Loading...

Thursday, November 10, 2011

UZINDUZI WA VITABU VIPYA VYA NYERERE NA MJADALA

Ndugu zangu salaam,


Kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru hapo Disemba 9, 2011; Tarehe 17 na 18 Novemba, 2011 Taasisi ya Mwalimu Nyerere imeandaa tafakuri ya pamoja juu ya Katiba na Maadili kwa mustakabali wa Taifa. Tafakuri kuu ya siku hizo ni “Historia ya Katiba: Tulikotoka, tulipo na tunakotaka kwenda kama taifa katika muktadha wa mjadala wa Katiba mpya.”


Sambamba na mjadala huo, kuanzia tarehe 16 mpaka 18 Novemba, 2011 kutakuwa na maonesho ya wazi ya harakati na shughuli mbalimbali alizoshiriki Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius K. Nyerere. Pia tarehe 16 Novemba, 2011 kuanzia saa 05:00 asubuhi katika ukumbi wa maonesho kutafanyika uzinduzi wa vitabu vitatu vya Mwalimu Nyerere 1. Freedom and Liberation; 2. Freedom and A New World Economic Order na 3. Freedom, Non-Alignment and South-South Cooperation”Mapitio ya Vitabu hivyo yatafanywa na


Prof. Issa G. Shivji na

Dr. Ng’wanza Kamata.


2. Mjadala juu ya Katiba na Maadili; na maonesho hayo vitafanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa mtaa wa Sokoine Drive (jirani kabisa na Chuo cha IFM). kuanzia saa 3:30 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kila siku.


Watoa mada wakuu katika mjadala huo wanatarajiwa kuwa ni pamoja na

1. Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta,

2. Prof. Palamagamba Kabudi, Mkuu wa shule ya sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

3. Jaji Mstaafu Damian Lubuva, Mwenyekiti wa Secretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma

4. Jaji mstaafu Amir R. Manento, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu

5. Mzee Ibrahim Kaduma,

6. Prof. Gammaliel Fimbo;

7. Mzee Ibrahim Kaduma, na

8. Ndugu Francis Stolla, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika; na wengine wengi.


Mawasiliano kwa taarifa zaidi:

1. Miraji Magai; 0719 946 371 (mairamjr@hotmail.com )

2 Edgar Atubonekisye; 0713 199 858 (mwandemanieddie@yahoo.com)


Hii si tafakuri ya kukosa! Nyote mnakaribishwa.


Edgar Atubonekisye

Assistant Programme Officer;

The Mwalimu Nyerere Foundation

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP