Loading...

Tuesday, August 31, 2010

Serikali ya Umoja wa Kitaifa au Serikali ya Mseto?

Lifuatalo ni jibu alilolitoa Mwanasheria wa Masuala ya Katiba, Profesa Issa Shivji, kuhusu tofauti kati ya 'Serikali ya Umoja wa Kitaifa' na 'Serikali ya Mseto' kufuatia Referendamu ya Kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar:

Katika mfumo wa vyama vingi, pamoja na ushindani wa kisiasa, inaweza ikatokea kwamba hakuna chama chochote kinafanikiwa kupata viti [vingi vya kutosha] (majority seat) katika Bunge ingawa kimepata wingi wa viti ukilinganisha na vyama vingine. Kwa hivyo kitashindwa kutawala kwa sababu sheria na maazimio ya kawaida yanatakiwa kupitishwa kwa [wingi wa kutosha] (majority) bungeni. Kwa mfano, [mgawanyo] (distribution) wa viti katika bunge la viti 200 ukiwa ni chama A - 80, chama B – 60, chama C – 30 na chama D – 30 hakuna chama chochote kilichopata zaidi ya viti 100. Kwa hiyo, chama A kitaanza kujadiliana (negotiate) na vyama vingine ili kuunda muunganiko (coalition) – serikali ya mseto. Katika majadiliano (negotiations) vitu muhimu ni: 1) kwa kiasi gani wanaweza kukubaliana(compromise) juu ya programu na sera zao na 2) uelewano kuhusu kugawana wizara (share ministries). Mfano wa hivi karibuni wa serikali ya mseto ni Uingereza.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa [SUK] ni tofauti kabisa. SUK inaweza ikatokea katika hali mbali mbali – kwa mfano, katika kipindi cha mpito kutoka mfumo moja kwenda mfumo mwingine – kwa mfano huko Afrika ya Kusini. Ili kuepukana na machafuko ya hali nchini vyama vinakubali, kama kamuafaka, kugawana madaraka (share power) ili hatimaye waweze kujenga imani ya wananchi katika mfumo wa siasa za ushindani (competitive politics). Pia inaweza ikatokea katika hali ya machafuko kiasi kwamba hakuna hata chama kimoja kinaweza kikadai kwamba kina uhalali wa kutosha – yaani legitimacy na walio wengi katika jamii (Kenya ni mfano) au kama Zanzibar, jamii yenyewe imegawanyika takribani sawia (almost equally) – imegawanyika katikati kisiasa au imegawanyika katikati kwa namna mbalimbali ukiachilia kisiasa (split in the middle politically or split along certain lines other than political equally). Katika hali kama hiyo hata ukipata viti vingi kuliko chama kingine bado hukubaliki na karibia nusu ya wananchi (almost half of the population). Katika hali hiyo kutakuwa na migogoro baada ya migogoro na kila mara uchaguzi utavurugika au utakuwa rigged (chakachuliwa) n.k. Kwa hivyo vyama vikuu vinakubaliana kugawana madaraka (negotiate to share power) ili warudishe imani ya watu katika mfumo wa ushindani. Ndio maana, Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) sio muundo wa kudumu bali ni muundo wa serikali ya mpito au temporary (wa muda mfupi). Katika SUK vyama vinayoingia katika seriakali vinakuwa na lengo moja tu – lengo lao ni kuleta mshikamano wa kitaifa ili warejeshe hali ya ushindani na sio uhasama. Kwa hivyo wanaweka programu zao na sera zao kando na wanakubali kuwa na programu moja ambayo wanaona itakubalika na walio wengi (large majority), hususun kuchukua hatua za makusudi kabisa kurejesha amani na utulivu.

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP