Loading...

Wednesday, August 18, 2010

Mazungumzo ya Tanzania Njema Yaanza Rasmi!

Wazungumzaji Wakisikilizana
(Kutoka Kushoto: Fancy Nkuhi, Zitto Kabwe na Omar Ilyas)

Washiriki wakifuatilia Mazungumzo

Wadau wakijumuika katika Iftar
------------------------------------------
Mfululizo wa Mazungumzo ya Tanzania Njema umeanza rasmi Jumapili iliyopita. Mazungumzo haya yanaratibiwa na Taasisi ya Tanzanianjema. Washiriki mbalimbali hususan vijana walijumuika pamoja siku hiyo katika Mkahawa wa Vitabu wa Soma kuzungumza na wanasiasa vijana kuhusu changamoto wanazozipata katika medani ya siasa na hasa katika harakati zinazoendelea za uchaguzi. Wanasiasa waliotoa uzoefu wao ni Fancy Nkuhi, aliyekuwa katika kampeni za kupata nafasi ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM/UVCCM, na Zitto Kabwe ambaye anagombea tena nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA. Mfululuzo wa mazungumzo haya utaendelea, kwa taarifa zaidi tembelea http://www.tanzanianjema.com/

2 comments:

emu-three August 18, 2010 at 9:38 AM  

Tanzania njema itawezekana kabisa kama viongozi wetu wataondoa ubinafsi, na hili linatakiwa lianzie kwenye katiba yetu kwa kuondoa yale yanayokipa chama tawala utawala wote, kama chama kikishinda kiweze kuchukua viongozi wengine kwenye chama kingine, kuongezea nguvu na ushirikiano.
Kuna wahujumu au mafisadi kunatakiwa kuwa na njia ya kuwabana hata kuwafilisi ili kuwe na kuogopa kuhujumu uchumi wa nchi kwa manufaaa ya wachache.
Na kubwa lao ni kuondoa huyu adui rushwa, kwani huyu ananyima haki wanyonge!

Anonymous August 19, 2010 at 10:18 AM  

Tanzania njema itatokana na nchi kuwa na mwelekeo katika mifumo yetu mbalimbali ya kimaisha. Hao viongozi vijana wanaunganishwa vipi kimfumo na watanzania wa kada mbalimbali? je kuna namna ya kuwapata, kuwajenga maadili, kuwakuza katika taasisi zenye itikadi za kizalendo au wanapatikana kwa hulka, hisia za kuigiza kuongoza au hasa kurithishwa kwa namna isiyo rasmi? Mwache Zito Kama alivyo tunamjua na hao ni wachache hata kiganjani hawajai je vijana wengine wana hata hiyo vision ya Tanzania njema? walete hapo kwenye Mkahawa uone kama njozi zao sio zile za kutaka kila mtanzania aendeshe gari kama za vodacom, awe na power tiller hata kama hana namna ya kulihudumia, asomeshe mtoto wake academy au nje ya nchi na asikilize kwa makini na kufuata kama kasuku maelekezo ya kisera toka benki ya dunia, IMF, wahisani na hasa Marekani. Mawazo yakiwa vinginevyo kama nionavyo mimi yanapswa kuwa, basi tusitegemee Tanzania njema toka kwa hao wanasiasa vijana watakaofuatia. Ni mawazo yangu tu mwingine anaweza kuwaza vinginevyo na akawa sahihi kwa mtazamo wake.
Wema (mr.)

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP