Loading...

Thursday, July 21, 2011

KAMALA: BAA LA NJAA KAGERA!

Baa la Njaa Mkoani Kagera: Chakula Kitatoka Wapi? Mbona Serikali Iko Kimya?

Kamala J Lutatinisibwa

Ni hatari kwa mustakabali wa chakula na utamaduni kwa Mkoa wa Kagera ambao chakula chao kikuu ni ndizi na hata tamaduni za wanyeji wa hapa huendana na ndizi na kahawa.

Hali si shwari tena, migomba inaumya, kuna kirusi cha kushambulia migomba maarufu kama mnyauko, kimekausha migomba kwa kuishambulia, haijulikani kimetokea wapi lakini migomba imeathiriwa kwa kiasi kikubwa.

Ugonjwa huu hukausha mgomba mzima, hushambulia kwa kasi, katika kata ya Kashanda wilayani Muleba, nimeshuhudia mashamba yakiwa matupu kutokana na ugonjwa huu huku migomba michache iliyobaki ikizidi kunyauka kwa kasi ya kutisha. Hali hii inaathiri uchumi na afya za wakazi wa maeneo ya mkoa huu. Wilaya za Muleba, Karagwe, mMisenyi na Bukoba zinazidi kuathiriwa kwa kasi ya kutisha.

Serikali iko kimya, wabunge wako kimya na hata serikali za wilaya hazionekani kujishughulisha kwa lolote. Baya zaidi ni kuwa hata asasi za kiraia ziko kimya. Njaa kali imeanza kuwaathiri wakazi wa mkoa huu huku baadhi ya wanasiasa wakidai hamna tatizo la chakula hapa.

Chanzo cha ugonjwa huu hakijulikani, kuna wanaodai unatokana na miti ya mi-pine iliyopandwa kwa kasi lakini wengine wanadai ilitokana na na sumu iliyomwagwa ziwa Victoria kuuwa magugu maji.

Baya zaidi ni kuwa wakazi wa mkoa wa Kagera hawana utaratibu wa kulima nafaka wala kutunza mazao kwani ndizi ni chakula cha kutegemewa kwa mwaka mzima, sasa mambo yamegeuka, ndizi hukatwa na kuchomwa moto kama njia mojawapo ya kukabiliana na ugonjwa huu japo kuwa haisaidii chochote.

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP