Loading...

Wednesday, January 5, 2011

Siku 5 Baada ya Rai ya Rais Arusha Kwachafuka!


Polisi na Raia


Najua wapo baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa ambavyo vimepanga mikakati ya kuendeleza malumbano ya uchaguzi na kutaka Watanzania waishi kama vile nchi ipo kwenye kampeni za uchaguzi.Wamepanga wakati wote kutafuta jambo au hata kuzua jambo ili kuwachochea wananchi waichukie Serikali. Wamepanga kuchochea migomo vyuoni na maandamano ya wananchi mara kwa mara. Kwao wao huo ndiyo mkakati wa kujijenga kisiasa ili kujiandalia ushindi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

Nawatanabaisha ndugu zangu myajue hayo ili msipoteze muda wenu muhimu wa kujiendeleza na kugeuzwa kuwa mbuzi wa kafara kwa ajili ya kuendeleza maslahi ya kisiasa ya watu fulani. Kwa jinsi watu hao walivyokuwa wabinafsi na wasivyokuwa na huruma na wenzao, wako tayari kuchochea ghasia bila kujali madhara yatakayowakuta watu watakaoshiriki. Wao hasa wanachotaka ni ghasia kutokea na vyombo vya dola kuingilia ati waiambie jumuiya ya kimataifa jinsi Serikali yetu ilivyo katili. Nawasihi ndugu zangu msiwasikilize wala kuwafuata wanasiasa hawa.

Nawaomba, wakiwafuata wakumbusheni kuwa wao wanazo fursa nyingi za kusema wayatakayo Bungeni na kwingineko, waache kuwatumia kama chambo au wahanga wa maslahi yao.

2 comments:

Emmanuel January 5, 2011 at 11:20 PM  

Ni ajabu na nusu kuona Polisi Tanzania wamegeuka mbwa wa kutumwa tu na hata aibu hawana. Inasikitisha sana lakini dawa yao ipo. Siku wananchi wakiamua kuwaadhabisha mmoja. watajua kuwa wao nao raia

Anonymous January 6, 2011 at 8:17 PM  

He jamani, mbona kwenye picha inaonyesha kana kwamba polisi wanapigana na majambazi, loh! inasikitisha sana, mbona chama kile kingine walivyoandamana hawakupigwa, au kwasababu wale walishaungana.EEE Mungu ee,Ibariki Tanzania.

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP