Loading...

Tuesday, August 3, 2010

MKUTANO MKUU WA MTANDAO WA VIKUNDI VYA WAKULIMA TANZANIA (MVIWATA) WAANZA

Mkutano Mkuu wa 15 wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) umeanza rasmi leo hapa Mjini Morogoro Katika Ukumbi wa CCT, Kigurunyembe. Mada Kuu ya Mkutano Huu ni 'Soko la Pamoja la Afrika Mashariki: Je, Ni Fursa kwa Wakulima Wadogo?' Hivi sasa mada ya kwanza ndio imeanza kutolewa na Profesa Faustin Bee, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MUCCOBS). Mada hii inahusu 'Changamoto za Soko kwa Wakulima Wadogo'. Muhtasari wa Kiuchambuzi wa mada zinazotolewa hapa utawajia kadri mada zinavyotolewa.

Profesa Issa Shivji akiwasili Mkutanoni, hapa anaonekana akikaribishwa na Mwanachama wa MVIWATA - Mchana huu atatoa Mada kuhusu 'Demokrasia na Wakulima Wadogo'.

Wanachama wa MVIWATA wakijiandikisha tayari kuanza Mkutano - Leo ni Warsha ya Kitaifa na Kesho ni Uchaguzi wa Viongozi Katika Mkutano Mkuu wa Mwaka (AGM).

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP