Loading...

Monday, February 14, 2011

Hatma ya Barabara ya Kaskazini ya Serengeti Imeshaamuliwa bila Mjadala wa Ripoti ya EIA?

Ripoti ya EIA ya barabara ya Serengeti (kama ndiyo ripoti rasmi) inachanganya na inatoa tahadhari kuwa kuna hatari ya vitu na matukio fulani kutokea baadae ambayo si mazuri kwa hifadhi na uendelevu wa maliasili/rasilimali ya Serengeti (fuatilia: http://news.mongabay.com/2011/0210-hance_serengeti_road.html). Pia tukiangalia lugha inayotumika, inaelekea kuwa uamuzi wa kujenga barabara hiyo ulishafanyika siku nyingi tu.

Pia najiuliza, kwa nini mamlaka husika hazichukui hatua za kuujulisha umma (open and informed public communication) na kuutoa wasi wasi uliopo . Tuone hizo ramani, barabara itapitia wapi, idadi ya wakazi watakaoguswa na suala hili sehemu zote ambapo barabara (z)ita pita, matatizo na machungu ya wananchi wa maeneo husika tuoneshwe n.k. maana si wote tumefika huko na wala kuyajua yote kwa undani. Uwazi unasaidia kuondoa mashaka!

Ni ukweli kwamba maendeleo wakati mwingine yanaleta migongano na kusababisha kufanyike uamuzi mgumu ama mzito lakini vigezo vyote na njia zote lazima ziangaliwe. Mwalimu Nyerere aliyaona haya na alifanya maamuzi magumu. Tujikumbushe yaliyomo katika Manifesto ya Arusha (Sera ya Wanyamapori ya Tanzania 1998) ya 1961 na nakuu maandiko yafuatayo -

" The survival of our wildlife is a matter of grave concern to all of us in Africa. These Wild creatures amid the wild places they inhabit are not only important as a source of wonder and inspiration but are an integral part of our natural resources and of our future livelihood and well-being.

" In accepting the trusteeship of our wildlife we solemnly declare that we will do everything in our power to make sure that our children's grandchildren will be able to enjoy this rich and precious inheritance.

" The conservation of wildlife and wild places calls for specialist knowledge, trained manpower and money and even look to other nations to co-operate in this important task - the success or failure of which not only affects the continent of Africa but the rest of the world as well.

Mwalimu na wenzake waliyaona haya na walijua kuwa kutatokea masuala kama haya na kutoa rai kwamba tutafute njia zote na misaada yote ili kuwezesha kuhifadhi na kuitumia vema maliasili yetu. Aliona kwamba hili si tu suala la maendeleo ya sasa ama ya leo, ni vile vile ya baadae, na ya watu wetu wa baadae. Tusipoteze dira kwa kusema huu ni mgongano kati ya uhifadhi na jamii au watu fulani, tuangalie pande zote (japokuwa inawezekana kabisa kuwa huu ni mgongano kati ya uhifadhi/maendeleo endelevu na watu fulani fulani!).

Nikijaribu, kwa mfano, kuangalia tena ile 'ofa' ya Benki ya Dunia ya kusaidia kujenga barabara ya kupita kusini mwa Serengeti ingeweza kukubaliwa na kuwasaidia waishio huko, na bado tutafute njia nyingine za kuwafaidisha wale waishio maeneo yaliyopo kaskazini au mbali na huduma muhimu na masoko. Kwa nini tunatumia njia ya "either/or'? Haiwezi kuwa vinginevyo? Kwa nini tusikae pamoja, kama alivyosema Mwalimu katika Manifesto ya Arusha na tutumie utaalamu wetu na juhudi zetu zote (ndani na nje) kuyawezesha yote yafanikiwe?

Ni kweli kabisa lazima tuangalie manufaa ya wananchi/raia wetu, na hasa kama hawa ambao wamepigwa chenga na maendeleo kwa muda mrefu, lakini pia ni busara kuangalia jinsi ya kutunza rasilimali ambayo ina uwezo wa kuwasaidia kiendelevu raia hao hao, sasa na baadae.

Mradi huu unatia wasi wasi kuwa henda ziko agenda za ziada, sijui. Lakini natumaini hiyo ripoti itajadiliwa wazi na watu watapewa muda wa kutosha wa kuisoma na kuijadili, pamoja na kwamba mamlaka kuu zimeonesha kwa maneno na vitendo kuwa penda usipende barabara hiyo itajengwa tu. Sawa ijengwe, lakini baada ya kutafuta 'best possible alternative/option.'

Swali lingine la kujiuliza, nini maana ya kuwa na Idara zinazosimamia taratibu za EIA au kujiwekea taratibu za EIA na serikali yenyewe kuzikwepa? Nikijaribu kusoma 'alama za nyakati' inaelekea huenda pasiwe na nafasi ya mjadala rasmi tena juu ya suala hili, na hivyo kupoteza nafasi ya kutafuta muafaka mzuri kwa pande zote.

Najiuliza, je huu ni mgongano wa maamuzi ya kitaalam dhidi maamuzi ya kisiasa n.k.? Ni wazi pia ni maamuzi yanayofanywa na rika lililopo hapa sasa dhidi ya marika yanayokuja. Tumetafakari kupatikana kwa manufaa kwa marika yote?

Tuyatafakari.

Sina zaidi kwa leo [...] nilipenda tu kuyawasilisha haya kwako na tutafute nafasi ya kuyajadili kwa mapana na busara, bila jazba. Maliasili ni yetu na nchi ni yetu.

Wasalaam

[Mdau wa Rasilimali/Maliasili Zetu]

2 comments:

Temu, A.B.S February 17, 2011 at 3:15 AM  

What I really struggle to understand, most decisions and when challenged, the government and decision makers all they know is to muscle in!

Why can't we learn to debate and see the pros and cons in the open as opposed to doing things under tables and creating all the pa-lavas?

Kwanini tunakuwa WABISHI na WABABE wakati maswala ya nchi ni yetu wote na athari au manufaa yake ni kwa nchi ?

Huu UJENZI ile noise tuu ni disturbance to the nature. Hizo barabara za kati ni kweli zinasumbua lakini kwa kuingia ndani zinatakiwa bado ila lazima traffic iwe controlled. Maendeleo sio kuvuruga.

Ile njia ya kwenye Rombo kupitia Marangu ndio utajua UHARIBIFU kwa jina la maendeleo. Ukitembea duniani ndio utaweza KUJUA how beatiful our country sides in Tanzania are, and we are busy demolishing our greens and trees in the name of maendeleo! Huku ni kufilisika kimawazo na kwa wale viongozi ni ubabe usio na faida kijamii wala KITAIFA.

Mfano pale kwenye Rombo, ukiuliza why not putting tarmac on the same road which was there before and wide enough, wanasema ni gharama. Sasa gharama gani ni kubwa KULIKO lifelihood ya watu na vizazi? Mababu na mababu walitunza hadi leo tumekuta and we ought the same to future generations.

Temu, A.B.S February 17, 2011 at 3:15 AM  
This comment has been removed by the author.
Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP