Loading...

Friday, September 30, 2011

Watanzania Wajizatiti/Wajidhatiti Twitter!

Watanzania wanazidi kujumuika katika Twitter kujadili masuala mbalimbali!

Mijadala hiyo ina mvuto sana hasa ukizingatia kuwa viongozi wa kijamii, kibiashara na hata kisiasa wanajumuika. Wapo Wabunge (mf. @DocFaustine na @zittokabwe), Wakurugenzi wa Makampuni (mf. @iMashibe na @beyakuze), Wanazuoni (mf. @Mwanasosholojia na @Mwanafalsafa) , Wanamuziki (mf. @mwasitiJ na @Profesa_Jay), Waandishi wa Habari (mf. @kabsjourno na @salvarweyemamu), Watangazaji (mf. @barbarahassan na @nyangorojs)Wanaharakati (mf. @Irenei2011 na @rakeshrajani), Asasi za Kiraia (mf. @Darajatz na @HakiElimu) Mawaziri (mf. @AnnaTibaijuka na @Mnyambi ) - na hata Rais wa Nchi na Mama wa Kwanza (@jmkikwete na @salmakikwete)!

Kwa sasa mijadala mikali inayoendelea ni pamoja na wa #udinitz na #mashoga. Jana kulikuwa na mjadala mkali sana kuhusu #DowansAward ambao bado unaendelea. Hivi karibuni pia kulikuwa na mjadala mkali kuhusu ajali ya meli Zanzibar #ZanzibarBoatAccident . Udadisi ilijiunga rasmi mwaka jana baada ya kusitasita kwa muda mrefu (rejea http://udadisi.blogspot.com/2010/12/twittering-tanzanias-transinformation.html)!

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP