Loading...

Monday, July 25, 2011

An Enanga Performance/Maonyesho ya EnangaINVITATION TO AN ENANGA PERFORMANCE AND DISCUSSION

Two enanga performers from Kagera Region who are currently in Dar es Salaam attending the international Ethnomusicology Symposium at the University of Dar es Salaam have kindly agreed to stage a live performance for fans and patrons at the Soma Book Café on Tuesday, 26/7/2011, from 6:00 to 8:30 p.m. All interested individuals and groups are kindly invited. There will be no entrance fee, but patrons may make small voluntary donations to the bards in appreciation of their work. Performances will be interspersed with discussions on the enanga tradition and other Kagera and Tanzanian music traditions.


The discussions will be coordinated by the distinguished enanga scholar, Prof. M.M. Mulokozi.

As usual drinks and other refreshments will be on sale at the Café counter and the bookshop will be open. Kindly help make the occasion a highly sociable, educational and enjoyable event by your attendance.


NOTE Enanga is a musical instrument – a trough zither used in the Lake Region and elsewhere in epic and song performance. The term also denoted such performances.


MWALIKO WA KUHUDHURIA MAONYESHO NA MAJADILANO YA SANAA YA ENANGA Wasanii wawili wa muziki wa nanga kutoka Mkoa wa Kagera ambao wako Dar s Salaam kuhudhuria Kongamano la Muziki wa Asili linalofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam watafanya maonyesho ya muziki wao siku ya Jumanne, tarehe 26/7/2011, kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2:30 katika viunga vya Mkahawa wa Vitabu, Soma, Regent Estate Na 53, Dar es Salaam. Vikundi na watu binafsi wanakaribishwa kushiriki. Utendaji wa nanga utaambatana na majadiliano na maelezo kuhusu muziki wa asili wa Kagera na Tanzania kwa jumla. Hapatakuwa na kiingilio ila wateja wana hiari ya kuwatunza wasanii hao wakati wa utendaji. Majadiliano yataratibiwa na mwanazuoni mashuhuri wa enanga, Prof. M.M. Mulokozi.


Kama kawaida, vinywaji na viburudisho anuwai vitauzwa Mkahawani na duka la vitabu litakuwa wazi.


MUHIMU Enanga ni ala ya muziki inayotumika katika Ukanda wa Ziwa na kwingineko wakati wa kuimba tendi na fani nyingine za nyimbo. Wimbo unaoimbwa kwa kutumia ala hiyo vilevile huweza kuitwa enanga.


Demere Kitunga


E&D Readership and Development Agency—Soma Contacts: info.soma@infinet.co.tz P.O. Box 4460 Dar es Salaam Tel: 022 2772759 Location: Mlingotini Close, Plot No 53 Regent Street, Regent Estate

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP