Thursday, April 26, 2012

Kufundishia Kiingereza Kunatudumaza Kielimu?

Kufundishia Kiingereza Nchini: Ni Kasumba Tu Inayodumaza Elimu!

Angalia Saa yako, unahesabu Saa kwa Kiswahili, lakini  lazima
utakuwa umeirekebisha isomeke kwa Kiingereza!


Na Saidi Nguba

Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini huru, Nelson R. Mandela, aliwahi
kusema katika nukuu zake nyingi za busara, kwa Kiingereza:“If you talk
to a man in a language he understands, that goes to his head. If you
talk to him in his language, that goes to his heart.” Kwa tafsiri
yangu, ya Kiswahili: “Ukizungumza na mtu neno katika lugha
anayoielewa, linamuingia kichwani. Lakini ukizungumza naye katika
lugha yake, linamuingia moyoni mwake”.

Mbunge, Profesa Kulikoyela Kanalwanda Kahigi, ambaye ni mtaalamu wa
lugha, akizungumza katika mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na  Michezo, bungeni  mjini Dodoma Agosti
mwaka 2011 alisema: “Lugha ni nguzo ya msingi ya kujenga uzalendo.
Vinginevyo utajengaje uzalendo kwa kutumia lugha ya kukopa ya
kigeni?”.

Profesa Kahigi aliongeza: “Tunawafundishia vijana wetu kwa Kiingereza.
Je, tunawapa maarifa vijana wetu au tunawafurahisha mabwana zetu?”.
Hii ndiyo hali ilivyo nchini Tanzania, tuna kasumba ya Kiingereza,
lugha ya kigeni na lugha ya kikoloni.  Mpaka sasa, miaka 50 ya Uhuru
wa Tanzania Bara, uamuzi haujafanywa wa kuitumia Lugha hii adhimu ya
Kiswahili kufundishia nchini katika ngazi zote, pamoja na kuwa lugha
hiyo ina vigezo vyote vya kukidhi kazi hiyo. Hii haina maana kukipuuza
Kiingereza, ambacho watu wengine hapa nchini wanakiita kuwa ni
“Kiswahili cha Dunia”. Ni vizuri  Kiswahili kifundishwe vizuri,
kitumike kufundishia na Kiingereza pia kifundishwe vizuri kama lugha
na liwe ni somo la  lazima kwa kila mwanafunzi kuanzia darasa la
kwanza, hadi Sekondari, ili wanafunzi wote, wakifika kidato cha nne,
kwa mfano, wazungumze na kuandika lugha hiyo kwa ufasaha mkubwa.
Kasumba imefikia kuona jambo hili kuwa ni kitu cha kawaida. Kwa mfano,
ukimuuliza mtumiaji wa Kiswahili, je, sasa saa ngapi? Atakujibu, sasa
ni saa 6. Lakini mwambie aangalie alivyorekebisha saa yake. Utaona
mshale, badala ya kuwa katika sita,  uko kwenye namba 12, kama vile
walivyozoea Waingereza, kwa mfumo wao  wa kujua wakati.  Saa 6 ya
mchana, kwa Kiswahili, Kiingereza  siyo “Six o’clock” ni “Twelve
o’clock”!

Kiingereza ni Lugha siyo Elimu

Swali la kujiuliza: Je ni kwa nini basi tunaendelea na kasumba hii ya
kukipa kipaumbele Kiingereza na kupata kigugumizi cha kukitumia
Kiswahili kufundishia katika ngazi zote?
Ubishi unaoenea kwa kasi ni kuwa Kiingereza ni “Lugha ya Kimataifa” na
kwamba kwa kufundishia, vijana wetu watakuwa na elimu inayolingana
kimataifa. Pili, kwa vile hakuna vitabu vya kutosha vya Kiswahili,
ukilinganisha na vya Kiingereza, kufundishia  Kiswahili, ni tatizo.
Sababu zote hizi zinamfurahisha zaidi Mwingereza tu.

Ukweli  ni kwamba Kiingereza ni lugha tu na mtu anaweza akajifunza, na
kwa utaalamu wa kisasa wa kufundisha lugha na nyenzo zilizopo, hata
kwa miezi mitatu mtu anaweza akakielewa na kuzungumza. Lugha siyo
elimu, isipokuwa ni chombo cha kusaidia kutolea elimu. Elimu ni uwezo
mkubwa wa kuelewa na kugundua mambo, ili hayo unayoyaelewa na
kuyagundua yatakusaidia kuleta mageuzi katika maisha yako na ya
binadamu wengine, kutoka kiwango fulani na kwenda kiwango cha juu
zaidi chenye kuleta manufaa na tija. Ili elimu nayo itolewe kwa vizuri
zaidi ni lazima lugha ya kufundishia iwe ile ambayo anayefundisha na
anayefundishwa wote wanaifahamu vizuri. Pili, hakuna vitabu vya
Kiswahili nchini kwa sababu havina soko. Mara uamuzi wa kufundishia
Kiswahili utakapochukuliwa, basi vitabu vya Kiswahili vitakuwa
biashara kubwa na vitaanzishwa hata “viwanda” vya kufyatua vitabu vya
elimu mbalimbali kutoka lugha za kigeni na kuwa vya Kiswahili.

Wataalamu wamekwishathibitisha

Uwezo wa Kiswahili kufundishia ili hatimaye elimu ikue kwa kiwango
kikubwa nchini na kujenga taifa la kujitegemea badala ya kuendelea
kuwategemea wengine kwa kila kitu, siyo mahitaji ya kisiasa, bali ni
jambo linalowezekana na lililothibitishwa na wanataaluma wa elimu na
wa lugha pia.

    Profesa John Kiango, Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakati anamkaribisha Waziri Mkuu Mizengo
Pinda kuzindua Taasisi mpya ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Julai 26, 2009, alisema: “Nikiwa mtaalamu wa lugha, napenda
nichukue nafasi hii, kukuhakikishia kuwa Kiswahili kinaweza, na
kikipewa nafasi kitaleta mageuzi ya kitaalamu na kiugunduzi nchini.”
    Anaongeza:“Tafiti zimebaini kuwa nchi zote zilizo na ugunduzi asilia
ambao siyo ule wa kuiga ni zile zinazotumia lugha  zao. Nchi
zinazotumia lugha za kigeni katika kutolea elimu zimebaki kuwa
watumiaji wa teknolojia zilizogunduliwa mahali pengine, teknolojia
ambazo tunauziwa kwa bei mbaya sana.”

    Hatutaki tu kuuona ukweli. Kwa mfano, ukimuandaa mtaalamu wa Kilimo
hadi anapata shahada, akija kuwa Bwana shamba kijijini, je elimu yake
atawapatia wale wakulima kule vijijini kwa lugha gani? Kiingereza,
alichojifundishia au kwa lugha ambayo walengwa wanaielewa? Kwa vile
madhumuni ya elimu ni kwa watakaobahatika kuipata wawagawie maarifa na
huduma wengine, kwa nini sasa tunalazimika hapa hapa nchini ambako
tuna lugha yetu, kuifundisha elimu hiyo kwa lugha ya kigeni na ya
kikoloni? Kama elimu utaipata kutoka China, ni dhahiri lazima
kujifunza kwa Kichina.

Katika kitabu “Focus on fresh data on the Language of Instruction
debate in Tanzania and South Africa” kilichoandikwa na Brigit Brock-
Utne, Zubeida Desai na Martha Qorro, mwaka 2006, ikiwa ni sehemu ya
matokeo ya tafiti za LOITASA (Language of Instruction in Tanzania and
South Africa) ambayo  ni Mradi wa NUFU (The Norwegian Programme for
Development Research and Education) ulioanza mwaka 2001 na
unaomalizika mwishoni mwa mwaka 2011, imebainishwa  jinsi lugha ya
Kiingereza ilivyokuwa tatizo katika ufundishaji kwenye shule za
Sekondari nchini Tanzania.

Utafiti wa LOITASA ulifanywa katika shule mbili za Sekondari kwa
kutumia utaratibu wa kufundishia somo la Baiolojia – darasa moja kwa
Kiingereza na darasa jingine kwa Kiswahili. Kwa mujibu wa kitabu
hicho, katika darasa lililokuwa linafundishiwa Kiingereza, wanafunzi
walionekana kutochangamka na hawakuelewa kilichokuwa kinaendelea,
wakati lile la Kiswahili, wanafunzi walikuwa wanachangia kwa uelewa wa
hali ya juu na ukawepo mjadala wenye tija baina ya mwalimu na
wanafunzi.

Tume ya Rais ya Elimu, iliyojulikana kuwa Tume ya Makweta (mwanasiasa
na mwanataluma mashuhuri nchini) ilitoa mapendekezo ya kutaka
Kiswahili kitumike katika ngazi zote, hatua kwa hatua, kuanzia kidato
cha kwanza mwaka 1985  na Chuo Kikuu kuanzia mwaka 1992.  Mapendekezo
hayo mpaka sasa hayajatekelezwa.

Mapema tangu mwaka 1953, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO), lilitoa azimio  lililosema, pamoja na mambo
mengine, ni vema hasa kwa elimu ya msingi kwa watoto wadogo,
kuwafundisha kwa lugha wanazozielewa vizuri na hasa lugha za mama zao.
Sasa, kama wataalamu wamekwishamaliza kazi yao na kuthibitisha kuwa
Kiswahili ni lugha inayojitosheleza kwa msamiati karibu katika kila
fani, mbona Kiswahili hakitumiki nchini katika kufundishia, hasa elimu
ya juu? Kwa nini?

    Jibu la uhakika ni kwanza, matokeo na athari ya kutawaliwa na
Waingereza na hivyo kupandikiza ndani ya akili zetu hali ya
kutojiamini wenyewe, kuanzia katika lugha na hata katika maeneo
mengine. Kazi yetu ni kuwategemea wengine, wa nje tu. Pili, kasumba tu
ya kawaida kwamba Kiingereza ndiyo elimu na tatu ni kusita kuchukua
uamuzi.

Sera; Dira, hazitekelezwi

    Sera ya Elimu ya Mwaka 1995 nchini inasema kuwa Lugha ya Kufundishia
ni Kiswahili na Kiingereza. Sera hiyo inafanyiwa mapitio, lakini
katika maandiko ya  awali ya marekebisho yanayopendekezwa, haionekani
kwamba uamuzi unafanywa wa kukitumia Kiswahili katika ngazi zote.
Kwa mfumo wa sasa nchini, kuanzia shule ya awali hadi darasa la saba,
lugha ya kufundishia ni Kiswahili, lakini kuanzia kidato cha kwanza
hadi kwenye vyuo, lugha ni Kiingereza. Ingawa ukweli ni kwamba hata
kwenye vyuo, mwalimu akiona haeleweki kwenye ukumbi wa mhadhara, huwa
anabadilisha lugha na anatumia Kiswahili na mara mambo yanabadilika na
kwenda vizuri.

    Katika Sera imetamkwa rasmi kuwa: “Serikali itakuza elimu ya awali ya
watoto wenye umri wa miaka 0-6. Elimu hii itahakikisha kudumishwa kwa
maadili yetu kiutamaduni”. Lakini hali halisi ya sasa, ni tofauti na
tamko la Sera. Siku hizi kuna shule za binafsi nyingi zilizochipukia
zinazofundisha kwa Kiingereza, ziitwazo kwa Kiingereza “English-Medium
Schools”, hata kwa zile za elimu ya awali, tena nyingine ada ni lazima
kulipwa kwa fedha za kigeni, hasa za Kimarekani, Dola! Kwa msingi huo,
haitawezekana kuwa elimu hiyo “itahakikisha kudumishwa kwa maadili
yetu ya kitamaduni”, kama yenyewe inatolewa kwa lugha ya kigeni ya
kikoloni na kulipiwa  kwa fedha za kigeni!

    Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, sehemu yake inasema: “Tanzania haina
budi ijijengee misingi ya kujitegemea inayotokana na mazingira ya
ukombozi wa kisakolojia, kifikra na kuweza kujiamini ili jamii iweze
kuamua kuliongoza gurudumu lake la maendeleo kwa lengo la kutosheleza
mahitaji ya msingi ya watu wote, wanaume, wanawake na watoto”. Je,
tutaliweza hilo kwa kufundishia lugha ya kigeni, ya kikoloni?

Ni siasa, uchumi na utamaduni

Karibu nchi zote duniani, zinatumia lugha zao kufundishia. Lakini
katika Afrika karibu nchi zote (isipokuwa Ethiopia, inayotumia lugha
yake ya Amharic na maandishi yake, pamoja na  nchi za Kaskazini mwa
Afrika zinazotumia Kiarabu na maandishi yake) zinatumia lugha za
kigeni za Kiingereza, Kifaransa au Kireno, zilizorithiwa kutoka kwa
Wakoloni hao. Haishangazi basi kuwa miaka 50 sasa tangu ukoloni
uondoke, bado tunakuwa tegemezi kutoka kwa wakoloni hao.
    Msomi B.F.P. Masele, katika makala yake yenye kichwa cha habari:
“Kiswahili au Kiingereza? Siasa na lugha muafaka ya
kufundishiaTanzania,” alikariri “janga” lilioikuta nchi ya Afrika ya
Madagaska iliyoamua mwaka 1975 kutumia lugha yake ya asili ya
Kimalagasi, inayofahamika na kutumika kwa ufasaha zaidi nchini humo,
katika nyanja zote za maisha ya watu, ikiwa ni pamoja na kufundishia
elimu ya awali hadi vyuo vikuu.

    Kwa mujibu wa Masele, baada ya Madagaska kukumbwa na hali mbaya ya
kiuchumi, nchi ya Ufaransa, iliyokuwa ikiitawala zamani, ilishinikiza
kuwa Kimalagasi kifutwe kama lugha ya kufundishia au kutumika katika
shughuli nyingine rasmi kitaifa. Serikali, ikalazimika kukirudisha
Kifaransa kuwa lugha kuu Madagaska baada ya kupewa ahadi ya fedha
kutoka Ufaransa ili itatue matatizo yake ya kiuchumi. “Hili ni somo
muhimu sana kwa Tanzania na nchi zote zinazofanana nayo”, anasema
Masele.

    Masele anaongeza: “Utekelezaji wa maamuzi ya matumizi ya Kiswahili
kufundishia katika ngazi zote za elimu umekuwa mgumu ingawa jambo
lenyewe liko wazi kiutafiti, kitaaluma, kipedagogia na kimantiki tangu
zamani. Ugumu unatokana na ukweli kwamba, ingawa Kiswahili ni suala
linalohusu lugha, mizizi yake ya fitina imejikita katika uwanja nyeti
wa siasa, huku siasa hii ikifungamana na masuala ya uchumi na
utamaduni. Bila ya kuichokonoa mizizi hii kutoka katika siasa, uchumi
na utamaduni ilikojificha, si tu itakuwa vigumu, bali haitawezekana
kukithamini Kiswahili”.

    “Waafrika,” Masele katika makala hiyo amemnukuu mtaalamu mwingine
nchini,  M.M. Mulokozi akisema: “ni watu wa pekee duniani waishio kwa
vitu vya kuazima; utamaduni wa kuazima, dini za kuazima, lugha za
kuazima, majina ya kuazima, teknolojia ya kuazima, fasihi/fani za
fasihi za kuazima, nywele na rangi za ngozi za kuazima, sanaa za
kuazima, mavazi ya kuazima, vyakula vya kuazima…vitu ambavyo wengi
wetu vinatufanya tuwe viumbe bandia, vichekesho vya dunia.”
Hivyo basi ni  maoni yangu kuwa, kwa vile miaka 50 imekwishapita tangu
uhuru bila ya kukifanya Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia nchini
katika ngazi zote,  maandalizi yaanze sasa kwa kufundishia Kiswahili
Sekondari na baadaye Chuo Kikuu. Kwa namna hii, utamaduni wetu
utaendelezwa, vijana wetu wanaopata elimu watajijua vizuri wanatoka
wapi na wanakwenda wapi na watakuwa na kitu cha kujitambulisha kama
taifa. Isitoshe elimu  itapanuka mno  na taifa litapata wataalamu
wanaoweza kujitegemea na wazalendo na hivyo utajengeka utamaduni wa
kuwaamini wataalamu wetu na siyo wa nje. Ikifikia hapo, kasi ya
maendeleo nchini itakuwa kubwa mno, kwa muda mfupi sana, kiajabu.
                    (mwisho)

•    Saidi Nguba aliwahi kuwa Mhariri Mtendaji wa Magazeti
yanayochapishwa kwa Kiswahili ya UHURU (2000 – 2004) na Mwananchi
(2004 – 2005). Hivi sasa ni Mwandishi wa Habari wa Waziri Mkuu. Haya
ni maoni na mawazo yake binafsi.
    Simu: 0754 -388418, Barua-Pepe: sanguba@gmail.com

LOTS OF SCHOOLING, LITTLE LEARNING

CLICK IMAGE ABOVE TO ENLARGE IT

TANZANIAN UNION: CONSENT OR COERCION?

"I fear [Zanzibar] will be a big headache for us" - J.K. Nyerere

"In January [1964] a new factor intervened, the Zanzibar revolution, followed by army mutinies in all three East African countries. In the case of Tanganyika, the mutineers almost succeeded to overthrow the government with Nyerere disappearing for a whole week. In all these countries, British troops were invited to put down the mutinies and disarm the mutineers. Nyerere's nationalist pride was deeply hurt...The mutiny together with the earlier events in the Congo  culminating in the murder of Patrice Lumumba and the assassination of President Olympio of Togo left Nyerere with a deep sense of insecurity. Survival became his major concern, at least during those early years of independence. The Zanzibar revolution further endangered the survival of the mainland government, as it threatened to invite Cold War conflict to its doorstep. Nyerere came under severe pressure from Western governments as they relentlessly cajoled him to do something about communism next door. As a nationalist, he probably resented being told by the former colonial power what to do, though as a politician he must have realised he had little choice. Until the last moment, Nyerere was hoping that Zanzibar would be brought into a federation of more than two-states even if it meant only with Kenya.  When that effort failed, Nyerere and Karume signed the Articles of Union, which had been prepared in great secrecy [by "Nyerere's expatriate legal advisers"].... Nyerere's decision was pragmatic, to survive, contrary to his own Pan-Africanist pronouncements. His own rabid anti-communism may also have contributed. Yet, left on his own, it is quite likely that Nyerere might not have made the decision to go it alone with Zanzibar. Once formed, Nyerere became almost paranoid to maintain the Union. Short of outright military force, he deployed every tool - including manipulation and Machiavellism - available in the political kitbag to maintain the Union, in the process trampling on Pan-Africanist principles of which he himself was a great and most articulate proponent"" - Issa G. Shivji on Pan-Africanism or Pragmatism? Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union

Tuesday, April 24, 2012

Comparing Women's land rights challenges

Women's land rights challenges in the Netherlands

Marc Wegerif

I recently attended a conference in the Netherlands (www.agricultureinanurbanizingsociety.com/UK) and as part of the conference had an opportunity to go on a field trip to some farms. I joined a trip that was to visit women entrepreneurs on farms and was of course interested in women's land and property rights. Thought you may be interested to hear about women's land and property rights from a different context so my notes are below. 

Women’s property rights 

A highlight of the "agriculture in an urbanising society" conference was getting to visit some Dutch farms involved in multi-functional agriculture. It was an opportunity to meet farmers and an opportunity to explore an issue of particular interest in my work: women’s land and property rights. 

On one farm there was an interesting tenancy arrangement that gave the husband of the women entrepreneur a lifelong tenancy right on land belonging to a private estate. He had got this from his father and it is inheritable by his children. The new large dairy building that they have built on the land is also registered in his name. If the family should decide to give up the tenancy right the land owners will pay him out the value of the building. When asked about the inheritability of the tenancy right the farmer (the husband) first confirmed that his son could inherit it. When asked about his daughters he acknowledged that it could also be inherited by them. His explanation for his wife not being included as having a tenancy right was that the owners would not like that as it does not give them security: “if I were to pass away she may bring another man”. That another man, from outside the family, might be brought in by the women should she have land rights is a classic fear I have heard expressed in many African villages. It is of course rooted in the assumption of a patrilineal passing on of rights to land and property that does not see any problem with the risk of the man bringing another woman in the future. The woman farmer declared herself happy with the arrangement and explained that she has a share of the business they run (excluding the land and new building), which is better than many women have as some, according to her, have no legal rights despite efforts to educate women on farms about the importance of securing legal rights. 

On another farm a women entrepreneur was running an accommodation operation that provides group, family and weekend getaways. She was coy about whether her operation made more money than the work her husband who runs the dairy operation, but the figures that were shared indicate she clearly made more money. The farm had been passed down from her husband’s father and grandfather to him and his brother.  She had, however, managed to get her name on the title and as a joint owner of the business. When asked how she managed this she explained the trust that had been built through eight years of marriage (during which time she lived on and developed the property of her husband and his brother) and that the opportunity opened up when the two brothers split the land between them. She also said that maybe she was “very sneaky”. This was said with humour and I am not suggesting it confirms that she was actually sneaky, but it is a reference to the classic assumption and often reality that women need to be ‘sneaky’ or manipulative to gain rights in the context of weak formal rights. 

On a third farm the women entrepreneur ran a business that had made owning and living on a piece of otherwise unviable (due to size and other limitations) farm land an option. The land and the business were, however, owned by her parents on land belonging to her parents. I did not manage to confirm, but would bet, after what I found out on the day, that it is in the name of her father. 

On all the farms there was a strong gender division of roles and an apparent deference to the husbands contribution even when the woman’s initiative was clearly of great economic and wider importance to the farm operation. We were treated to explanations such as “I look after the small animals and the administration, my husband does the hard work”. 

From an African perspective there is often an assumption that women in Europe, especially liberal countries like the Netherlands, have strong land and property rights. It was interesting on this short visit to find that women in Europe apparently face many similar challenges, related to asserting their rights, to those encountered by African women. It was fascinating to also hear a similar discourse of excuse and justification. None of the above is intended to undermine the role these women are playing, in fact for me it highlights that they are doing a great job despite the obstacles that still exist. 

MAUAJI YA HALAIKI YA WATOTO WA TANZANIA

MAUAJI YA HALAIKI YA WATOTO WA TANZANIA KUPITIA KATIKA LUGHA YA KUFUNDISHIA SEKONDARI NA VYUONI

F.E.M.K Senkoro

Makala kwa Ajili ya Warsha ya Usambazaji wa Matokeo ya Tafiti Kuhusu Kuhusu Lugha ya Kufundishia Sekondari na Vyuoni Tanzania Desemba 5, 2006 F.E.M.K. Senkoro Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 

Kwanza kabisa, nieleze matukio mawili ambayo nimekutana nayo hapahapa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Asubuhi moja nilikutana na mwanafunzi wangu mmoja akiwa anatoka jasho chapwachapwa mwili mzima. Kwa vile yalikuwa majira ya baridi hapa Dar es Salaam, nilimwuliza kama anaumwa. Alinijibu kuwa hakuwa anaumwa, bali alikuwa na uhudhurishaji wa swali la semina siku hiyo. Kidogo alinishangaza kwani katika semina zangu na hata katika mitihani yangu alikuwa akifanya vizuri sana. Sikuelewa kwa nini alikuwa anaogopa semina ile hadi aliposema, "Afadhali semina yenyewe ingelikuwa ya Kiswahili. Hii ni kwa Kiingereza, na sijalala usiku kucha, na hata chamshakinywa kimenishinda asubuhi hii. Unajua Profesa, si kwamba mawazo sina, ila siwezi kuyatoa vizuri kwa Kiingereza, na siwezi hata kuonyesha hisia zangu kikamilifu kwa lugha hiyo. Basi tu. " Nilidhani anatania, lakini nilipomwangalia usoni nilijua kuwa hakuwa anatania hata kidogo. Niliamua kuwauliza wanafunzi mbalimbali kuhusu hali hiyo, na karibu wote wakanijibu kuwa hali ile huwapata kila wanapokabiliwa na zoezi la kuhudhurisha kwa Kiingereza katika semina. Na hawa hawakuwa wa mwaka wa kwanza tu, bali hadi wa mwaka wa nne wote walilalamikia hali hiyo.

 Tukio la pili lilinitokea hivi karibuni sana nilipokaribishwa na mwalimu mwenzangu kwenda kutoa muhadhara kuhusu ngano ambazo zinavuka mipaka ya kijiografia na kiutamaduni. Muhadhara huu ulikuwa kwa Kiswahili. Na mwishoni niliwaeleza wanafunzi kuwa nilikuwa na kifikirishi kuhusu mada ile na kwamba ningempatia mwakilishi wa darasa kitini hicho. Nilipowaeleza tu kuwa kifikirishi chenyewe kilikuwa kwa lugha ya Kiingereza, wanafunzi wote waliguna na kuonyesha kukata tamaa. Walionyesha dhahiri kuwa kifikirishi cha Kiingereza kisingewafikirisha kwani wasingeambulia kitu. 

Tutarejelea matukio haya mawili hapo baadaye. Kwa sasa ningependa kulihusisha suala la lugha ya kufundishia na Katiba Mama ya nchi yetu. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza kuwa kila mtu ana haki na uhuru wa kutoa maoni yake, na pia uhuru wa kujieleza, kutafuta, kupokea na kusambaza mawazo na habari kupitia chombo chochote kile bila kujali mipaka ya kitaifa; pia ana haki ya uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa. Inasisitiza pia kuwa kila mtu ana haki ya kutoa fikra zake kwa uhuru kabisa. Nimekuwa nikiwaza sana kuhusu haki na uhuru huo, sambamba na suala zima la lugha ya kufundishia katika sekondari na vyuo nchini Tanzania, na nimekuwa nikijiuliza kama serikali haiendi kinyume na Katiba ya Jamhuri kwa kuwalazimisha waalimu na wanafunzi kutumia lugha ya kufundishia ambayo licha ya kuwa ni ngeni kwao, tafiti nyingi zinaonyesha pia kuwa hawaimudu kabisa, kwa hiyo hawana uhuru wala haki ya kujieleza kwa lugha wanayoiweza, lugha inayobeba utamaduni na dhana nyingi wazielewazo. 

Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi kuhusu hali ilivyo katika shule za sekondari na vyuo vingi nchini Tanzania ambako watoto wa Kitanzania wamepigwa marufuku kuongea lugha zao, ikiwemo ile ya taifa, Kiswahili, na hata huadhibiwa kwa kubebeshwa matambara machafu au hata mawe na magogo pindi wanapokutwa wakizungumza lugha hizo. Badala yake wanalazimishwa kuongea Kiingereza, lugha ambayo ni ngeni kwao na imebeba tamaduni ambazo ni ngeni kwao. Watoto hao basi, hawana haki ya kutoa fikra zao kwa uhuru hata kidogo. Maswali yamekuwa mengi zaidi niyawazapo haya sambamba na kauli ya Mwalimu Nyerere kuwa taifa lisilo na utamaduni wake lenyewe ni taifa lisilo na uhai, ni taifa lililofilisika lisilo na utu wala roho yoyote. Lugha ni sehemu muhimu sana ya utamaduni wa jamii; na kwa hakika lugha ni kielelezo na kielezo cha utamaduni huo. Lugha ni sehemu mojawapo ya ufahari wa kitamaduni wa jamii fulani. Ndio maana Mwingereza anajivunia sana lugha yake ya Kiingereza, na vivyo hivyo Mfaransa, Mreno, Mjerumani, Mjapani, Mnorwei, Mdenish na wengi wengineo. Kinyume chake, Mtanzania anapigwa marufuku kuitumia na kujivunia lugha yake; badala yake anapoitumia anaadhibiwa kwa kubebeshwa tambara bovu, jiwe, au gogo. Ni kama kwamba, ndani ya ubongo wake, Mtanzania anatakiwa aionee aibu lugha yake ya taifa, na aikumbatie lugha ya utamaduni wa mtawala wake wa zamani. Anatakiwa aione lugha yake ya taifa kuwa ni sawa na tambara bovu, jiwe, au gogo. 

Matokeo ya hili ni kwamba tunamlea mtoto wa Tanzania aukane utu wake, na awe na woga wa kujieleza. Tunamfanya ajinyamazie tu kwani anaogopa kujieleza kwa lugha anayoimudu asije akaadhibiwa, na anaogopa kujieleza kwa lugha ngeni asiyoweza kujinasibisha nayo hata chembe, kwani anajua kuwa haijui na atakayoeleza yataonekana kuwa ni kichekesho. Nimekuwa nikiwaza sana kuhusu utandawazi ambao umechangia katika kumfanya mtoto wa Tanzania azidi kujivunia lugha na utamaduni wa kigeni, lugha na utamaduni wa Mwingereza, kwa kumfanya aamini kabisa, yeye na wazazi wake pamoja na watunga sera, kuwa akifundishwa kwa kutumia lugha hiyo ataimudu na itamsaidia apate kazi na aweze kuwasiliana na watu wa mataifa mengine. 

Nimekuwa nikijiuliza inakuwaje Wachina, Wajapani, Wakorea, Waswidi, na wengi wengineo ambao wanatumia lugha zao kufundishia vijana wao, bado wamepata kazi za kimataifa, wamefaulu mitihani yao, wameendeleza nchi zao na wameweza kuwasiliana na watu wa mataifa mengine. Hawa wamemudu kuyafanya yote hayo kutokana na kuthamini na kuzitumia lugha zao kufundishia shuleni na vyuoni. Utandawazi umetumika kama kisingizio cha kuigeuza dunia si kuwa kijiji kidogo bali ni msitu mdogo ambamo wanyama wakubwa sasa wanawapata wanyama wadogo kama mlo wao kiurahisi sana. 

Utandawazi umekuwa chanzo cha wakubwa kuwanyamazisha wadogo, na, kama mtu mmoja alivyowahi kusema, badala ya tangazo la "Punguza mwendo, kazi inaendelea mbele", utandawazi umeweka kibao cha "Nyamaza, mbele yanafanyika maendeleo!" Wale walionyamazishwa kwa kuaibishwa wakijieleza kwa lugha zao, wanatakiwa wabaki wakiwa wameduwaa wakati wenzao duniani kote wakipiga hatua nyingi za maendeleo. Badala ya kuwa washiriki na washirika wa maendeleo, wamefanywa wabaki kuwa watazamaji tu na kuelekezwa la kufanya, tena wakati mwingi wakielekezwa pabaya kuhusu maisha yao bila wao kuling'amua hilo kwani limeelezwa kwa lugha na utamaduni usio wao; hadi wanaposhituka mambo yakiwa yameharibika. 

Sitashangaa kuona kuwa mojawapo ya vyanzo vya watu kuweka sahihi katika mikataba ambayo inaonyesha dhahiri kuwa hawaielewi, ni suala la lugha ambapo historia inajirudia sawa na pale Karl Peters alipowafanya mababu zetu waridhie kutwaliwa kwa ardhi yao kwa kusaini mikataba wasiyoielewa. Mimi nina uhakika kabisa kuwa chanzo cha kubaki nyuma kimaendeleo ni ule ukimya utokanao na sera ya lugha ya elimu inayowanyamazisha watoto wa Tanzania, kwa kuwalazimisha wasijieleze wanavyopenda kwa kutumia lugha yao ya taifa, na badala yake kuwalazimisha, bila mafanikio, wajieleze kwa lugha ngeni kwao. 

Iko hadithi moja ambayo mimi hupenda kuirejelea kila mara ninapoongelea suala la lugha ya kufundishia. Ni hadithi itokayo katika kitabu cha Charles Dickens cha Hard Times chenye wanafunzi fulani wawili kwenye shule ya mjini, ambao wanaombwa watoe maelezo kuhusu farasi. Mmoja, msichana aitwaye Jupe, ameishi na farasi maisha yake yote huko kijijini, na mwingine, mvulana aitwaye Blitzer, amesoma tu kuhusu farasi katika Encyclopedia. Jupe anashindwa kueleza farasi ni nini kwani katakiwa afanye hivyo kwa lugha ya kisomi, na Blitzer ambaye hajawahi hata kumwona wala kumgusa farasi anafaulu kueleza farasi yukoje kwa kutumia maana za ki-encyclopaedia. Watoto wetu tumewageuza kuwa Jupe, ambaye pamoja na kuelewa fika kuhusu farasi, kanyimwa haki ya kueleza farasi ni mnyama wa aina gani kwa kulazimishwa ashikile maana za kikamusi za mnyama huyo. Ameishi na kuwagusa na kuwajua fika wanyama hao, lakini elimu inamlazimisha asieleze kuhusu awajuavyo bali awaeleze kama kamusi zinavyowaeleza. 

Vivyo hivyo, kwa Tanzania, tafiti nyingi, mathalani zile zinazotokana na mradi wa utafiti kuhusu lugha ya kufundishia Tanzania na Afika ya Kusini (LOITASA) zimedhihirisha kuwa wanafunzi wengi mno wangeweza kufaulu mitihani yao vizuri zaidi iwapo wangefundishwa kwa Kiswahili, kuulizwa maswali kwa Kiswahili na kutakiwa wajibu kwa Kiswahili. Na zimeonysha dhahiri kuwa kama wangefundishwa hivyo, hata lugha za kigeni kama Kiingereza wangezimudu vizuri zaidi. Lakini, badala yake, wameulizwa maswali hayo kwa Kiingereza – lugha ambayo hawaijui, na hawawezi kujinasibisha na utamaduni wake. Wamegeuzwa kuwa akina Jupe kwa kunyimwa uhuru na haki ya kujieleza. 

Haya yote yanatuongoza katika mjadala wa maana ya lugha, maana ambayo sitaikita katika malumbano ya kitaaluma, bali nitaielekeza katika hali halisi ya lugha ya kufundishia nchini Tanzania. Tusemapo kuwa lugha ni chombo cha mawasiliano baina ya mtu na mtu, tuna maana kuwa mawasiliano yoyote, yawe baina ya mzazi na mtoto, marafiki, mwalimu na mwanafunzi, yanahusu matumizi ya lugha. Lugha na ishara na taswira zinazowakilishwa nayo hufinyanga na kuathiri tabia na mikabala aliyo nayo mtu. Maneno yanayotumika humweka msemaji katika nafasi fulani miongoni mwa watu wengine – na nafasi hiyo huweza kuwa ile ya masafa marefu au mafupi baina ya msemaji huyo na wenziwe, au inaweza kuashiria mamlaka au ubia baina ya wahusika. Nafasi hiyo huwaathiri wahusika kwa namna moja ama nyingine, wakati mwingine kwa kuwadarakisha au hata kuwadogosha, kuwashawishi na kuwahimiza au kuwakatisha tamaa, kuwafanya wajione wako kwao au kuwagenisha. Kwa hakika, matumizi ya lugha wakati huohuo yanaingiliana na mtazamo wa kitamaduni kwani ili kusiwe na uhusiano hasi baina ya watumiaji wa lugha fulani, yale mambo ya ndani ya utamaduni mahsusi unaobebwa na lugha mahsusi hayana budi kueleweka kwa wote wanaowasiliana kwa lugha hiyo, la sivyo, mawasiliano yatakuwa ya upande mmoja tu. 

Historia ya jamii zetu nyingi za Kiafrika inaanzia pale ambapo Mwafrika alikuwa anajitawala, anajitegemea na anajiletea maendeleo yake yeye mwenyewe. Historia hii ilipoingiliwa na ukoloni na ubepari, ukawa mwanzo wa kudidimia kwa maisha ya Mwafrika. Ukoloni na ubepari havikuja vivi hivi tu. Vilitanguliwa na kutawaliwa kimawazo kwa Mwafrika huyo, akaletewa dini, mila, desturi na tamaduni za nje, zikiwemo lugha ngeni, akafanywa aviabudu hivyo na kuvidharau vyote vilivyokuwa vyake. Alifanywa azione dini, mila, desturi na tamaduni zake kuwa ni za kishenzi zisizofaa mbele za mtawala wake. Akaiga kila kitu cha nje, na kudharau kila kitu chake. 

Vita vya uhuru vililenga kumkomboa Mwafrika huyo ili aondokane na minyororo ya ukoloni na ubepari. Vilinuia kumtoa Mwafrika katika lindi la kujidharau na kuudharau utu wake. Lakini ubepari hauruhusu mambo kama hayo. Ubepari hujigeuza nyuso zake kama kinyonga, na kama awali ulikuwa joka la vichwa saba, sasa, baada ya uhuru wa bendera na wa wimbo wa taifa ubepari uligeuka kuwa joka linalotabasamu, lenye vichwa sabini, na kila uchao vichwa hivyo huongezeka. Kichwa cha hivi karibuni ni kile cha utandawazi ambao ni dhahiri kuwa ni kielelezo cha kuanguka kwa utaifa wa Mwafrika na kukita kwa mizizi ya kiliberali. Tabasamu la dudu hili liko ndani na nje ya mataifa mengi ya Kiafrika. Wako viongozi ambao tabasamu hilo limewakatisha tamaa kabisa kuhusu utu wa watu wao, na wamebaki kushangaa huku wakishangilia tabasamu hilo, na kulisifu tabasamu hilo kwa kuliruhusu lishamiri kwa njia nyingi, ikiwemo ile ya kurudisha mikabala ya ukoloni, mikabala inayosifu vya kigeni na kudharau vya "wenyeji". Hapo ndipo tuonapo mawaziri wetu wa elimu wakikikumbatia Kiingereza, na wakidharau tafiti mbalimbali zilizofanyika zinazoonyesha kuwa watoto wetu hawaambulii chochote madarasani wanapofundishwa kwa lugha hiyo ya kigeni. 

Hapo ndipo tuonapo zikichipuka shule nyingi ziitwazo za kimataifa, zenye kutumia lugha ya Kiingereza kuwafundishia watoto wetu, tangu chekechea hadi sekondari. Tabasamu hili la ubepari ambalo limejengeka ndani ya dude liitwalo utandawazi ndilo linaloleta programu kama ile ambayo ghafla inamwonyesha Waziri Mkuu wa Uingereza akiwa na huruma ya ajabu kwa Afrika hadi kuunda Kamisheni ya kuushughulikia umasikini ambao, kwa hakika, nchi yake ilishiriki mno kuuleta Afrika na bado inashiriki kuusambaza duniani kote, hata inapolazimu kwa mabavu. Na viongozi wetu wameonyesha kulifurahia tabasamu hilo la Blair walipoteuliwa kuwa wanakamati wa kamisheni hiyo. Pamoja na hayo yote, tabasamu hili linajitokeza pia katika juhudi za wazi kabisa za Baraza la Uingereza au British Council la kukisambaza Kiingereza duniani kwa kumwaga pesa nyingi kwa wizara za elimu kwa kile kiitwacho programu za kuimarisha Kiingereza. Kama tujuavyo, ubepari hugeuza kila kitu kuwa bidhaa sokoni, na lugha ya Kiingereza ni mojawapo ya bidhaa muhimu sana kwa Waingereza kiasi kwamba mapato yatokanayo na kuuzwa kwa bidhaa hii duniani hutangazwa kila mwaka katika bajeti ya Uingereza. Mfumo wetu wa elimu, hasa sera zake za lugha ya kufundishia, unatufanya sisi tuwe wateja wakubwa wa bidhaa hii, huku tukiikanyagakanyaga bidhaa yetu muhimu, lugha yetu ya Taifa, Kiswahili. Hauhitajiki utafiti kudhihirisha kuwa hakuna nchi hata moja duniani iliyopata kuendelea kwa kutumia lugha ya kigeni. 

Nchi zote tuonazo zikiinukia kimaendeleo leo hii, kwa mfano zile za Asia na Uchina, zimeendelea na zinazidi kuendelea kwa kutumia lugha zao. Nchi hizo zinaendelea kujitegemea kimawazo na kiuchumi kwa vile masuala yote muhimu yamo katika mawazo yanayoelezwa kikamilifu kwa lugha zao. Na imeshadhihirika kiutafiti, kuwa wale wanaotumia lugha zao kufundishia shuleni na vyuoni, humudu kujifunza lugha nyingine za kigeni vizuri zaidi. Hali nchini Tanzania ni kinyume na hali katika nchi hizo. Twaelekea kuamini kuwa tunaweza kupiga hatua ya maendeleo kwa kutumia Kiingereza, na hata mara nyingi, katika kuidharau lugha yetu ya taifa, Kiswahili, utasikia mtu akisema sentensi kwa Kiswahili halafu anasema, "Kwa lugha ya Kitaalamu, maana yake ni kwamba...." akimaanaisha kuwa kwa Kiingereza aliyoyasema yana maana fulani. Huu ni uleule utumwa ambao tumeutaja awali, wa kudharau chetu na kukumbatia cha kigeni. 

Tumefikia hata hatua ya kuaminishwa na huo utandawazi kuwa kuna utamaduni wa kimataifa bila kujua kuwa popote pale palipo na mwenye nguvu na mnyonge, utamaduni wa mwenye nguvu huutawala ule wa mnyonge. Na hili linaanzia hata katika ngazi ya kitaifa ambako suala la lugha ya kufundishia ni la kitabaka. Kimataifa, tunaona leo hii jinsi ambavyo utamaduni wa Marekani na wa mwenza mkuu wa Marekani, Uingereza, umetawala duniani. Ni katika utawala huu wa kitamaduni ndimo mlimojificha siri za kuabudu Kiingereza na Ukingereza bila kujali athari zake katika utoaji wa elimu nchini Tanzania na kwengineko Afrika. Lugha na utamaduni ni vitu ambavyo vimo ndani ya ubongo na roho ya jamii. Tunapowalazimisha watoto wetu washindwe kujifunza na kujieleza kwa lugha yao iliyobeba dhana mbalimbali za utamaduni wanaouelewa, tunaunda lile taifa alilolikemea Mwalimu Nyerere, taifa mfu lisilo na uhai. Tunawaandaa watoto wetu wawe wazungu weusi, tena wazungu wenyewe ni wazungu koko wasio na nyuma wala mbele kwa kuwadanganyia gololi zinazong'ara huku wakizitupa dhahabu za tamaduni zao na lugha zao. 

Tunashuhudia historia ikijirudia! Tunapowafanya vijana wetu watokwe jasho na washikwe na woga kila inapowabidi kujieleza kwa lugha isiyo yao, wakati ambapo wangejengewa misingi ya kujieleza vizuri kwa lugha ya utamaduni wao wasingepata matatizo hayo, hatuendi tu kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu haki ya kupata elimu na ile ya kutoa maoni na kujieleza kwa lugha anayoimudu mtu, wakiwemo wanafunzi wetu, bali, kwa hakika tunafanya mauaji ya kiakili na kiroho ya watoto wetu, mauaji ya halaiki ambayo yatatufanya tuhukumiwe na historia.

Roy Singham on Software Colonialism in Africa

Monday, April 23, 2012

MSHINDI WA TUZO YA MWANASAYANSI YA MAMA KAMM

MWANAFUNZI: SHAHADA YA UZAMIVU

TUZO: 

Tuzo hii inatolewa kwa mara ya kwanza mwaka huu na imeanzishwa rasmi na Dakta Mwele Malecela ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR. Lengo la tuzo hii  kuenzi jitihaba za Mama Maria Kamm katika kuhamasisha wanawake kushiriki katika Masomo ya sayansi wanapokuwa mashuleni, jambo ambalo limesaidia kuongeza idadi ya watafiti wa Kisayansi nchini na hata NIMR.


Mama Maria Kamm alikuwa Mwalimu Mkuu maarufu wa Shule ya Sekondari wa Wasichana ya Weruweru ambaye alibobea katika miaka ya 1970, kwa umahiri wake katika kazi na kwa kuzingatia maadili halisi ya kazi ya ualimu.


Mama Kamm alikwa ni miongoni mwa walimu wachache kwa kipindi hicho waliopata Shahada ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Notre Dame.
Tunamuenzi Mama Maria Kamm kwa juhudi zake katika kuzalisha wanawake watafiti na viongozi katika sekta mbalimbali jambo ambalo limechangia kuinua uwezo wa wanawake katika kuongoza na kuleta maendeleo ya jamii.Mkunde Chachage1, Lilli Podola1,2, Petra Clowes1,2, Dickens Kowour1, Anthony Nsojo1, Inge Kroidl2, Leonard Maboko1, Michael Hoelscher2, Elmar Saathoff2 & Christof Geldmacher2 1Mbeya Medical Research Centre, Mbeya, Tanzania; 2Department of Infectious Diseases and Tropical Medicine, University of Munich, Munich, Germany

It has been hypothesized that helminth infections modify HIV susceptibility and disease progression and thus might contribute to the high prevalence of HIV-1 in Africa. Immune system modulation by different helminth infections might contribute to such alterations. The objective was to study immune system modulation of different helminth infections (A. lumbricoides, Trichuris trichiura, Hookworms, S. haematobium and S. mansoni) in relation to HIV-1 susceptibility and disease progression. Within the region of Mbeya-Tanzania, up to 480 EMINI study participants were recruited and enrolled into the WHIS cohort after diagnosis of helminth species by the Kato Katz method. Helminth infected subjects received antihelmintic treatment at baseline and were followed up at 3 months and 1 year. Immune cell subsets were studied in peripheral blood using polychromatic flow cytometry in fresh, anticoagulated whole blood. HIV- specific CD8 T cell responses were quantified in freshly isolated peripheral blood mononuclear cells using an Interferon gamma (IFNg) ELISPOT assay after stimulation with a pool of 16 HIV peptides containing frequently recognized CD8 T cell epitopes. A total of 300 volunteers have been enrolled to date. CD25+ FoxP3+ CD4 T cells (Tregs) were increased in subjects infected with Ascaris and Trichuris (p<0.05). In HIV+ subjects Treg frequencies were highest (mean 4.1%) with no apparent influence of helminth coinfection. Interestingly, a substantial fraction of Tregs (mean 50%) expressed the HIV co-receptor CCR5, indicating that Tregs could be a potential cellular target for HIV infection. Neither concurrent helminth infections nor their treatment had a significant effect on HIV-specific T cell numbers. Antihelminthic treatment had no beneficial effect on CD4 counts. Preliminary results do not support the hypothesis that helminth infections in general are associated with accelerated HIV disease progression, or depressed HIV-specific CD8 T cell responses that secrete IFNg. Regulatory CD4 T cells might be susceptible to HIV infection due to expression of CCR5.

Sunday, April 22, 2012

HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012

•    Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini
•    Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’

Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 ya wabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu. Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge isipokuwa tu kama; (a) “taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;” Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa “hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri”.

Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo Bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’ hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi. Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni;

…………………………….
Kabwe Zuber Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.

'A Historian's Jackpot': Accessing Lost/Hidden Files

The Foreign and Commonwealth Office (FCO) is making available to the wider public a large collection of lost (or hidden) files from former British colonial territories. According to FCO, these files -  "sometimes known as the 'migrated archives'" -  are being made available between April 2012 and November 2013. Those on Tanganyika/Tanzania are expected to be available in the national archives between September and November 2013. For more information visit http://www.fco.gov.uk/en/publications-and-documents/colonial-administration/. Also click this link to read this conversation on What is the real legacy of colonialism? and this link to read an article on The colonial papers: FCO transparency is a carefully cultivated myth.


Saturday, April 21, 2012

SAHIHI 70: G71 YAWEKA HISTORIA


 1. 1.     Mhe. Rashid Ali Abdallah – cuf
 2. 2.     Mhe . Chiku Aflah Abwao- chadema
 3. 3.     Mhe . Saluim Ali Mbarouk – cuf
 4. 4.     Mhe . salum Khalfam Barwany – cuf
 5. 5.     Mhe . Deo Haule  Filikuchombe- ccm
 6. 6.     Mhe.Pauline Philipo Gekul- chadema
 7. 7.     Mhe. Asaa Othman  Hamad-cuf
 8. 8.     Mhe. Prof.Kuliyokela Kahigi- Chadema
 9. 9.     Mhe.Naomi  Mwakyoma Kaihula – chadema
 10. 10.  Mhe . Sylvester Kasulumbayi- chadema
 11. 11.  Mhe. Raya Ibrahim Khamis  - chadema
 12. 12.  Mhe. Mkiwa Hamad Kiwanga  - cuf
 13. 13.  Mhe. Susan  Limbweni Kiwanga- chadema
 14. 14.  Mhe. Grace Sindato Kiwelu –chadema
 15. 15.  Mhe. Kombo Khamis Kombo – cuf
 16. 16.  Mhe. Joshua  Samwel  Nassari – chadema
 17. 17.  Mhe. Tundu Antiphas Lissu- chadema
 18. 18.  Mhe Aphaxar  Kangi Lugola- ccm
 19. 19.  Mhe susan Anselim Lymo- chadema
 20. 20.  Mhe. Moses Machali – NCCR Mageuzi
 21. 21.  Mhe. John Shibuda Magalle – Chadema
 22. 22.  Mhe. Faki  Haji  Makame- Cuf
 23. 23.  Mhe . Esther Nicholas Matiko- chadema
 24. 24.  Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi- Chadema
 25. 25.  Mhe. Freman  Aikaeli Mbowe- chadema
 26. 26.  Mhe. Kurudhum Jumanne Mchuchuli – chadema
 27. 27.  Mhe. Halima James Mdee-chadema
 28. 28.  John John Mnyika- Chadema
 29. 29.  Mhe. Augustino Lyatonga Mrema- TLP
 30. 30.  Mhe . Maryam Salum  Msabaha- chadema
 31. 31.  Mhe. Peter Msingwa-chadema
 32. 32.  Mhe. Christowaja Gerson Mtinda- chadema
 33. 33.  Mhe. Philipa Geofrey Mturano- chadema
 34. 34.  Mhe. Christina Lissu Mughwai- chadema
 35. 35.  Mhe. Joyce John  Mukya – chadema
 36. 36.  Mhe. Mchungaji  Israel  Yohane  Natse – chadema
 37. 37.  Mhe. Philemon Ndesamburo- chadema
 38. 38.  Mhe. Ahmed  Juma Ngwali- - cuf
 39. 39.  Mhe. Vincent  Josephat  Nyerere- chadema
 40. 40.  Mhe. Rashid  Ali Omar- cuf
 41. 41.  Meshack  Jeremiah Opulukwa- chadema
 42. 42.  Mhe. Lucy Philemon Owenya- chadema
 43. 43.  Mhe. Rachel Mashishanga- Chadema
 44. 44.  Mhe. Mhonga Said Ruhwanya – chadema
 45. 45.  Mhe. Conchesta Rwamlaza – Chadema
 46. 46.  Mhe. Moza Abedi  Saidy- cuf
 47. 47.  Mhe. Joseph  Roman Selasini – Chadema
 48. 48.  Mhe. David Ernest  Silinde- chadema
 49. 49.  Mhe Rose Kamili Sukum  - chadema
 50. 50.  Mhe. Cecilia Daniel Paresso- chadema
 51. 51.  Mhe .Kabwe Zuberi Zitto- Kigoma Kaskazini
 52. 52.  Mhe. Magdalena Sakaya – Cuf
 53. 53.  Mhe Rebecca Mngodo- Cuf
 54. 54.  Mhe. Sabreena Sungura -chadema
 55. 55.  Mhe. Hamad Rashid Mohammed- CUF
 56. 56.  Mhe. Rukia Kassim Ahmed (Cuf)
 57. 57.  Mhe. Mustapha Boay Akoonay (Chadema)
 58. 58.  Mhe. Abdalla Haji Ali (CUF)
 59. 59.  Mhe. Khatibu Said Ali (CUF)
 60. 60.  Mhe. Hamad Ali Hamad (CUF)
 61. 61.  Mhe. Riziki Omar Juma (CUF)
 62. 62.  Mhe  Haji Khatibu  Kai (CUF)
 63. 63.  Mhe. Anna Marystella John Malack -Chadema
 64. 64.  Mhe. Hamad Rashid Mohamed  (CUF)
 65. 65.  Mhe. Rajab Mbarouk Mohamed (CUF)
 66. 66.  Mhe. Thuwayba Idrissa Muhamed (CUF)
 67. 67.  Mhe. Masoud Abdallah Salum (CUF)
 68. 68.  Mhe. Muhamad Ibrahim Sanya (CUF)
 69. 69.  Mhe. Ali Khamis Seif (CUF)
 70. 70.  Mhe. Haroub Muhammed Shamis (CUF)
 71. 71.  Mhe. Amina Amour Nassoro (CUF)


Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP