Loading...

Monday, September 26, 2011

Mkapa anaweza Kugombea Urais tena kama Putin?

SWALI LA KIZUSHI:
JIBU:
Kwa ufahamu wangu hili haliwezekani kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingawa linawezekana kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliacha lile neno muhimu "Consecutive" vipindi vya uraisi mtu anavyoruhusiwa kutawala.

Kuhusu uraisi katiba ya Jamhuri inasema a person cannot run for more than two terms wakati ile ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kama zilivyo ya Urusi na nchi kadhaa nyingine inasema a person cannot run for more than two 'consecutive' terms. Na hapo ndipo tofauti ilipo. Kwa Zanzibar, kama ilivyo Urusi, waweza kugombea zaidi ya vipindi viwili mradi tu umpumzike kwa angalau kipindi kimoja hapo katikati. Lakini kwa Jamhuri hakuna namna unayoweza kugombea zaidi ya vipindi viwili, iwe mfululizo au vinginevyo.

Kwa hiyo jibu ni Hapana, Mkapa hawezi kugombea tena uraisi kama Putin kwa katiba ilivyo sasa, kama mchakato wa mabadiliko ya katika hautalibadili hilo.
CHANZO:
PICHA:

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP