Loading...

Wednesday, September 28, 2011

I WAPI RIPOTI YA NEMC KUHUSU BARRICK NORTH MARA?

Mdadisi anauliza: I wapi ripoti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Tanzania kuhusu matatizo ya kimazingira na kijamii katika mgodi wa dhahabu wa North Mara uliowekezwa na Barrick? Inasemekana kuwa ripoti hiyo ilikamilika toka mwezi Julai 2011! Pia inasemekana kampuni hiyo ya kiwekezaji imeshalishughulikia ipasavyo suala la kimazingira na kuwa kilichobaki ni kutatua kikamilifu tatizo la kijamii. Wadadisi wa mambo na wananchi kwa ujumla wana haki ya kujua utekelezaji wa matatizo hayo ambayo, kimsingi, yanaendeana umefikia wapi na nini hasa chanzo chake kwa ujumla ili kuzuia yaliyowahi kuripotiwa kupitia CALL FOR ACTION IN NORTH MARA GOLDMINE na WHEN BARRICK GOLD'S CAPITAL COMES DRIPPING WITH BLOOD AND DIRT! yasijitokeze tena. Kinga ni bora kuliko tiba.
---
Picha:

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP