Loading...

Saturday, April 7, 2012

KWAHERI KANUMBA - MZEE WA MGUNO WA 'MMHH'!

"I am schocked kwa kweli! I can still memorise your voice calling me "big boss" I can't believe it! Ni jumatatu hii ulinipigia nakuniomba nikuandalia safari uende kijijini angalau kwa wiki moja una mengi ya kuongea na kinamama na wakulima kwa ujumla ili ukirudi uweze kuyasemea kwa uhakika, mipango ilishaanza na leo haupo tena. "Big boss" ndio tulikuwa tunaanza safari ya kanumba "the social activist" ila muumba amekupa safari njingine. Sitahau ucheshi wako na upendo kwa wote. Mungu akulaze mahala pema peponi. Ameen" - Mwanahamisi Salimu

"Pole sana Mishy. Mara ya mwisho kumuona Mzee wa kuguna 'Mmhh' ni kwenye ule mkutano mliouandaa. Hizo pozi zake zilikuwa zinatuchekesha. Atakumbukwa" - http://groups.yahoo.com/group/Wanazuoni/message/14597

"Lulu is traumatized. This is not the time to demonize her. As Tanzania mourns let us value life. Fare thee well the mmh harmonizer" - https://twitter.com/#!/Udadisi

"Sina kawaida ya kukutana na wasanii wa filamu Tanzania lakini miezi miwili iliyopita nilijikuta nyumbani kwa Kanumba hapo Sinza Vatican. Nilikutana naye ili kuona uwezekano wake kushiriki katika kipindi kipya cha TV ambacho kitarushwa na kituo kimojawapo cha televisheni cha uingereza kitakachoanza kurusha matangazo yake kutoka Afrika hivi karibuni. Mkutano wetu ulitakiwa kuchukua nusu saa lakini tukaishia kukaa kwa masaa manne. Akanisimulia maisha yake katika tasnia ya filamu na mafanikio aliyopata kwa miaka michache. “Kila mtu akikuona kwenye televisheni, anafikiri wewe ni milionea kwahiyo unaombwa hela na kila mtu. Hali hiyo imenipelekea kukaa nyumbani kama siendi kazini au kuzima simu. Siku ya leo tu, nimetoa milioni moja kuwasaidia watu.” Akaniambia alikuwa amebadilisha mwelekeo wake na kushiriki zaidi katika filamu za Nigeria na Ghana. Apumzike kwa amani!" - Erick Kabendera

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP