Loading...

Monday, September 19, 2011

Mjadala Mkali wa Ushoga na Tamasha la Jinsia

Mjadala mkali unaendelea katika mtandao wa wazi wa http://groups.yahoo.com/group/wanazuoni/ kuhusu uwepo na uwazi wa mashoga katika Tamasha la Jinsia lililofanyika katika viwanja vya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wiki iliyopita. Hiyo hapo chini ni dondoo kutoka kwa mwanamjadala Leila Sheikh alipokuwa akijibu hoja za baadhi ya Wanazuoni waliokasirishwa na kitendo kinachoonekana kuwa ni cha kutetea haki ya ushoga na kuvunja maadili. Unaweza kufuatilia zaidi mjadala huo katika uzi huu: http://groups.yahoo.com/group/Wanazuoni/message/11148. Picha hiyo hapo juu ya baadhi ya washiriki wa tamasha hilo ni kwa hisani ya blogu ya http://francisgodwin.blogspot.com/.

----
Mimi ni Mwanachama wa TGNP na ndiye niliyefanya Mapping ya HIV Intervention among Men who have Sex with Men kwa ajili ya Center for Human Rights Promotion (CHRP) asasi ya kitanzania; TACAIDS na UNAIDS.
Kaka Poa wapo kwenye jamii yetu na tukifumbia macho uwepo wao, huduma ya ujumbe juu ya kijikinga na maambukizi ya [Virusi vya Ukimwi] VVU miongoni mwao haitakuwepo.
Ilikuwa muhimu kufanya Mapping hiyo ili kama taifa tutayarishe mkakati wa kuwafikia hao akina Kaka Poa ambao ninyi mnawaita mashoga; wasenge; kuchu; samaki; n.k. Aidha, wale Kaka Poa wanaoishi na VVU hawatapata huduma ya ARV au ushauri nasaha.
Nilifanya utafiti kwenye mikoa 3 kabla ya Desk Review halafu nikatayarisha ramani itakayoongoza National Strategic Plan on Most at Risk Populations (MARPs).
Kaka Poa ni kundi moja la MARPs.
Hiyo ramani ni mali ya watanzania na TACAIDS ndiyo custodian [...]
Cha muhimu nataka kusema kuwa rasimu ya Marekebisho ya Sera ya Taifa ya VVU/UKIMWI 2001/2010 imeweka kipengele kinachojadili hayo makundi ambayo yamo kwenye mazingira hatarishi (MARPs), wakiwemo Kaka Poa na Dada Poa ambao jamii inawaita makahaba; changudoa; dala dala n.k.
Wakati wa utafiti niligundua kuwa hao Kaka Poa wapo wengi zaidi kuliko tunavyofahamu. Takwimu sahihi hazipo kwa sababu wengi wapo kwenye kificho wengine hata kufikia kuoa kwa kukhofu unyanyapaa kutoka kwa jamii na mara nyingi kupigwa; kutukanwa na kutengwa.
Huyo Zungu ni rafiki yangu. Niliunga urafiki nae wakati nafanya utafiti.
Nataka kuwaambia wanazuoni kuwa Kaka Poa ni binadamu kama sisi.
Wana huruma. Wana haki ya kupata huduma ya afya; elimu; upigaji kura; vyeti vya kusafiri; pango kwenye nyumba; akaunti za benki n.k.
Kwenye utafiti niligundua kuwa iwapo hiyo rasimu ya kupeleka ujumbe na huduma juu ya VVU/UKIMWI kwa Kaka Poa itapita kuwa Marekebisho ya Sera, haitaweza kutekelezeka kwa sababu itakosa uwiano na Sheria ya Makosa ya Kujamiiana (1998) na Penal Code Amendments 2002 kwa sababu kitendo hicho kimehramishwa kisheria.
Hapo hapo, Kaka Poa watakataa kufikiwa na Mipango ya Taifa ya Udhibiti wa UKIMWI kwa kukhofu wanaweza kufunguliwa mashtaka ya jinai.
Nawaomba wanazuoni tuwe na upendo kwa makundi yote.
Nimeshuhudia unyanyapaa; vipigo; matusi ambayo wanayopata Kaka Poa na sisi kama watetezi wa Haki wa kutokomeza ukatili na unyanyapaa inabidi tuwe na compassion.
Leila
---
Kwenye mipango na mikakati ya kudhibiti VVU/UKIMWI hakuna kundi ambalo lipo insignificant kwa sababu sote sisi tuna haki ya kupata huduma ya afya.
Na hayo mashirika yaliyonituma kufanya mapping hayakufanya hivyo kwa sababu ya fedha za wazungu bali mazingira ambayo tunamoishi kwa sasa yamewapelekea kufanya hizo mapping ili kupata mikakati ya kupeleka ujumbe wa udhibiti wa maambukizi ya VVU na huduma kwa wanaoishi na VVU kwa makundi yote nchini.
Kwenye ulimwengu wa ndoto tungependa kuona familia ina baba; mama; watoto; wajukuu wote wakiishi pamoja kwa amani bila ya bughudha au umasikini.
Kwenye ulimwengu wa ukweli, single parents; divorce; break up of family structures; lack of respect to our elders (wengine kufikia kuua wazee kwa tuhuma za uchawi) ndivyo vilivyotawala.
Tunatakiwa tuangalie upya kitu gani hasa kimeleta mfumo huu.
[Leila]
---
Taifa/Mipango ya kudhibiti UKIMWI imeweza kutambua makundi ambayo yamo kwenye mazingira hatarishi yakiwepo- wanaojidunga sindano za dawa za kulevya; makahaba; wanaume wanaofanya ngono na wanaume wenzao; waliopo kwenye migodi; wanaoendesha malori kwenye misafara mirefu na wanaoishi kwenye transport corridors.
Makundi haya yanaitwa Most at Risk Populations (MARPs).
Ili taifa liwe na Mpango wa Udhibiti UKIMWI wenye kuwafikia wanachi wote, hao MARPs imebidi wawekewe mikakati maalum kupitia mitandao yao.
Mbali ya Kaka Poa, mimi ndiye niliyefanya Mapping ya HIV Intervention among Sex Workers/Dada Poa kwa kuongoza timu ya Strategy Mappers wa Afrika Mashariki.
Kamwe sioni aibu kuwa nimefanya Mapping hizo mbili kwa sababu UKIMWI umegusa kila familia; kaya; mtaa; n.k. nchini.
Na huwa tunaita magonjwa yatokanayo na ngono isiyosalama siyo magonjwa ya zinaa kwa sababu wapo wanaoambukizwa ndani ya ndoa.
[Leila]

3 comments:

herie16m September 19, 2011 at 4:37 PM  

Watanzania wenzangu, napenda kuwakumbusha tu kuwa mahusiano ya kimapenzi kati ya watu,iwe wa jinsia mmoja au tofauti, yapo, yalikuwepo na yatakuwepo katika jamii za watu woote ulimwenguni, hata zile ambazo homosexuality ni crime. Tunavyo fumba macho ndio tunaharibu zaidi, kwani watu hufanya hivi kwa kujificha na bila kujali maafa mengine ya kiafya kama matumizi ya mipira nakadhalika kwa ajili ya kuogopa jamii yenye "mwelekeo wa kulia". Nchi nyingi za magharibi wameliacha hili suala wazi, na kidogo kuna mafanikio katika vita dhidi ya magonjwa, lakini hata kidogo sio rahisi kufunga watu kamba shingoni kwa suala la mahusiano.
hii chini ni historia ya homosexuality toka miaka kabla ya Kristu.
http://www.youtube.com/watch?v=TKLeTinSaqM
Heradius, São Paulo- Brasil

Tanganyikan September 19, 2011 at 6:38 PM  

Mwana mimi naamini kila mtu ana haki ya kuchagua aishi maisha ya aina gani, lakini kwa hili nadhani tusitake kuiharakisha jamii yetu kukubaliana na mapenzi ya jinsia moja. Tofauti yetu na magharibi ni kwamba kule kuna watu wa dini tofauti,sisi wengi ni Wakristo na Waislamu ambao wote vitabu vinapinga. Hebu tuchukulie mfano marekani. Imechukua mda mrefu sana hadi baadhi ya mjimbo kutambua haki zao, Nadhani tuwe wavumilivu na tujaribu kuielimisha jamii kwa utaratibu kama tulivyoweza kufanya kwa unyanyapaa wa wagonjwa wa UKIMWI. Nna uhakika tutafika.

Anonymous September 20, 2011 at 4:12 PM  

Msiweke nguvu zenu kwa wanaume wanao jamiiana na wanaume pekee.Waangalieni na wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao ( Wasagaji ). Kwa maoni yangu, wanawake wanao jamiiana na wanawake wenzao nchini Tanzania wapo katika hatari kubwa sana ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kuliko inavyoweza kufikiriwa, hii inatokana na njia wanazo tumia kujamiiana paamoja na mapungufu makubwa yaliyopo katika Sera ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi 2001/2011. Nawapa changamoto hii. Fanyeni utafiti na majibu yenu yatakubaliana na maoni yangu kwa kiasi kikubwa. CIAO

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP