikopo kutoka mashirika ya kimataifa na nchi marafiki ili kuweza kupata rasilimali zaidi za kufanikisha miradi ya nishati nchini. Nchi na mashirika ya fedha ya kimataifa yameonesha nia ya kutusaidia zikiwemo Korea ya Kusini, Saudi Fund, BADEA, na OPEC Fund." - HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI MHE. MUSTAFA HAIDI MKULO (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAPENDEKEZO YA SERIKALI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2009/2010

KTY: Kwa mujibu wa hotuba hii ya Bajeti aliyotoa Waziri huyo, kati ya sekta/maeneo 6 "muhimu" ambayo "kwa pamoja yametengewa jumla ya shilingi bilioni 5,103.2 sawa na asilimia 64 ya bajeti yote ya mwaka 2009/10", ni sekta ya nishati na madini tu ambayo bajeti yake ilipungua/ilipunguzwa kutoka kwenye bajeti ya mwaka jana - za zingine 5 zilizobakia ziliongezeka kama takwimu hizi na asilimia zake za ongezeko kwenye mabano zinavyoonyesha:

Elimu: Sh Bilioni 1, 743. 9 kutoka 1,430.4 (22%)

Kilimo: Sh Bilioni 666.9 kutoka 513.0 (30%)

Miundombinu: Sh Bilioni 1,096.6 kutoka 973.3 (12.7%)

Afya: Sh Bilioni 963. 0 kutoka 910.8 (5.7%)

Maji: Sh Bilioni 347.3 kutoka 231.6 (50%)


Swali: Kuna uhusiano gani kati ya maeneo haya 5 yaliyopata ongezeko na eneo la 6 la 'nishati+' lililopata punguzo?

Jibu: Mgawo wa Elimu, Kilimo, Miundombinu, Afya na Maji!

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP