Loading...

Tuesday, September 7, 2010

KIJANA NA KURA YAKO 2010: WAKATI NI HUU!

Asasi ya Tanzania Youth Vision Association (TYVA) imezindua rasmi mradi wa kuhamasisha vijana kupiga kura unaoitwa; “KIJANA NA KURA YAKO 2010”. Uzinduzi huo umefanyika Shule ya Makongo jijini Dar es Salaam. Asasi hiyo itaendeleza harakati zake katika shule nyingine za jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani. Pia asasi itaenda kwa vijiwe/kempu vya vijana mitaani kuwahamasisha vijana.

Sambamba na kuwafuata vijana walipo, asasi pia imezindua blogu yahttp://www.kijanakurayako2010.wordpress.com/ na kundi katika mtandao wa kijamii wa Facebook kwa jina la “Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010”.

Mradi huu ni wa kujitolea, unaendeshwa na vijana wenyewe pasi ufadhili wa wahisani ama shirika lolote. Lakini, inashirikiana na mashirika yaliyotoa machapisho ya Elimu ya Mpiga Kura kusambaza kwa vijana.

Tunawahamasisha vijana wote watembelee mitandao na kuchangia kwa habari, picha n.k.

Kijana Jitokeze Kupiga Kura 2010!

Frederick Fussi,

Katibu Mtendaji -Tanzania Youth Vision Association

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP