Loading...

Thursday, January 19, 2012

'ULIZA TU' - NA EVARISTO HAULLE


Enyi wanazuoni weledi,

Amani iwe nanyi!

Napenda kumpongeza jukwaani mwanazuoni Evaristo Haulle kwa 'kukataa kufa'. Amekataa kufa kwa kutoenda kuuza mchicha ama kuanzisha dirisha la kuuza sabuni pale nyumbani kwake, aitwe mjasiriamali. Amekataa kufa kwa kugomea kunyamaa afe kibudu; Amekataa kufa kwa kukionea haya Kiswahili lugha adhimu ya Taifa;

Mwenzetu kakataa kufa, amechapisha Diwani yake ya kwanza; ULIZA TU (kitabu cha mashairi), amekataa kufa, amekibinua kiulizo!

Onja Ladha ya yaliyomo:

MAHABA:
Mahaba ni kama moto, joto utafurahia
Mahaba ni kama moto, chakula utapikia
Mahaba ni kama moto, mwanga tajipatia
Mahaba ni kama moto pia unaangamiza,
Mahaba ni kama maji, mwilio wahitajia
Mahaba ni kama maji, kiu yatakukatia
Mahaba ni kama majiukikosa wajutia
Mahaba ni kama maji, yazoa yaangamiza


KAMA KWELI WAFAA:
Kama kweli unafaa, khanga vitenge vya nini?
Kama kweli unafaa,huhitaji bilioniKama kweli unafaa, huna haja kurubuni
Kama kweli unafaa, waonekana machoni....

Na

WAFALME MWITUNI:
Tembo na miguvu yako, ni vipi unatishika
Ndani ya himaya yako, kichwani unajishika
Tazama unyayo wako, sisimizi watishika
Ni nini uoga wako, waache waandamane.

Langu ni neno la pongezi kwako mwanazuoni Evaristo, changamoto umenipa. Ninazo nakala chache kwa walioko Dar waweza kujipatia.

Adam Lingson

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP