Loading...

Wednesday, June 15, 2011

WASOMI CHUO KIKUU WANAPOTISHIWA CHUI!

Ufuatao ni ushauri uliotolewa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam Kuhusu Tetesi za Uwepo wa Chui katika Maeneo ya Kampasi ya Mlimani:

Chui ni mmoja wa wanyama wa jamii ya paka na ni mnyama hatari. Pamoja na hayo chui ni
msiri sana na jamii inaweza kuishi na chui sehemu moja kwa muda mrefu bila watu kufahamu kuwa yupo. Hii ni kwa sababu chui huwa wakati wote anawakwepa watu na sio kawaida yake kushambulia watu. Aidha kila aina ya mnyama ana umbali ambao akiona mtu au mnyama mwenzake au hatari yoyote basi ana utashi wa kuamua kukimbia au kushambulia. Umbali huu kitalaamu unajulikana kama “flight distance”. Umbali huu wanyama hujiwekea miongoni mwao na pia unahusu umbali ambao mnyama anaweza kukimbia hatari . “Flight distance” kwa hiyo hutofautiana baina ya wanyama na pia kwa mnyama mmoja inaweza kuwa tofauti kutegemea na mazingira. Endapo mnyama atamuona mtu akiwa karibu zaidi ya “flight distance” anaweza kudhani kuwa mtu huyo alikuwa anamvizia kwa lengo la kumshambulia; hivyo anaweza kushambulia kwa kujihami ingawa mtu aliyeshambuliwa ataona kuwa ameshambuliwa kwa makusudi na huyo mnyama. Watu wanashauriwa kutomchokoza chui endapo watakutana naye. Inashauriwa pia kuwa ukikutana naye kwanza kwa haraka soma mazingira na ukiweza muangalie usoni ili umsome malengo yake na mara nyingi chui ataacha kukuangalia na atakimbilia porini kwani ana kawaida ya kuona aibu. Uamuzi wa mtu kukimbia inabidi uchukuliwe kwa tahadhari sana kwani unaweza kumfanya chui aanze kumfukuza mtu ambaye mara tu baada ya kuonana anaanza kukimbia. Pia endapo chui ana watoto watu wasiwakaribie kabisa watoto na endapo watoto wa chui kwa vile ni watundu na wanapenda sana kucheza na kila mtu wanaweza kumkimbilia mtu basi ni vizuri mtu huyo kuwakimbia maana mama yao atashambulia bila kutoa tahadhari yoyote endapo ataona mtu amewakaribia watoto wake na bila kujali kuwa watoto wa chui ndio watakuwa wamemkimbilia huyo mtu.

Soma Taarifa Kamili Hapa: http://groups.yahoo.com/group/Wanazuoni/message/9742

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP