Loading...

Friday, January 28, 2011

Matokeo ya Kidato cha 4:Tumeikatia Tamaa Elimu!

Salaam wadau wa elimu Tanzania -amani na iwe nanyi! Sijaona jipya kwenye Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 yaliyotangazwa juzi - kufeli bado kunaongezeka tu! Sioni jipya pia katika mijadala na malalamiko achilia mbali maazimio na mipango yetu ya kuinusuru sekta hii mahututi - ni yale yale tu! Sidhani kama nitakuwa mbali na ukweli nikisema kuwa tumeshaikatia tamaa elimu - tumeiacha iende zake kaburini! Sasa tumekubali yaishe na ndio hivyo tupo kwenye hitma ya kifo cha kifikra na kimaarifa cha kizazi hiki - naam kizazi cha kijinga!

2 comments:

Richard January 28, 2011 at 7:03 AM  

Mimi nadhani wazazi wa shule za ukata wanatakiwa kufungua 'class action suit' dhidi ya Wizara ya Elimu kwa kuwadanganya watoto wao watapata elimu. Ni sawa na kuwapa dawa bila kujua side effects zake

Anonymous January 28, 2011 at 9:48 AM  

Si tulisema 'KILIMO KWANZA' badala ya 'ELIMU KWANZA' kwahiyo hao waliokalia ndoo wataenda kulima.
Kwi kwi kwi kwi kwiiiiiii!
Tanzania oyeeeeeeeeeeeeeeeeee.
CCM Oyeeeeeeeeeee.

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP