Loading...

Wednesday, April 11, 2012

Maneno ya Mama Lulu na Neno La Leo la Mjengwa


Maggid Mjengwa

Ndugu zangu,

Jana amemezikwa Steven Kanumba , kipenzi cha wengi.

Mauti ya Steven Kanumba yanatukumbusha wanadamu ukweli huu; kuwa maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana. Hivyo, lililo jema kwetu wanadamu ni kuishi kwa kutenda yalo mema. Kuwatendea mema hata tunaodhani wametukosea, maana, tutawasaidia kujifunza kutenda mema. Na ni mwanadamu gani asiyekosea?

Na moja ya adhabu kubwa mwanadamu unaweza kuipata humu duniani kutoka kwa wanadamu wenzako ni adhabu ya kutengwa na wanadamu wenzako.

Msichana Lulu ameshapata na anaendelea kuipata sasa, adhabu kubwa sana kutoka kwa wanajamii. Adhabu ya kupewa hukumu ya mauaji na kutengwa na wengine. Lulu , ambaye ni mmoja wa waliokuwa karibu na marehemu Kanumba hata katika dakika zake za mwisho maishani, na ambaye alikuwa mpenzi wa Kanumba, hakuweza kushiriki mazishi ya mpenzi wake. Hiyo nayo ni adhabu kubwa kwa Lulu kupewa na wanadamu wenzake.

Yumkini Lulu ana mapungufu yake kama mwanadamu, lakini, kwa sasa hastahili adhabu kali hiyo kutoka kwa wanajamii. Kwa kosa ambalo hakuna aliye na hakika leo kuwa amelitenda. Ndio, Lulu aweza kuwa mwanadamu mwenye mapungufu yake mengine, lakini , hayo yasitufanye wanadamu tuwe na haraka ya kumpa hukumu isiyo ya haki. Na kwenye mienendo ya maisha, ni mwanadamu gani asiye na mapungufu?

Maana, tangu mara ile ilipofahamika, kuwa msichana Elizabeth ‘ Lulu' Michael alikuwepo kwenye mazingira ya kutokea kwa kifo cha Kanumba, basi, jamii, huku ikisaidiwa na vyombo vya habari, haraka ikapata wa kumnyoshea kidole. Na hukumu ya Lulu kutoka kwa wanajamii walo wengi ikawa imetolewa hapo. Kwamba Lulu ndiye muuaji. Kwa sasa, hukumu hiyo haiwezi ikawa ya haki mpaka pale wenye mamlaka ya kututhibitishia hilo watakapofanya hivyo.

Na hata kama ugomvi, uliotokana na wivu wa kimapenzi , wa Lulu na mpenzi wake ulipelekea mauti ya Kanumba, bado maelezo tuliyoyasikia hayamwonyeshi Lulu kuwa na dhamira ya kutaka kutenda maovu anayohukumiwa na wanajamii kuwa kayatenda. Hivyo, naye, kama mwanadamu, anastahili msamaha kutoka kwa wanajamii wengi walo wema.

Katika wakati huu mgumu sana kwa msichana Lulu, vyombo vya habari viwe mbele katika kumsaidia Lulu kama mwanadamu mwenzetu, badala ya kutumia balaa lililomkuta kama mtaji wa kuandika na kutangaza udaku wa kuuzia magazeti na kuvutia watazamaji wa runinga na wasikilizaji wa redio.

Maana, kwa adhamiriae kutumia magumu yanayomkabili msichana Lulu kuvuna, basi, hana atakachokivuna zaidi ya kuvuna dhambi.

Badala yake, media isaidie katika kutufanya wanajamii tujitafakari. Kwa vile, habari za matukio ya mahusiano yasiyo na staha na matendo ya kiuhuni yanayofanywa na baadhi ya wanajamii wakiwemo wasanii, huwa yanashabikiwa na vyombo vya habari badala ya vyombo hivyo kushiriki kukemea na kuelimisha jamii. inasikitisha, kuwa katika wakati huu, vyombo hivyo vya habari vyaweza kabisa kuwa kwenye harakati za kuandaa stori zaidi za ‘ kumning’iniza’ zaidi Lulu ambaye tayari ameshaning’inizwa hadharani.

Ndugu zangu,

Kama wanajamii, na wengine kama wazazi. Lulu anabaki kuwa ni msichana mdogo anayehitaji kusaidiwa katika wakati huu mgumu kwa maisha yake. Yumkini vyombo vya dola vinaweza vimtie au visimtie hatiani. Hivyo, kumwachia huru Lulu.

Lakini, bado hukumu ya jamii ikabaki pale pale. Hukumu ya Lulu kutengwa na jamii. Hiyo ni hukumu mbaya zaidi inayoweza kuchangia hata kuyafupisha maisha ya msichana huyu mdogo. Jamii haina faida na hukumu kama hiyo. Ni heri ikamwacha huru aende akapambane na yanayomkabili mbele yake. Ndio, akapambane na maisha haya magumu ya dunia hii bila kujisikia kutengwa na wanajamii wenzake.

Na naamini, leo kuna wengi kama mimi, wenye kufikiri hili, kuwa jamii ya walo wema imsamehe Elizabeth ‘ Lulu’ Michael.

Na hilo ni Neno La Leo.

Maggid Mjengwa
Dar es Salaam.
0788 111 765
http://mjengwablog.com

2 comments:

Anonymous April 11, 2012 at 8:30 PM  

wiki jana lulu alisema yeye hana mpenzi! msisahau aliyasema kwenye kadamnasi kwenye luninga akiwa na salama; aliaaswa aondokane na matatizo aliyo nayo na kuaswa hata kama mtumiaji wa madawa ya kulevya awache na mtu ambaye ni msanii mwenzake. turudi nyuma tuseme kifo kimetokea, aidha kwa bahati mbaya au kwa makusudi--acheni sheria ichukue mkondo wake. mtamuweka binti huyu hatiani mkiongeza gia ambayo itaanza kuuliza kulikoni?

Amani Swalehe April 17, 2012 at 11:51 AM  

marehemu naye anamakosa kwani kwa sababu alikuwa maarufu ndo tusiseme??? LULU is just a innocent kids not in need of forgiveness from anybody
MJENGWA.

Wa kulaumu ni KANUMBA mwenyewe ambaye alikuwa ni mtu mzima umri miaka 28 anatoka na LULU kale katoto.. kinyume na sheria hata utamaduni wetu wa leo, LULU kamaliza kidato cha mwaka jana, binti mdogo coz she is a teenager living by imitating wat other superstars doing.


Wakati wa kuacha sheria ifuate mkondo wake kwa hata marehemu anamakosa nani anajua uhusiano huo ulianza lini?? mimi sikutegemea msanii nilikuwa namheshimu kama MAREHEMU KANUMBA angekuwa anatoka na mtoto mdogo kama LULU!!! ni aibu kabisa.

Mimi nina omba wazazi wote wajiweke kwenye nafasi ya wazazi wa LULU na uchungu unaopata unaposikia mwana mwenye umri huo agalabu anatoka na mtoto mzima wa aina ya KANUMBA au wazee wengine wenye uchu!! i knw every body got some weaknes but we shouldnt provide cover up for late KANUMBA finding reasons to justify what he did and push all the blames to LULU!! TUACHEE USHABIKI NA KUANGALIA HISIA NA STATUS YA MTU BALI KUJALI HAKI YA KILA MMOJA WETU AWE HAI AU AMETANGULIA MBELE YA HAKI..TUSIJITWISHE MAJUKUMU YA MAHAKAMA MJENGEWA, LET US SUPPORT THE KIDS WITHOUT JUDGING HER, WHO KNOWS WHAT HAPPENED?? EVERY BODY KNOWS WHAT WE ARE CAPABLE OF DOING BCOZ JEALOUS.. REST IN PEACE THE GREAT KANUMBA YOU AND WE WILL BE NEXT, it's nature, we will never LIVE FOREVER

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP