Loading...

Tuesday, November 29, 2011

HAYA MATUNDA YA KULE KWETU KUMBE NI DAWA!

Nchini Uturuki nilikuta kila asubuhi katika hoteli fulani wakati wa kifungua kinywa kunakuwa na matunda ambayo kule kwetu milimani tunayaita thambia/sambia. Bahati mbaya sikuuliza yanaitwaje kwa Kiingereza. Ila niliyapiga picha na kuwaonyesha wanafesibuku kutoka huko kwetu na wakathibitisha kuwa kweli ni hayo matunda. Jana bahati nzuri nilimuuliza dada wa Kituruki hapa nilipo haya matunda wanayaitaje. Akasema wanayaita malta eriği (maltese plum) au muşmula, pia akasema wengine wanasema ni matunda kutoka 'dunia mpya' ('new world'). Ila akanipa linki hii hapa chini inayoonesha kuwa jina lake lingine ni Loquat na ni dawa. Sijui watu wa kule kwetu wanalitambua hilo au wanayala tu kama matunda pori mengine. Nitakapomtembelea Bibi yangu hivi karibuni nitamuuliza.


0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP