Loading...

Friday, March 23, 2012

Ujana, Uzee na Urais

Zifuatazo ni dondoo zitokanazo na mjadala wa Wanazuoni: Tanzania's Intellectuals ulioibuliwa na makala hii Ayub Rioba ' Zitto, Januari na umri wa rais: Mjadala uliopotea njia'.

"Hii hoja sio ya kuitazama kijuu juu, kuna masuala mengi ya kujadili na kuyatafakari hasa linapokuja suala la wakati na mazingira. Kwa nchi za Afrika ambapo suala la uroho wa madaraka ni sawa na urithi wa shamba kutoka kwa baba kwenda kwa mwana, tunapozungumzia suala la umri ni lazima kuwa makini. Mimi nadhani tunapojadili hoja hii tusiwatazame January na Makamba pekee, tutazame vijana wengine wengi ambao watakuja kuitumia fursa hiyo. Angalizo tunapojadili hili tuanze na kujadili suala la kuongeza muda wa kukaa madarakani muda mrefu zaidi wa miaka kumi(10) ya sasa. Mnaelewa ninapozungumzia kuongeza ukomo wa kukaa madarakani zaidi ya miaka kumi kama hamuelewi tazameni jirani zetu toka miaka ya 1980s mpaka leo, kisa waliingia wakiwa vijana. Mimi pamoja na ujana wangu bado naunga mkono utaratibu uliopo wa kuwania urais kuanzia umri wa miaka 40 na kuendelea" - Cathbert

"Umejitahidi sana kuchambua hoja kwa kutumia mbinu ya kulinganisha hoja zako. Ila jambo moja la msingi ambalo ama umelisahau au hukuliona ni kua Zitto na January wanawakilisha kundi gani la vijana? Je hawa vijana wawili wanaelewa na kuhisi kwa dhati machungu ya vijana ambao hawana ajira au wanafanya kazi za chini ya kiwango mbali na kua na digrii zao? Vijana dhana pana,inayohitaji ufafanuzi. Hili sio kundi linalofanana. Je zitto na January ambao wanapiga vita rushwa huku wakiukumbatia ubepari mbali na kujua fika kua ubepari na rushwa ni mapacha watatufikisha wapi?" - Dan

"Old age is not synonymous with failure in leadership. Churchill, Xiaoping, Mandela, etc, were not young men when they rose to power. On the other side, Alexander the Great was not old either- but I doubt if his style of leadership would have made him that popular in this post-WW2 world. (Museveni and Kagame can choose to object though...) Maturity is the key. Young men can be capable but naive. The risk to the nation for putting an immature leader at the top can be significant. A President needs to understand the dynamics of politics, economics, security, social psychology, international relations, policy, and a hundred other things. The President also needs to be proven in many areas. Instead of electing novices who will try to be Presidents in the offices, I wish they learn to be one before they become one. After all, anybody who thinks that it will be late for him/her to become president at 40 should probably not be elected to the office. You don't want impatient people at the helm of power...If there is a discussion which has lost its way, then it is the fact that we are discussing reducing the lower age limit instead of setting the upper age limit for people to be elected into power. Biology has a lot to say about the upper age limit. Think Mugabe. You have got to feel for Zimbabweans!" - Charles

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP