Loading...

Monday, February 28, 2011

MHESHIMIWA RAIS NDIO TATIZO LA UMEME MMELIKUTA - MTALIACHA HIVYO MKITOKA?

IFUATAYO NI SEHEMU YA HOTUBA YA RAIS:

Hali ya Umeme

Ndugu wananchi,
Jambo la nne ni hali ya umeme. *Kama mnavyofahamu, hali ya upatikanaji wa umeme nchini ni mbaya. *Chanzo cha matatizo ni kupungua sana kwa maji katika Bwawa kubwa la Mtera. * *Hadi jana kina cha Bwawa hilo kimeshuka hadi kufikia mita 691.25 ambacho ni pungufu kwa mita 7. *Kwa sasa zimebaki *mita 1.25 tu juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme.

Tarehe 15 Februari, 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa TANESCO wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme. *Baraza limeitaka Bodi na Menejimenti ya TANESCO kuhakikisha kuwa mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi. *Aidha, imesisitizwa kuwa pamoja na udharura uliokuwepo sheria na taratibu za manunuzi ya umma vizingatiwe. *Pia, wahakikishe kuwa mkataba wataoingia uwe ni wenye maslahi kwa taifa. * Vile vile, watoa huduma wawe ni makampuni yanayofahamika na yenye sifa stahiki na kuaminika.

Natambua kuwa Bodi na Mejemienti ya Shirika la Umeme, wanaendelea na mchakato wa kupata umeme huo wa dharura kati ya sasa na Julai, 2011.

Ndugu Wananchi;
Tulipopata tatizo kama hili mwaka 2006/2007 tuliamua kuwa tuanze safari ya kupunguza kutegemea mno umeme wa nguvu ya maji kwa kuongeza matumizi ya vyanzo vingine vya nishati. *Mpango umetengenezwa na utekelezaji wake unaendelea. *Tayari umeme wa MW 145 wa kutokana na gesi asilia umeongezwa kwa kugharamiwa na Serikali. Aidha, mwisho wa mwaka huu MW 160 zitaongezeka yaani MW 100 Dar es Salaam na MW 60 Mwanza kwa gharama za Serikali.

Bahati mbaya kutokana na matatizo ya fedha ya kimataifa, wawekezaji wa sekta binafsi wa kuzalisha MW 300 za umeme wa gesi asilia pale Mtwara walijiondoa. *Umeme huo ungekuwa tayari umeshaingizwa katika gridi ya taifa hivi sasa na kuondoa tatizo la sasa. *Wawekezaji wengine wamepatikana na mazungumzo yanaendelea vizuri. *Mradi wa Kiwira umecheleweshwa na mchakato wa kubadili milki na kupata mkopo wa dola za Marekani 400 milioni za kuwezesha ujenzi wa kituo cha kuzalisha MW 200. *Suala la kubadili milki limefikia ukingoni na mchakato wa kupata mkopo unaendelea kwa matumaini. *

Ndugu Wananchi;
​Waswahili wana msemo usemao “jitihada za mwanadamu hazishindi kudra ya Mwenyezi Mungu”. *Bahati mbaya sana tatizo la ukame limetukuta tena wakati mipango hiyo haijakamilika. *Miaka miwili ijayo hali itakuwa tofauti sana kwani miradi hii na mingine kadhaa itakuwa imekamilika na kulihakikishia taifa uhakika wa umeme.
*
Naomba ndugu zangu muelewe kuwa miradi hii huchukua muda kukamilika. *Mitambo huchukua muda kutengenezwa na ujenzi wa kituo nao pia. *Ingekuwa ni mitambo ya kununua tu dukani tungefanya hivyo na kulimaliza mara moja tatizo hili. *Tena lingeisha zamani na wala sisi tusingelikuta. *Subira yavuta heri.

CHANZO: HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWA WANANCHI, 28 FEBRUARI, 2011

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP