Loading...

Wednesday, June 23, 2010

KUMBUKIZI YA PROFESA HAROUB OTHMAN

HUYO NDIYE HAROUB
Profu Profesa nakwita, kimya shii umeshata
Wapi tutampata, wa namnayo kwa chapa?
Komredi twatafuta, mwenzetu wapi kapita?
Haroub wa Othman, utakumbukwa daima

Maendeleo na sheria, elimu lijipatia
Siasa, demokrasia, huko kote lipitia
Vitivo vingi liingia, taluma ajazilia
Usomi hiki na kile, katu sio kile kile

Haki lipigania, wanyonge wanamjua
Demokrasia lililia, Afrika inatambua
Usafi lilipalilia, ubaya liutumbua
Usomi sio maskuli, ni kutenda vile vile

Usomi si pesambele, usomi huduma mbele
Usome si kile kile, usomi hiki na kile
Ndio maltiprofeshenale, msomi namna ile
Lipokuwepo Harubu, liyafanya yote hayo

Usomi jamiitaa, uvunguni sio pake
Mkandala shule paa, nyumba enda uezeke
Jamii ipe kupaa, wanyonge na wainuke
Angekuwepo Harubu, nahaya angeyasema

Usije kuone tope, msomi ulikalie
Usije kuziba kope, motoni waungulie
Sije geuka upande, haki zao chukuliwe
Angetoa kawosia, nahaya angeyaamba

Huyo ndiye Harubu mapumzikoni
Haji hasauhuliki vitabuni
Nauliza nyi wasomi wa nchini
Mwafanyani mkumbukwe Tanzaniani?

Usomi pesambele na makelele?
Wasomi waibia wala matembele?
Uige vyake Harubu vipaumbele
Yani huduma mbele na utu mbele

© Immaculate Dominic

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP