Tuesday, April 12, 2011

ALIYOYASEMA EDWARD MORINGE SOKOINE

Ndugu Edward Moringe Sokoine (01/08/1938-12/04/1984) alikuwa Waziri Mkuu wa aina yake nchini Tanzania. Aliongoza katika kipindi ambacho nchi ilikuwa katika hali ngumu sana ya kiuchumi. Leo ni miaka 27 toka Taifa limpoteze shujaa huyu. Katika kuenzi fikra zake ambazo bado zinahitajika sana leo, Udadisi inakuletea nukuu zifuatazo kama ilivyozipata kutoka kwenye Kitabu cha Edward Moringe Sokoine: Kiongozi wa Watu Aliyejitolea kilichoandikwa na Luteni Kanali Albert N. Kigadye mnamo mwaka 1984:

"Ole wake kiongozi mzembe na asiye na nidhamu nitakayemkuta: Kiongozi wa siasa hana usalama wa aina yoyote. Usalama wake ni kudra ya Mungu na Wananchi peke yake. Viongozi wazembe na wabadhirifu wahesabu siku zao. Labda tusiwajue. Hawa hatuna sababu ya kuwapa imani, kuwa tutawalinda kama vitendo vyao viovu" - Edward Moringe Sokoine, 26 Machi 1983

"Juu ya suala hili la mapato kutolingana na matumizi ni kwamba tungependa kupunguza uongezaji wa wataalam wasiohitajika katika Serikali na katika mashirika ya umma mpaka hapo hali yetu ya uchumi itakapokuwa katika hali nzuri" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1982

"Serikali inasimamia bei, lakini Serikali yetu itakwenda mpaka itasimamia bei ya mhogo, dagaa na bei ya kila kitu? Haiwezekani, vitu vingine ni lazima vizalishwe kwa wingi ili bei yenyewe iweze kujirekebisha" - Edward Moringe Sokoine, 24 Septemba 1983

"Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa" - Edward Moringe Sokoine, 4 Oktoba 1983

"Vijana leo wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanae, 'mali hii umeipata wapi?'" - Edward Moringe Sokoine, 23 Oktoba 1983

"Katika nchi inayojali haki na usawa, majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi. Na kamwe hayaruhusiwi kuwa ni chombo cha wachache wenye kujali nafsi zao na kusahau maslahi ya walio wengi" - Edward Moringe Sokoine, 1Februari 1977

17 comments:

sisulu December 2, 2011 at 5:43 PM  

alikuwa mtu wa MUNGU aliyeletwa kusaidia watu wa MUNGU.

Anonymous December 19, 2011 at 9:06 AM  

Kwa maneno aliyosema hapo juu alishajiweka hatarini

Anonymous July 19, 2013 at 12:46 PM  

Jamaa hakika alikuwa ndiye rais tuliyemhitaji sana, tena nyakati hizi

Anonymous April 12, 2014 at 11:00 PM  

Alikuwa mkweli mpenda haki hakuwa kigeugeu kama mnafiki na woga aliutupa pembeni sana.

Anonymous April 12, 2014 at 11:16 PM  

itachukua muda sana kupata viongozi waadilifu kama EDWARD MORINGE SOKOINE!

Anonymous April 13, 2014 at 1:10 PM  

Never shall we get such a person!

Anonymous February 22, 2015 at 4:57 PM  

Hao ni viumbe ambao walikuja kwa wakati maalum haitowezekana kuwapata watu kama hao

Anonymous June 1, 2015 at 12:10 PM  

Kwa hakika Tanzania ya leo inahitaji kiongozi mwenye uthubutu.Anonymous June 1, 2015 at 12:11 PM  

Kwa hakika Tanzania ya leo inahitaji kiongozi mwenye uthubutu.Anonymous June 6, 2015 at 1:36 AM  

alikuwa na kauli nzito sana...sasa hivi hazipo tena

Anonymous November 24, 2015 at 7:09 PM  

Ndivyo ilivyo Mtu mzuri hawezi kuishi muda mrefu.
Soma maandiko haya; Zaburi 146:3-5

salumu ngayonga November 25, 2015 at 3:43 PM  

Hahaha mungu mlaze pema

salumu ngayonga November 25, 2015 at 3:43 PM  

Mungu amlaze pema

WINNER MOHAMED April 12, 2016 at 6:40 PM  

Moringe ndio magufuri Wa Leo mwendo Wa magufuli ndio nyayo za marehemu Edward sokoine

Anonymous July 12, 2016 at 12:30 AM  

Mimi nadhani tufike mahali tuelewane kwamba, nchi haitakiwi kuongozwa kwa akili za mtu binafsi, bali, tufuate misingi ya Katiba ambayo ndiyo sheria mama. Nchi ni kama chombo kilicho hai na kina mfumo kamili wa uhai wake.Kama chombo kinatumia petroli, kila rubani anayekabidhiwa atumie petroli asiweke ubunifu wake binafsi la sivyo injini ambayo watu wengi waliisha ikubali yaani (KATIBA) haitakuwa na maana. Kuibuka kwa viongozi mashujaa ni tafsiri kuwa watangulizi walilegeza mambo fulanifulani katika mfumo wa chombo.

Anonymous October 14, 2016 at 12:44 PM  

Hakika alikuwa kiongozi wa watu.lakini Mungu hajatuacha wakiwa kwa kutupatia Magufuli.
Magufuli hana mfano wake. Mungu amejibu maombi ya watanzania na waafrika kwa ujimla wetu.

Anonymous December 26, 2016 at 8:13 AM  

Sokoine kafufukia chato...asante mungu

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP