Loading...

Friday, October 29, 2010

FUATA NYAYO ZA MWALIMU - PIGA KURA YAKO!

SHERIA KUMI KUU ZA UCHAGUZI MKUU KWA MUJIBU WA JENERALI ULIMWENGU NA RAIA MWEMA - MUUNGWANA NI KITENDO

1. Tambua kwamba kura ni silaha takatifu inayokuwezesha kumchagua yule unayeamini kwamba unaweza kumkabidhi sehemu ya maisha yako na ukawa salama. Tumia busara.

2. Jua kwamba ni usaliti kwako mwenyewe na kwa wananchi wengine iwapo utapiga kura kwa misingi ya rushwa. Anayekununua hakuthamini. Kwake wewe ni bidhaa tu, kama maharage.

3. Usiruhusu hisia za ubaguzi wa kabila, rangi, dini, jinsia, au ubaguzi wa aina yoyote nyingine ili utawale uamuzi wako katika kupiga kura.

4. Tenda haki kwa wengine, na pia dai haki yako kutoka kwa wengine. Usimwonee yeyote na wala usimruhusu yeyote akuonee.

5. Watetee na walinde wanyonge na wasiojiweza. Wasaidie ili waweze kutumia haki yao ya kupiga kura.

6. Imarisha uhuru wako na uhuru wa nchi yako kwa kuhakikisha kwamba uchaguzi unakuwa na maana, na kwamba kila kura inayopigwa ina maana.

7. Epuka vurugu, vitisho na ugomvi. Kura ni jambo la raha, si karaha.

8. Kumbuka kwamba amani ni mwana wa haki. Penye haki, aliyeshindwa akubali kushindwa, na aliyeshinda bado atende haki kwa aliyeshindwa.

9. Tambua kwamba uchaguzi unakuja na kwisha, viongozi huja na kuondoka, lakini Taifa na watu wake hudumu milele. Tuliza hamasa, epuka chuki, uwe na ustahimilivu.

10. Hii ni fursa adhimu; ifurahie.

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP