Wednesday, February 29, 2012

malumbano ya hoja 3 machi 2012

RATIBA:

Saturday, February 25, 2012

KISWACENTRIC: ENGAGING THE POLITICS OF LANGUAGE

KISWA-CENTRIC: The politics of language in East African culture, art, and media


Yale University


Linsly-Chittenden Hall Room 211


63 High Street, New Haven


Friday, March 2, 2012


10am-5:30pm


This one-day symposium will explore the politics of language and representation in East African culture, art, and media, reflecting on the tension between artistic choices and conventions, on the one hand, and colonial and post-colonial legacies of "foreign" and indigenous languages, on the other.


SPEAKERS:


Omari Kaseko, Filmmaker


Zavara Mponjika, Hip Hop Artist, Emcee


Catheryn Massamu, Presenter, East African Television


Mukoma wa Ngugi, Author, Nairobi Heat


Mohamed Yunus Rafiz, PhD Student and Filmmaker


For more information and to RSVP, visit https://docs.google.com/spreadsheet/viewform?formkey=dEk4Q0NONUFJM3o0cmVWUmVjbmtDUlE6MQm


If you have other questions, contact zachary.enumah@yale.edu

Thursday, February 23, 2012

UHARIBIFU WA KISWAHILI MITANDAONI

UHARIBIFU WA KISWAHILI MITANDAONIZAVARA MPONJIKANimefurahishwa sana na waraka wa "Watanzania Tunavyokiharibu Kiswahili Twitter"na namna mwandishi anavyokabiliana na hili tatizo. Nimefurahi kuona kuna watu wengi wanaguswa na tatizo hili linaloanza kupevuka. Watu wengi wanaoingia humu kwenye hizi baraza za kijamii(Facebook, Twita) kiukweli wana zile athari za ulimbukeni.Ugonjwa wa ULIMBUKENI ni mbaya yaweza kuwa pengine kuliko UKIMWI na SARATANI, ila unaweza kupona. Inasikitisha kuona hadi leo watu wanadhani eti kuongea kikoloni ndo' ujanja. Bahati mbaya pamoja na kulundikana kwa mashule yanayoitwa English Medium hicho kikoloni bado hakina nguvu. Nimeshakaa na wanafunzi kibao wa vyuo vikuu ambao hawawezi kuongea lugha hii wanayoinyenyekea. Ni aibu kweli wanachokinyenyekea hawakiwezi na cha kwao kinaanza kuwaponyoka.Nilitarajia kwenye makala yako ungegusia kuhusu huu mtindo wa kuingiza herufi C (inatamkwa CHE kwa kiswahili) na kuingiza namba 2 na 4 kwa kujifanya kama mtu anaandika kikoloni, mtindo ulioanzia kwenye kuandika ujumbe wa maandishi kwenye simu. Kuna wanaohadaika kudhani eti ni ubunifu kuandika vile, wakati ukweli ni kwamba ni UJINGA wa hali ya juu. Maandishi na herufi hizo haziendani na lugha ya kiswahili hata kidogo. Ukiandika "m2" kwa kiswahili inasomeka "mmbili" - kitu ambacho unakuwa umeondoka kabisa kwenye mantiki. Kwanza hairahisishi lolote kwa vile inabidi utafsiri mara tatu ili kupata maana. Kwa hiyo kusudio la msingi linapoteza maana yake. Hii inadhihirisha watu hawajui kusoma na wana utata kwenye kuandika. Hili jambo limeanza kukomaa sana. utaona mtu anaandika "cina" akimaanisha sina ambapo kwa Kiswahili inasomeka C"chena". Je, hapo unawasilisha nini na kupunguza herufi gani? Kwa huo uandikaji ulikusudiwa na lugha ile kupunguza urefu wa maneno. Hapo ule ujinga niliousema unajidhihirisha.Sasa ina maana gani kwa neno kama hilo hapo juu iwapo idadi ya herufi inakuwa ileile?Inafaa tufanye juhudi za dhati wadau wa kiswahili hasa wa kizazi hiki kukemea na kufanya mambo mbali mbali kuonyesha madhara ya kudharau lugha na tamaduni zetu na kuendekeza vya wengine. Nimewahi kuwa na mijadala na watu wengi kuhusiana na suala hili, kuna wanaojitetea eti ndio usasa. Nilicheka sana na kuwaambia sio usasa bali ni ULIMBUKENI na kama hao wanaojaribu kuwanakili mbona hawachanganyi Kiswahili? Usasa iweje uwe unaathiri upande wetu tu?Hongera sana kwa kukemea hili, kwa wote wanaokemea tuko pamoja kwenye mapambano haya. Nahitilafiana tu kidogo na mwandishi wa makala kule Tanganyikan pale usemapo Kenya Kiingereza ndio lugha yao ya kwanza, hilo sio sahihi lugha ya kwanza haimaanishi lugha unayokutana nayo shule. Wapo watu wengine pia wanosema na kudhania kuwa Kiingereza ndio lugha ya kwanza. Nigeria hilo pia sio sahihi. Lugha ya kwanza ni ile unayoongea ukizaliwa, unayokuta mama akiongea nawe. Kule Kenya lugha za kwanza mara nyingi ni zile asilia na Kiswahili ni ya pili kwa mantiki hiyo, ila kiswahili ni lugha ya taifa ya Kenya pia kama ambavyo ni ya taifa hapa Tanzania. Huu mjadala ni mrefu tuendelee kujenga ili tunusuru taifa letu kuangamia kwenye dimbwi la maangamizi. Upendo na amani.Twitter: @Rhymson


Facebook: Zavara Mponjika

Wednesday, February 22, 2012

chakula

Chakula(Dedicated to those who can read the signs of times)Want for chakula and more want …Hunger pangs without being hungryGreed!Thirsting for more food, drink and pleasureCraving!For food, drink and pleasureSometime, just the notion of itCraving for power!To make all humanity bow at the snap of your fingersSuch a craving!For means to sustain that POWERHunger pangs leading to grab, grab, and more grab!Money grab, sex grab, land grab and more grab!A drunken feeling of emptinessVoid!In spirit, deeds, relations and all life’s endeavorsAn empty feeling of want and more want…Selfish pursuit for more pleasure, power and ACCUMULATIONOpulence!Cry my beloved countryFor birthing this monstrous pursuit for chakula among the least hungryA land of abundance that feeds not its hungry bodies and minds!©Demere Kitunga, February, 2012

Sunday, February 19, 2012

MGENI KWETU NYUMBANI

Shikamoo

Unashangaa nini?


Msiba kwetu nyumbani


Kisiwani mwa amani


Kizazi hadi kizaziSisi tumeuzoea…Mgeni kwetu nyumbani


Kamwe si hayawani


Twamthamini mgeni


Kuliko hata mwenyejiSisi tunampokea…Biashara kwetu ndani


Haikosi mshitiri


Bara hata visiwani


Nyanda juu hadi pwaniSisi tunaiwezesha…Walokuja kwa jahazi


Wakisukumwa na kusi


Wa merikebu za mbali


Mizinga zikisheheniSisi tuliwaitika…Wengine wakichuuza


Na baadhi kulowea


Bara wakitangatanga


Kuzitafuta ngawiraSisi tuliwaonyesha…Nasi hatukukaidi


Kuwapokea kwa jadi


Walipoibisha hodi


Na misafara kuhodhiSisi tuliwapenyeza…Hatukuuanza leo


Ukuwadi tufanyao


Tulianzia na hongo


Kwa kila jino la temboSisi tulijitwalia…Mambo yalipogeuka


Tukageuzwa ngawira


Ndiposa wenye dhamana


Bei walipotupigaSisi tuliwahofia…Ni hawa hawa wakuu


Wa jana na leo yetu


Wanaofanya mizungu


Kutugeuza vizuuSisi tunawatazama…Wametuweka jamvini


Kututia msibani


Tulie kwa ufakiri


Na mali zetu lukukiSisi tumehamanika…Leo ushangae nini


Kwani ulikuwa wapi


Nyuki wakipigwa moshi


Na kulala usingiziSisi tukisuasua…Masega yalipovunjwa


Na asali ikarinwa


Na wanapozindukana


Nta wakasake tenaSisi tulinung’unika…Lini tutakuwa mbogo


Tuyakatae makombo


Tukashikane mikono


Tusitoe shikamoo?Sisi tunajiuliza!©demere kitunga, 2012

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP