Monday, December 13, 2010

Kifo Hakina Huruma: Remmy Ongala (1947-2010)

Mwanamuziki mashuhuri, Dkt Remmy Ongala, ametutoka kimwili jana usiku. Atakumbukwa kwa nyimbo zake zenye ujumbe muhimu kuhusu maisha haya mafupi ya mwanadamu. Vibao hivyo ni pamoja na 'Kifo'; 'Kipenda Roho'; 'Mtaka Yote'; na 'Mama Nalia'. Baada ya kubatizwa na Kanisa la Waadventista Wasabato aliimba nyimbo za Injili vile vile.

"kifo, kifo
siku yangu ikifika eeh
kifo niarifu mapema
niage wanangu
niage familia yangu yote
pesa zangu nizigawanye
zimebaki nizile mwenyewe
kifo nakusubiri kwa hamu
"

- Dkt Remmy Ongala

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP