Loading...

Tuesday, August 2, 2011

KISWAHILI OR/AU SWAHILI?

What follows is Mobhare Matinyi's critique of the use of the term 'Kiswahili' instead of 'Swahili' in the English language /Ifuatayao ni hoja ya Mobhare Matinyi dhidi ya matumizi ya neno 'Kiswahili' badala ya 'Swahili' katika lugha ya Kiingereza:

When one communicates in English, the name of our language is not Kiswahili, for God’s sake; it’s Swahili. Kiswahili becomes the name when we communicate in Swahili. That’s it!Kwenye mawasiliano ya Kiingereza lugha hii huitwa “SWAHILI,” basi!

Ni nchini Kenya ndiko kuna uzembe wa kukiita Kiswahili hivyo hivyo hata wanapowasiliana kwa Kiingereza; ni sawa kwao, kwani hii si lugha yao. Lakini kwa Mtanzania kukiita Kiswahili eti “Kiswahili” hata kwenye mawasiliano ya Kiingereza, ni ujuha.

Lugha zina majina yake, na huwezi kujichanganyia tu kama mtu anayepika chakula cha Irio cha Wakikuyu ama Matoke kwa Waganda au Pure kwa Wapare. Kwa muundo wake, Kiingereza hakiwezi kutumia kiambishi awali cha “Ki-“ ili kujenga jina la lugha.

Ni sisi Waswahili ndiyo tuna muundo huo, mathalani tunaposema Kiarabu ama Kikurya ama Kinyasa. Ukichukulia kwa mfano, lugha za Kibantu za Waganda, wao huita lugha ya kabila lao kuu la Waganda, kuwa ni “Luganda.” Hii ina maana neno mzizi ni “-ganda” na kiambishi awali “Lu-“ kinamaanisha “lugha ya -.”

Ukichukua Kikurya mathalani, kinatumia kiambishi awali “Ghi-“ ili kuunda jina la lugha; hivyo wakati Waganda wanastahili (hata kama hawafanyi hivyo) kukiita Kiswahili “Luswahili,” Wakurya wanastahili kukiita “Ghiswahili” na ndivyo wanavyofanya.

Kwa mantiki hii basi, swali linakuja, Waingereza wao wanafanyaje? Jibu ni kwamba kwa lugha za Kibantu wanachukua mzizi wa neno na kuutumia kama jina kamili; hawana kiambishi awali cha kuundia jina la lugha. Hii ndiyo sababu Kiswahili huitwa SWAHILI, Kizulu huitwa ZULU, Kihausa huitwa HAUSA, Kitigrinya cha Eritrea huitwa TIGRINYA, n.k.

Kwa kuheshimu majina ya lugha, ndiyo maana pia Wafaransa huiita lugha ya Wajerumani ALLEMAND, wakati Waingereza wao huiita GERMAN, Waswahili tunaiita KIJERUMANI, na wao wenyewe Wajerumani wanaiita DEUTSCH. Lugha zina majina yake; siyo kutwanga tu.

Source: The Citizen (28 July 2011) and Majira (31 July 2011) Respectively

Photo: http://osx-e.org/img/rosetta-stone-v2-swahili-level-1_182747_500.jpg


0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP