Loading...

Monday, November 21, 2011

MAJADILIANO YA WAZI/OPEN FORUM 28-30/11/2011

TAARIFA KWA UMMAMAJADILIANO YA WAZI JUU YA ELIMU NA KUFUTA UJINGAMazungumzo ya kisera miaka 50 ya Uhuru: Hatua na mstakabali wa elimu na kufuta ujinga nchini Tanzania.Taasisi ya Usomaji na Maendeleo ya E&D —Soma na Chama cha Wauza Vitabu wa Tanzania (BSAT) zinajihusisha na harakati za kufuta ujinga kwa njia ya kuhimiza usomaji na maendeleo ya vitabu. Dira ikiwa ni kuiona Tanzania ikitimiza malengo yake ya maendeleo kama ilivyojiwekea katika malengo ya milenia na MKUKUTA. Tunaamini jambo hili linaweza kufanikiwa kama tutatafakari kwa umakini mstakabali wa elimu yetu: falsafa, ruwaza, na utendaji kwa kuzingatia ubora, ushiriki, rasilimali, uendeshaji na vipaumbele inavyowekewa.Katika kutimiza hilo, taasisi hizi zimeandaa, kama muendelezo wa Tamasha la VIitabu, mjadala wa wazi utakaofunguliwa jumatatu ya tarehe 28 Novemba 2011 na kufungwa jumatano tarehe 30 Novemba 2011 muda ukiwa ni saa 11:00 jioni hadi saa 4:00 usiku kwa siku zote ili kutafakari hatua zilizopigwa na wadau mbalimbali katika elimu na kufuta ujinga ndani ya miaka hamsini baada ya uhuru wa Tanganyika. Majadiliano haya yatafanyika katika viunga vya Mkahawa wa Vitabu Soma (Mtaa wa Regent Estate, Kitalu Na. 53, Mlingotini Close) kama sehemu ya Tamasha la Vitabu. Madhumuni ya majadiliano haya ni kutoa fursa kwa wadau mbalimbali wa elimu: wanajamii, waelimishaji, watekelezaji na watunga sera, wanataaluma, wanazuoni, pamoja na wanafunzi, kutafakari kwa kina kuhusu juhudi za wananchi na Serikali tangu enzi za Mwalimu Nyerere katika kufuta ujinga kama mojawapo ya maadui watatu wa maendeleo yetu.Mdahalo utafanyika jumanne tarehe 29 Novemba 2011 huku ukihusisha tafakuri ya kina itakayofungamana na vionjo vya kisanaa, ukiwaleta pamoja wadau wenye stadi, mitazamo, na uzoefu mbalimbali katika elimu kuzungumzia hatua tuliyopiga katika maendeleo ya elimu na juhudi za kufuta ujinga. Maswali makuu yatakuwa: “kipi tumefanya vyema?”, “kipi tungeweza kufanya vyema zaidi?” na “nini tunahitaji kufanya?” ili ndani ya muongo mmoja tuweze kuwa mfano bora wa jamii inayojua kujifunza.Mbali na hivyo, kuanzia jumatatu yatakuwa yakifanyika matukio kwa ajili ya jamii nzima kama vile maonesho ya vitabu na huduma za kielimu, vionjo vya kifasihi kama vile mashairi, ngonjera, ngano; shughuli za kuchangisha fedha kwa ajili ya huduma za kielimu ikiwemo ujenzi wa maktaba za jamii na mashindano ya fasihi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari, mnada wa vitabu vilivyotumika, maonesho ya muziki, dansi, nyama choma, na vinywaji.Hivyo basi, tunatoa rai kwa jamii nzima na watu wote wahudhurie kwa wingi bila kukosa kwa siku zote tatu ili kuja kubadilishana mawazo na watu wengine wenye maono na mitazamo tofauti kuelekea kuboresha hali ya elimu nchini. Hapatakuwa na kiingilio chochote kwa siku zote tatu.Demere Kitunga-(SOMA) Hobokela Magale-(BSAT)

PRESS RELEASEOPEN FORUM ON EDUCATION AND LITERACY21 NOVEMBER 2011A policy dialogue on 50 years of Independence: reflecting on the state of education and literacy in Tanzania, now and beyond.E&D Readership and Development Agency--Soma and Booksellers Association of Tanzania (BSAT) are practitioners in literacy through readership and book development; with an aspiration to see Tanzania meeting its development targets as spelled out in the Millennium Development Goals (MDGs) and MKUKUTA. We believe this can happen if we rethink about our education: philosophy, approach and practice including quality, how inclusive, how it is resourced, managed and what gets prioritized.These two institutions are jointly organizing a public event, that will take place at Soma Book Café (Regent Estate, 53 Mlingotini Close) from Monday 28th to Wednesday 30th November 2011 from 5pm to 10pm, for education stakeholders to reflect on the state of education and literacy 50 years of Uhuru. The event is a sequel to the National Book Week and is meant to provide space for private citizens, educators, education planners and policy makers, intellectuals and learners to reflect on efforts made by the people and their Government since Mwalimu Nyerere’s era in the fight against illiteracy as one of the three tier enemies of development.The event seeks to bring a balance between dialogue, serious reflection and creative expression, on Tuesday 29th of November 2011 the main activity will be a Policy dialogue bringing together a wide range of stakeholders with diverse skills, perspectives, and experiences on education, literacy and development to engage in a conversation on the state of education and literacy in Tanzania: “what grounds we have covered?”, “what we could have done better?”, and “what we need to do to become?” within the coming decade, a good example of a learning society. This will feature a panel, plenary, poetry, storytelling and other forms of literary expression.Apart from that, there will be other sub-activities daily from 28th through to the 30th November 2011 ranging from exhibition of books and other education related inputs, literary expression, and fundraising for a social cause by auctioning second-hand books, spontaneous talent shows, music, dance, barbeque and bar tenders in action.We hereby, urge all society members to come and participate in airing out their views on how we can improve our education for the betterment of the nation. No entrance fee! You are all welcome.Demere Kitunga-(SOMA) Hobokela Magale (BSAT)

1 comments:

Anonymous November 29, 2011 at 10:02 AM  

Hallo Chambi,
Nimevutiwa sana na hii event. Leo jioni nitahudhuria event hii.

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP