Loading...

Thursday, March 29, 2012

Zitto: Tanesco, Mgawo na Stahili ya Jenereta

Ndugu Wanamabadiliko,

Nimeona ni vema nitoe ufafanuzi kuhusu suala la Kamati yangu kuiagiza bodi ya TANESCO kuondoa stahili ya 'standby generator' kwenye mkataba wake wa kazi.

Rationale

Shirika la Ugavi wa Umeme nchini lina jukumu la kuhakikisha kuwa nishati ya umeme inapatikana kwa wananchi wote. Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO ndiye Mtanzania aliyepewa jukumu hilo na Taifa. Iwapo mkurugenzi mkuu wa TANESCO anawekewa stahili katika mkataba wake kwamba 'atapewa standby generator itakayolipiwa na Shirika' maana yake ni kwamba mgawo au kukatikakatika kwa umeme ni jambo litakalokuwepo tu. Kwamba Shirika linalopasa kuhakikisha kwamba Umeme unapatikana muda wote, Bosi wake anapewa stahili ya 'Generator' umeme ukikatika. Bosi huyu atajuaje machungu ya kutokuwepo Umeme? Morally this is wrong. Fundamentally this is a contradiction to CEO's mandate.

Jambo hili ni dogo sana lakini lina maana kubwa sana. Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO haikupaswa kuweka stahili hii.

Kuhusu wengine, kamati ya POAC haina mamlaka ya watu wengine. Mawaziri wapo kwenye kamati ya Makamba, kwenye POAC wanaohusika ni Bodi na CEO basi. Wanaonitaka kuagiza kwingine wananipa jukumu lisilo langu.

Hata hivyo kimsingi, Waziri wa Nishati hapaswi kuwa na Jenereta nyumbani kwake, iwe ya kulipiwa na Serikali au ya kujilipia mwenyewe. This is politics at higher level - Next level kabisa. Tukubali kubadilika ndugu zangu. Haya ni mambo madogo yenye maana kubwa sana.

Kuhusiana na Tanesco kutopewa fedha. Kamati imekuwa kali sana kwa serikali. Kamati ilimwita Katibu Mkuu kuhusu suala hilo. Kamati imeagiza kwamba suala hilo limalizwe haraka iwezekanavyo.

Kamati ya POAC inajitahidi sana kuhakikisha Mashirika ya Umma yanatimiza wajibu. Tunaomba mtuunge mkono na pale ambapo mnaona tumekosea, msitubeze bali mtueleze tujirekebishe. Kejeli, kurushiana maneno na kujadili mambo juu hakutasaidia Taifa letu. Tushirikiane, tusaidiane, tukosoane ili tusonge mbele kujenga Taifa letu zuri sana.

Zitto

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP