Loading...

Thursday, March 31, 2011

Udadisi Kutinga Clouds FM Leo Kujadili Loliondo

Mwanaudadisi atajumuika na wadau wengine kwenye redio ya Clouds FM http://www.cloudsfm.co/ katika kipindi cha asubuhi cha Harakati za Kutafuta Tiba kujadili suala la huduma ya Babu wa Loliondo na masuala mengine husika. Kwa mujibu wa waandaaji wa kipindi hiki, kitakuwa kinalenga zaidi katika "kupata maelezo ama taarifa sahihi kuhusiana na kupata tiba sahihi ya Ukimwi ugonjwa ambao umeitikisa Dunia kwa miaka kadhaa sasa". Mjadala huu unatarajiwa kuanza saa kumi na mbili na dakika arubaini, yaani saa moja kasorobo, asubuhi (12:45ASB/6:45AM) kwa masaa ya Afrika Mashariki. Wadau wengine wanaotarajiwa kushiriki ni pamoja na Dkt. Bwijo Bwijo - Mratibu wa Mfuko wa Kimataifa wa VVU/UKIMWI na Malaria wa Komisheni ya UKIMWI Tanzania (TACAIDS); Nuru Hangachalo - Mtoa Tiba za Asili, Mwenyekiti wa Chama cha Tiba ya Asili Tanzania (ATME) na Kamishna wa Komisheni ya Utafiti wa Tiba za Asili; Joanne Chamungu - Mwenyekiti wa Women+, Mtandao wa Wanawake wanaoishi na VVU; Dkt Emmanuel Kandusi - Mkurugenzi wa Kituo cha Kuhamasisha Haki za Binadamu (CHRP), na Dkt Bennet Fimbo - Mtaalamu wa Kutoa Elimu ya Umma kuhusu Kuzuia Maambukizi ya VVU pamoja na Huduma na Tiba kwa Watu Wanaoishi na VVU.

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP