Loading...

Friday, November 5, 2010

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS TANZANIA

Leo Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuwa mshindi katika Uchaguzi wa Rais 2010 kwa 61.17%. Katika uchaguzi huu wapiga kura wapatao 5,276,827 walimpigia kura ikiwa ni takribani 10% ya Watanzania wote. Kiwango hiki cha ushindi kimeshuka kwa takribani 20% ukilinganisha na uchaguzi wa 2005. Uchambuzi wa awali unaonesha kuwa matokeo haya yanadhihirisha kuwa Rais Kikwete ana changamoto kubwa ya kurudisha ari na imani kubwa iliyofanya wapiga kura wamchague kwa kishindo katika uchaguzi uliopita wakitegemea 'Maisha Bora kwa Kila Mtanzania'. Hatua ya awali ya kurudisha hiyo hali, ama uhalali huo wa kuongoza, mioyoni mwa wapiga kura hao ambao hawakumpigia kura safari hii, ni kuunda Baraza la Mawaziri dogo tena lisilo na nyuso tata ambazo wananchi walizikataa kwenye uchaguzi tete huu ama kutokana na utendaji mbovu au tuhuma nzito za ufisadi. Hatua nyingine ni kuhakikisha kuwa Serikali inabana na kupunguza matumizi yake hasa katika kipindi hiki kigumu kinasobabishwa na mtikisiko mkubwa wa uchumi ulimwenguni. Wananchi tumetoa tamko letu katika uchaguzi huu - ni tamko kuu ambalo Rais hawezi kulipuuza katika kusimamia utendaji/uwajibikaji wa Serikali hasa kama anaitakia kweli mema nchi yetu.

Mungu Ibariki Afrika
Wabariki Viongozi Wake
Hekima Umoja na Amani
Hizi ni Ngao Zetu
Afrika na Watu Wake

Ibariki Afrika
Ibariki Afrika
Tubariki Watoto wa Afrika

Mungu Ibariki Tanzania
Dumisha Uhuru na Umoja
Wake kwa Waume na Watoto
Mungu Ibariki Tanzania na Watu Wake

Ibariki Tanzania
Ibariki Tanzania
Tubariki Watoto wa Tanzania

3 comments:

ELIAS JM November 8, 2010 at 5:56 AM  

HONGERA MHESHIWA RAIS KIKWETE KWA KUCHAGULIWA NA WANANCHI KWA MARA NYINGINE KUIONGOZA NCHI YA TANZANIA ! SISI WATANZANIA TULIO HAPA MICHIGHANI TUNAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA AKTIKA UTEKELEAZJI WA SERA NA ILANI ZA UCHAGUZI WA CCM 2010-2015! MWENYEZI MUNGULU AKUJALIE NA AKUTANGULIE WEWE PAMOJA NA BARAZA LAKO LA MAWAZIRI UTAKALOCHAGUA! TUNAOMBA UCHAGUE WALE AMBAO WATAKUANGUSHA NA HATA KUVURUGA,NA KUKITIA DOA CHAMA CHA MAPINDUZI NA SERKALI YAKO KWA UJUMLA! KIPINDI!!!!
UKIJA HAPA MAREKANI USISAHAU KUTUTEMBELEA HAPA MICHIGANI HUSUSANI BERRIEN SPRINGS!!

Anonymous November 8, 2010 at 6:04 AM  

HONGERA SANA MHESHIMIWA DR. JK
KWA KUPATA RIDHAA KUTOKA KWA MUNGU KUPTIA KWA KURA ZA WANANCHI WAZALENDO WA TANZANIA KUWEZA KUIONGOZA KWA MARA NYINGINE NCHI YA TANZANIA!! MIMI NINAKUTAKIA BARAKA TELE KUTOKA KWA MWENYEZI MUNGU, KWAMBA UONGOZI WAKO NA SERIKALI YAKO IFANIKIWE ZAIDI HATA MAADUI WAKO WASHANGAE!
NINACHOKUOMBA TU NI KWAMBA WAPENDE WATU WOTE HATA WALIO KINUME NA WEWE MAANA NDIVYO MAANDIKO MATAKATIFU YANAVYOSEMA!!!
MUNGU BADO ANAKUHITAJI KWA AJILI YA MAENDELEO YA TANZANIA NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA NDIO MAANA UMEPITA KWA HIYO!!KWA HIYTO UWE NA MOYO MKUU MUNGU AMEKUKUBALI!!!ELIAS JM

Anonymous November 8, 2010 at 3:05 PM  

Asante sana kwa ufupisho wa matokeo ya uchaguzi. Changamoto hizo kubwa mbili ni muhimu Rais wetu kuzizingatia na kuhakikisha zinatekelezeka. Mungu Ibariki Tanzania.

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP