Loading...

Monday, February 6, 2012

ARDHI YETU

UWEKEZAJI KATIKA ARDHI

Rasilimaili zetu watanzania,


Mola ametupatia kwa uwingi,


Hifadhi za misitu na za wanyama,


Ardhi yenye rutuba na madini,


Kwa wingi tumekirimiwa na Mungu.Sheria na sera tukazitunga,


Ili kulinda rasilimali zetu,


Mfumo wa usimamizi kuweka,


Kurahisisha kazi za kuratibu,


Na usimamizi wa ardhi yetu.Sheria na sera zetu zimepwaya,


Zimerithi mfumo wa kikoloni,


Rais ana milki ya hatma,


Wananchi wana hadhi ya upangaji,


Katika ardhi alowapa mola.Vyombo vya usimamizi legelege,


Watendaji wamekosa maadili,


Rushwa imekuwa kipaumbele,


Maskini hawezi kupata haki,


Kama mfumo hautabadilika.Uwekezaji sasa ni uporaji,


Ardhi za vijiji zinawaniwa,


Sheria za ardhi hazifuatwi,


Watendaji wastahili lawama,


Kwa kuwa wasaliti wa wananchi.Haki za ardhi tuzifahamuni,


Sheria, taratibu kuzijifunza,


Kamwe tusikubali unyanyasaji,


Wanyonge tusiache kuwatetea,


Ardhi ni rasilimali! Itunze.Ardhi ni rasilimali ilindwe,


Haki na mfumo wa usimamizi,


Uwekwe na Katiba izitambue,


Milki ya hatma iwe kwa wananchi,


Ili wawe na maamuzi ya mwisho.© Godfrey Eliseus Massay 10/11/2011

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP