Loading...

Wednesday, November 2, 2011

ANA KWA ANA NA PROFESA MAZRUI AKICHAMBUA UDINI

Leo tulitembelewa na Mwanazuoni Mkongwe, Profesa Ali A. Mazuri. Alikuja kutoa mhadhara kuhusu Uislamu Barani Afrika - Ukuaji, Uamsho na Uchachuaji Wake. Kama kawaida yake aligusia masuala mengi, watu wengi na nchi nyingi. Kuhusu Tanzania/Zanzibar aliusifia muungano kuwa ndio muunganiko pekee wa nchi za Afrika uliobaki na kuitolea mfano nchi yetu kuwa imeweza kuwa na 'ustaarabu' katika miingiliano na migongano ya dini ya Uislamu na Ukristo. Hapa alikuwa anamaanisha kuwa hata tukiwa na migongano ya kidini bado huwa tunaijadili na kujaribu kuitatua 'kistaarabu' tofauti na nchi zingine ambazo zimefikia hatua ya kuwa na machafuko na mapigano ya kidini.

Alipoulizwa kuhusu suala la udini Tanzania na malalamiko ya kihistoria kuhusu upendeleo wa kisiasa na kielimu alisema nchi yetu ilikuwa na afadhali katika hilo kuliko nchi kama Ivory Coast. Hapa alikuwa akimaanisha kuwa pamoja na kuwa nchi zote mbili zilikuwa na Marais wa kwanza Wakristo tena Wakatoliki lakini Tanzania haikufikia kwenye kiwango cha ubaguzi wa kidini katika kutoa nafasi za kielimu na kisiasa ambacho kilifikiwa huko Ivory Coast. Pia alisema mlolongo wa kuwa na Rais Mkristo kisha Muislamu ambao umeweza kufanyika katika awamu nne ni jambo zuri na amejaribu kutoa ushauri huo kwa Nigeria ambayo inakabiliwa sana tatizo la udini katika medani ya kisiasa. Lakini alikiri kuwa kuna umuhimu wa kutatua tofauti hizo za kihistoria ndani ya nchi za Kiafrika ila sio kwa namna ambayo inapelekea jamii fulani ya kidini au kikabila kuilipa jamii zingine kama ambavyo wanadai nchi za Magharibi zizilipe nchi za Kiafrika. Hivyo, changamoto ni kujaribu kutafuta njia mbadala inayofaa zaidi kutatua matatizo na tofauti za kihistoria yanayosababisha kuwe na udini n.k.

Profesa Mazrui pia alitumia muda mwingi kujaribu kutofautisha ustaarabu wa kiislamu na dini ya uislamu. Alitumia mifano ya jinsi ambavyo wazungumzaji mbalimbali wa Kiswahili wamerithi ustaarabu wa Kiislamu katika maneno ya lugha yao japo sio waislamu. Katika kuweka msisitizo alitoa mifano ya maneno mbalimbali ya Kiarabu na jinsi yalivyokuwa sambamba na maneno ya Kibantu kana kwamba kulikuwa na fundi muashi aliyekuwa anajaribu kuhakikisha kuna uwiano fulani. Kwa mfano, majina ya nambari tano za kwanza - yaani moja, mbili, tatu, nne na tano - yote ni ya Kibantu ilhali namba kama ishirini, thelathini na elfu ni ya Kiarabu. Pia maneno 'mashariki' na 'magharibi' yanatokana na Kiarabu wakati 'kusini' na 'kaskazini' yanatokana na Kibantu'. Neno 'Rais' linatokana na Kiarabu ilhali 'Bunge' linatokana na Kibantu. Hali kadhalika neno 'jioni' linatokana na Kiarabu ilhali 'asubuhi' linatokana na Kiarabu. Mfano mwingine alioutoa kama changamoto ni wa neno 'amani' linalotokana na Kiarabu na neno 'vita' linalotokana na Kibantu. Kwa ujumla, alikuwa anajaribu kuonesha kuwa kuna masuala mengi ambayo jamii zimerithi kutoka kwenye ustaarabu wa kiislamu - kama vile mavazi yanayotumika wakati wa kuhitimu shahada za chuo kikuu na numerali - ambayo sio lazima yamfanye mtu awe muislamu na kuna umuhimu wa kulitambua hilo.

Maswali mawili aliyoyaibua ambayo anadai yanapaswa kufanyiwa kazi na watafiti wa historia ya Uislamu na ambayo huwa anawauliza wanafunzi wake ni: (1)Kwa nini Irani na Misri ambazo zilivamiwa na Waarabu katika vipindi vilivyopishana kidogo sana zilifuata mkondo tofauti ambapo Misri iliarabishwa ilhali Irani haikuarabishwa? (2) Kwa nini waislamu kutoka Asia waliohamishiwa Afrika Kusini waliweza kuendelea na Uislamu wao kwa takribani karne 3 ilhali waislamu waliohamishwa kutoka Afrika kwenda Marekani walipoteza Uislamu wao?

Kuhusu yanayojiri Libya alioneshwa kusikitishwa sana na mapambano yaliyojikita katika ubaguzi wa rangi na kudai kuwa hali hiyo katikaa kiwango hicho haijawahi kutokea tangu wakati wa mapinduzi ya Zanzibar. Ilhali mapambano ya Zanzibar yalikuwa kati ya 'Waafrika Weusi' waliokuwa wamenyimwa fursa dhidi ya Waarabu, Profesa Mazrui alisisitiza, yale ya Libya ni ya Waarabu dhidi ya 'Waafrika Weusi' wasio na fursa. Aliongeza msisitizo kuwa kuna Walibya wengi sana ambao ni 'Waafrika Weusi'. Katika kusisitiza hilo alihoji mbona katika mapambano ambayo Wamarekani na Wayahudi wanahusika neno 'mamluki' halitumiki? Japokuwa hakumtetea Gaddafi alikiri kusikitishwa sana na kitendo cha kumuua kwa namna ile na kutoa mfano wa wauaji wa Kinazi wa Ujerumani ambao pamoja na mabaya yao yote walipewa fursa ya kuhukumiwa kule Nuremburg kama wanadamu wenye haki hiyo.

Kuhusu Jos na Boko Haram huko Nigeria alisikitishwa na hali hiyo. Japo alikiri kuwa pamoja na kuelimishwa katika elimu ya kimagharibi na yeye ni mpinzani wa masuala mbalimbali ya elimu hiyo ila hakubaliani na upinzani wa elimu unaondeshwa na kikundi hicho. Na kuhusu Somalia na Kenya alionesha wasiwasi mkubwa kuhusu Wasomali wa Kikenya wasiohusika kwa lolote na mashambulizi ya Al-Shabab kujikuta wanahukumiwa na jamii bila hatia yoyote.

Ombi lake kubwa ni kurejea kwa hali ya ubinadamu.

4 comments:

Chambi Chachage November 2, 2011 at 3:36 PM  

Maoni:

Kwanza nikushukuru Chambi kwa taarifa ya kina kuhusu huu mdahalo na Prof. Mazrui. Ila niseme kwamba sikubaliani na uchambuzi wake hapo juu, hasa premise yake kwamba kuna kitu kinaitwa "ustaarabu wa kiislamu" na kwamba wazungumzaji mbalimbali wa Kiswahili wamerithi ustaarabu wa Kiislamu. Nadhani mwanazuoni huyu anachanganya ustaarabu wa kiarabu na dini ya kiislamu.

Ukienda katika nchi za kiarabu ambako mi nimeishi kwa miaka 6 hivi, utagundua kwamba mambo mengi. Ila mawili ambayo yanahusiana na mjadala huu ni:-
1. Kuna tofauti ya dhahiri kati ya "Uarabu" na "Uislamu". Ingawa Uarabu umekuwa influenced sana na Uislamu, lakini Uarabu si Uislamu. Kwa hiyo mifano anayotumia ya lugha, hiyo ni ustaarabu wa Kiarabu na si wa Kiislamu. In fact ukiongea na wanazuoni wa kiislamu unagundua wao mara nyingine wanakuwa frustrated na huu mchanganyo maana kuna mambo mengi yanayodhaniwa kuwa ya Kiislamu ambayo wao wanasema ni ya Kiarabu na si Kiislamu.

2. Katika nchi za Kiarabu kuna waarabu wengi wasio waislamu lakini wanao-share sutaarabu wa Kiarabu bila kujali dini zao.

Kwa hiyo nadhani mwanazuoni Mazrui amechanganya madawa kwa kulinganisha Uarabu na Uislamu kwani hvyo ni vitu viwili tofauti. Na ingawa dini ya Kiislamu ime-influence sana Swahili Coast, lakini ni Ustaarabu na Lugha ya Kiarabu vilivyo-influence Kiswahili na kuletea urithi wa maneno kama aliyotolea mifano. Na kusema kwamba ustaarabu mzima wa Kiarabu ni Uislamu ni ku-ignore kundi kubwa la Waarabu wasio Waislamu wanaopatikana katika nchi za Kiarabu.

-----------------------

Ni kweli hata mimi alinitatiza kuhusu hilo na jana bado kidogo nihoji hiyo tofauti kati ya ustaarabu wa kiarabu na ustaarabu wa kiislamu wakati natoa huo muhtasari ila nikasema ngoja nitafakari zaidi; sasa nimeangalia nukuu hizi katika kitabu cha mpwa wake kinachomnukuu, naona hapo wametoa mifano ya maneno yaliyopo kwenye Quran kama 'malaika' na ambayo tunayatumia pia katika Kiswahili:

http://books.google.com/books?id=o063rsBCIvMC&pg=PA93&lpg=PA93&dq=islamic+civilization+mazrui&source=bl&ots=9EKm7914G3&sig=TsLuqk4Rr3Fp2lxXBAmj_AG7oeM&hl=en&ei=RSOxTsK9MuTY0QH-0rytAQ&sa=X&oi=book_result&ct=result&resnum=4&ved=0CDAQ6AEwAw#v=onepage&q=islamic%20civilization%20mazrui&f=false

Pia kuna hii pepa yake kuhusu Utandawazi wa Ustaarabu wa Kiislamu nadhani inatoa picha kuhusu nia yake: http://www.themodernreligion.com/world/mazrui.html

Chambi Chachage November 3, 2011 at 5:27 AM  

MAONI:

Inawezekana ni huu ufinyu wangu tu wa mawazo ila the book is more confusing and not enlightning.

In my opinion, just because neno limetumiwa katika Quran does not Islamize the word. It is a fact kwamba Quran ilitumia an existing language, Arabic, to convey the intended message, it did not bring a new language. Kwa hiyo kwa kutumia neno malaika, ilitumia neno already existing in the Arabic Language.

Sidebar to the Linguistics: I understand kwa nini mtu wa kawaida anaweza ku-assume kwamba matumizi katika Quran yanaweza ku-consitute lugha. Katika kusoma kwangu kuhusu Semitic Languages niligundua kwamba Arabic is the only surviving and widely used semitic language kwa sababu lugha iliyotumika katika Quran ni kiarabu na wenzetu waislamu hawakutaka itafsiriwe katika lugha zingine hivyo kuhifadhi uasili wake. Kwa hiyo ukiangalia mnyumbuliko wa lugha ya Kiarabu utagundua imegawanyika katika makundi matatu, kuna Classical Arabic which is commonly refered to as Quranic Arabic, then you have Modern Standard Arabic, Al Fus'ha, and the Colloquial Arabic which is the many national and regional varieties spoken daily on the streets, the slang if you wish.

So based on the corellation of the Classical Arabic being refered to as Quranic, mtu anaweza kusema maneno yaliyotumiwa kwenye Quran ni ya Kiislamu, lakini in real sense ni ya Kiarabu, including Malaika.

Sasa baadhi ya nukuu katika Swahili Beyond Boundaries sizikubali which undermines mamlaka ya kitabu chenyewe. Nitakupa mfano. Uk 3 anamnukuu Kiango na Sengo "Kwa hapa kwetu, Kiswahili ndiye mlezi, ametukuza tangu siku za ukoloni na kutuunga pamoja hadi kufika siku za uhuru wetu. Ni lugha inayoeleza utaratibu wetu wa maisha...Mswahili ni Mtanzania na hapana shaka lugha ya Kiswahili ni lugha ya Watanzania." Sasa mimi binafsi sikubaliani na hii statement. Nadhani waswahili are more than Watanzania na Kiswahili ni lugha ya watu wengi zaidi ya watanzania pekee.

In fact, hata tafsiri yake ya baadhi ya vitu kama "Uswahilini" on P.13 I feel is off-base. Uswahilini is not the "land of the Swahili-speaking people." Uswahilini ni mtaani.

Anyway, what do I know.
---------------------


Prof. Mazrui ni mwanazuoni hasa aliebobea. Anajua kuchanganua na kujibu maswali vizuri kwa mifano iliyo dhahiri. Sikubaliani na comparative analysis baina ya TZ na Ivory Coast kwa kuwa inakuwa kama vile unawaambia watu "wakistajaabu ya Musa watayaona ya Firauni" Au kwa maneno mengine wavumilie tofauti za kidini na athari zake zinazoibuka kwa kuwa si kubwa sana. Sidhani kama mtu hata kama ni mmoja atakubali kuvumilia eti kwa kuwa tatizo kwa ujumla wake si kubwa sana. Therefore, such a comparative analysis obscures the nuanced experience and issues emerging in Tanzania. Instead an isolated and absolute analysis of each case could yield valuable contributions to both the theory and practice of religious tolerance in each case.

Thanks you Chambi, you made a every good summary. You were indeed a good participant to that seminar.
--------------

Chambi Chachage November 3, 2011 at 5:27 AM  

Maoni:


ndio ,tanzania tuko pazuri kuhusu udini, tatizo ni wanasiasa uchwara wanaojaribu kuibua udini ili tulumbane wao watufisidi. linatendeka ili hata serikali haikemei! ila hata wafanye vp ni vigumu kuwa na machafuko halisi ya kidini. tumechanganyika na kukubaliana sana kwa kweli

Ombi lake kubwa ni kurejea kwa hali ya ubinadamu......... hapa ndo namimi nakubali kabisa. maana watu wenye nia chafu wanatumia dini, ukondoo wa wafuasi wao na uhaba wa kujitambua kutumia watu kupigana, kuchafuana nk. Mungu anageuka chanzo cha vurugu. unakta mtu eti anapigania dini, anampigania Mungu, wakati Mungu huyo ndo anawapa wate pumzi wanayoshea kuuana! dini au Mungu zunachepuka ubinadamu!!

anyway, hakuna aliyechagua dini wala kuzaliwa na dini! ni ajali ya kuzaliwa tu
-----------------------

Ni kweli, kwa hapa kwetu `crosscutting cleavages complicate religious mobilization at least for political gains. Lakini kuna hatari moja.Ugumu wa maisha na tofauti za kipato zinazokua kila siku zinapelekea kukata tamaa.Watu wenye mtazamo finyu wameshaanza kutafsiri tatizo hili katika mtizamo wa dini na upendeleo. Hili sio la kupuuza

Ni wazi kua kdri ubepari unavyozidi kukita mizizi, zile values zetu za undugu na kubebana(extended family) zinakosa nguvu. Kama hatutafanya jambo,hata sisi itafikia hatua uvumilivu utatoweka.

Nilikua kijijini july iliyopita,kanisa likatuma ujumbe kutoka makao makuu kua `kuna vita inatangazwa na tuwe tayari`.` Tuombe ipite mbali ila tusifumbe macho kana kwamba haipo`--Wanavijiji walikusanyika kwa makundi na kujadili jambo hili.Kila mmoja akaingiwa na hofuu kuu.Hawakua wanajua kama kuna `vita`.Sasa wanafahamu.

Kwa ujumbe huo,tayari hofu ya udini imepenya mpaka vijijini.Sina hakika kwa siku za usoni zitatumwa jumbe ngapi kwa wanavijiji.Ninachojua ni kua baada ya muda watazoea jumbe hizi na chuki itajijenga taratibu.
-----------------
kanisa kutoa vitisho kama hivyo visikutishe sana kwani mtaji wa dini zote ni vitisho juu ya maisha yajayo hapa duniani na baada yake. bila vitisho hivyo, hamna msingi wa kanisa na linaweza kosa waumini

Unknown December 8, 2011 at 7:13 PM  

Asante kwa mazungumzo mazuri. Ni kweli kwamba kuna utata kuhusu kutofautisha tamaduni za kiislamu na utamaduni/ama ustaarabu wa kiarabu. Nafikiri kujaribu kutofautisha sana litakuwa ni zoezi la bure. Na fikiri mfano mzuri ni kama bongo flava ambayo ina mizizi ya ushairi wa Kiswahili. Hakuna mtu anaita bongoflava ustaarabu wa kiislamu kwa sababu ingawa athari zake kama vile vina na mizani inatokana na ushairi wa Kiswahili na kabla zake tenzi za kumsifu mtume, Bongo flava kwa ufinyu wa maneno umekwenda mbali sana na tenzi za kidini. Imechukua athari mbali mbali na kuwa kitu tofauti sana. Suala la kutofautisha tulichukulia kama aina fulani ya kujenga hoja maana kila kitu kina complications. Asante sana. Mohamed Yunus

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP