Loading...

Monday, November 21, 2011

KONGAMANO KUHUSU HALI YA ELIMU NCHINI


Salaam kutoka HakiElimu!

Yah: Mwaliko wa Kuhudhuria Kongamano kuhusu hali ya Elimu nchini; Tarehe 26 November 2011,Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Katika kuadhimisha miaka hamsini (50) ya Uhuru wa Tanzania Bara, Umoja wa Wanafunzi Walimu (UDSTA) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Shirika la HakiElimu wameandaa kongamano kuhusu hali ya elimu nchini. Kongamano hili litajadili maendeleo na changamoto katika Sekta ya Elimu tangu nchi yetu ilipopata uhuru. Kongamano hili litafanyika siku ya Jumamosi, tarehe 26 Novemba 2011 kuanzia saa 4.00 asubuhi katika Ukumbi wa Yombo 4, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wazungumzaji wakuu katika Kongamano hili watakuwa Ndugu Jackson Makweta, Waziri wa zamani wa Elimu, na Profesa Justinian Galabawa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Ukiwa mdau muhimu wa maendeleo ya elimu na ya kijamii hapa nchini, unaombwa kuhudhuria kongamano hili wewe mwenyewe pamoja na viongozi wenzako. Aidha, unaombwa kwa nafasi yako uhamasishe wadau wengine katika taasisi yako, taasisi zingine, pamoja na wananchi kwa ujumla kuhudhuria kongamano hili muhimu.

Tafadhali wasiliana nasi kwa ufafanuzi zaidi.

Simu ya mezani; 255 22 2151892/3, simu za mkononi: +255 655/784 283 163

Barua pepe: media@hakielimu.org

Tunatanguliza shukrani zetu kwa kukubali mwaliko huu.

Wasalaam,

Annastazia Rugaba

Idara ya Habari- HakiElimu

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP