Loading...

Thursday, March 24, 2011

Prof. Mahuna Kulikoni Mti wa Babu wa Loliondo?

Yu wapo Profesa Mahuna ambaye amebobea katika tafiti za tiba za mizizi/miti kama huu mti ambao Babu wa Loliondo anautumia? Kwenye mtandao kuna taarifa chache sana kuhusu Profesa huyu mahiri! Itakuwa vyema kama wadadisi wa mambo tutaweza kupata mada na makala mbalimbali za Profesa R.L Mahuna pamoja na maandiko ya shahada zake za Uzamili na Uzamivu. Zifuatazo ni dondoo, rejea na nukuu chache ambazo Udadisi imeziokoteza mtandaoni:

"Shughulikeni kwani bado kuna vitu vingi ambavyo dunia haijui lakini sisi tumevifanya kama mazoea tu. Kina Prof mahuna na zile dawa zetu nk ni vitu ambavyo havijulikani ... kwani kitu kama massage ya tumbo (kutufiwa) wakati linauma .. Tiba ya Mburathi (kimeta?) na Kirie (Cancer) wapare walikua navyo ni vile tu miti na majani yamepotea au wajuzi wamekufa nao.." - Yassin Mshana, 4 Oktoba 2010

"M., Magingo, F.S., Minja, A.N., Bitanyi, H.F. & Mahuna, R.L. Plant Genetic Resources and Biotechnology. Proceedings of the first national workshop held at Arusha, Tanzania, January 16 - 20, 1990" - Literature and References

"...Vuguvugu la tiba asilia lilianza kuibuka tena mwaka 2002 wakati Bunge la Jamhuri ya Muungano liliporidhia na kupitisha sheria Na.23 ya Tiba Asilia Mbadala ambapo Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alimteua Profesa Rogasia Mahuna kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asilia Tanzania...mbali na kuwa mwenyekiti wa Baraza hilo, Profesa Mahuna pia yumo katika kundi la wataalam wanaowashauri marais wa nchi 12 za Afrika juu ya matumizi ya Tiba Asilia na pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asilia barani Afrika" - Maishani

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP