Tuesday, May 22, 2012

Wakulima na Wafugaji Wanagombania nini?

"Kuna kiongozi mmoja alishasema wafugaji warudi walikotoka, kama kuna anayejua wafugaji wa Tanzania wanatoka wapi aniambie. Hostility iliyopo kati ya wafugaji na wakulima imejengwa na viongozi na watendaji wabinafsi wanaotumia uelewa mdogo wa sheria kuwatreat unfairly wafugaji. Unapomkamata mfugaji kwa kosa la kuingiza mifugo kwenye shamba la mkulima halafu kiongozi anajifanya polisi na mahakama kwa wakati mmoja ananyang'anya ng'ombe kama faini bila kufikishwa mahakamani tena wengine bila risiti inawafanya wafugaji wajenge chuki na wakulima wakidhani ndiyo wanaowafanya kuwa masikini. Tujenge utamaduni wa kushughulikia kero badala ya kusubiri matukio ndiyo tuchukue hatua. Mimi nikiangalia mbele na huu uwekezaji unachukua maeneo kwa kisingizio cha kilimo kwanza napata wasiwasi" 

- Mwanabidii AM

"Kuna shida hasa ya kiutawala. Mipango tunayo, haitekelezwi ipasavyo. Tatizo la ugomvi kati ya wakulima na wafugaji, wawekezaji na wakulima/wafugaji, wachimba madini wadogo na wakubwa ni la muda mrefu sasa. Maoni ya wadau mbalimbali yanatolewa serikali haisikii wala kutekeleza!

Kinachoendelea ni watanzania kuzoea fujo na mapambano ya kumwaga damu taratibu na kwa uhakika. Ni kweli itafika sehemu, hali itakuwa mbaya kama juhudi za makusudi kuepusha haya haitafanyika.

Ni mara ngapi sasa wananchi wanaona Polisi ndio kikwazo? Juzi juzi wakulima wa korosho kusini walipambana na polisi. Si muda mwingi umepita wananchi walichoma kituo cha polisi kule Hedaru. Na sasa Ikwiriri!! Risasi, mabomu na mizinga haijawahi kushinda duniani. La sivyo Siria ingekuwa imetulia sasa.

Watawala amkeni!!!!"

- Mwanabidii MP

"[S]isi wengine tulitarajia haya pia hasa mara tu walipoanza kuhamisha wafugaji toka Kilosa kuelekea kusini tuliona fika hapa waheshimiwa wanahairisha tatizo. huu ni mwanzo tu, tusubiri makubwa sana"

- Mwanabidii EH

"Kwanza naomba kabla sijatoa maoni yangu nitangaze maslahi mapema: mimi ni mtoto wa mfugaji na ni mfugaji pia. Shida ni je wafugaji waende wapi? Ardhi imeuzwa kwa wawekezaji, hakuna nyasi za kutosha malisho yao yameuzwa na kuitwa blocks za wawekezaji. Sina habari za mikoa ya kaskazini na usukumani, ila nimeshuhudia mwenyewe wafugaji Karagwe wanahangaika baada ya sehemu zao za asili kuuzwa kwa watu wenye pesa. Tena wengine walionunua ni wabunge wetu. Wanajua wafugaji wanahangaika na mifugo yao hawawezi kulisema hili maana wao ni beneficiary. Mimi wakati nikiwa kijana, ni muda kidogo, ng'ombe walikuwa wamenona na ndo walitusomesha sisi shule. Sasa hivi ng'ombe uzito kama mbuzi, kisa hamna nyasi, hakuna sehemu [za] malisho. Kila siku unasikia wafugaji wanapigana na wakulima, hakuna wa kulaumiwa. Ni matatizo ndio yanawafanya wavamie mashamba ya wakulima. Leo watu wa Karagwe wanalipa fedha wakati wa kiangazi kulisha ng'ombe wao kwenye hizo so-called blocks. Inaumiza sana! Na hizo blocks wameuziana kwa hila, ulaghai, rushwa na kwa bei ya kutupwa. Ukifika Karagwe na maeneo ya jirani ndio utajua kuwa vita ijayo ya nchi hii itakuwa ni ardhi. Nimeona unazungumzia ufugaji wa kisasa, kwani unadhani hawapendi? Lakini wataweza? Unajua kazi za waganga na madaktari wa mifugo huko kwenye wilaya? Wanakusanya kodi za serikali, wanawaomba rushwa wafugaji ili wafanye kazi ambayo wanalipwa ujira. Hawawapi ushauri wa kitaalamu wafugaji. Na hawa watu maisha yao ni kufuga, hawana mashamba wala kazi zingine zinazowaingizia kipato miaka nenda rudi, vizazi na vizazi"

- Mwanabidii LR

"Na hili la vyombo vya habari kuripoti kuwa mapigano ya wakulima na wafugaji wasukuma linalenga kuonyesha nini hasa? Siamini kuwa tatizo la Ikwiriri lina element ya ukabila ndani yake. Kwa nini reporters hawakutuambia pia wakulima walikuwa kabila gani? Tuache sasa kusema kabila, tunakoroga mambo. Kama tatizo ni la wakulima na wafugaji tuaddress issue(s) katika msingi wa kutatua tatizo halisi lililopo, sio kujenga tatizo jingine baya zaidi ya hili lililotokea."

- Mwanabidii PM

"Pamoja na kulaumu serikali lakini jamii pia inahusika. Serikali imeweka mwanya na ina viongozi na watawala corrupt. [Miji] haina uangalizi wa matumizi endelevu kama inavyosemwa hapa:
- Ndio mbung'o walisababisha miti kukatwa usukumani. lakini wanalima intensively na extensively kibiashara na pia wanafuga. Walio wengi hawatumii mbolea ambayo imezagaa katika maboma yao. Zile fikra za utajiri ni idadi ya mifugo sio afya ya mifugo upo bado kwa wafugaji. Hata mkulima na mfugaji apewe eka milioni lakini kama hana matumizi endelevu hazitamtosha. Zamani watu walikuwa wachache, sasa tumezaana sana, tunakaribisha wageni wahamiaji kwa siri hata ndani ya wildlife conservation area kama Loliondo (Soitsambu, Engerosambu etc), Ngorongoro wamo wanafuga kwetu na kulima kwao wamekodisha maeneo yao kwa walima maharage na wapanda maua ya kuuza.

- Mabadiliko ya kiuchumi - wafugaji walio wengi sasa wanalima ili asimalize mifugo, hela za machimboni zimetoa nafasi ya wale waliokuwa vibarua kwa wenzao kuwa na mifugo yao, kulimbikiza mifugo ndio Wealth Status idadi kubwa ya mifugo sio digrii wala kuwa na magari au nyumba ya kisasa - ni Idadi ya Ng'ombe, mbuzi, punda, kondoo. Hivyo katika maeneo yao wanalima kula na kuuza, kufuga-ardhi ipo kipara kabisa na kuingia ndani ya mbuga au misitu ya hifadhi. Unalima na kuhamisha mifugo kupeleka wilaya nyingine. Huko unalishia mashamba na kuchapa watu bakora si unauza mbuzi mmoja unahonga? Mkulima atauza mahindi mangapi ya kuchoma ili apate 50,000/= ampe mtendaji kata au polisi? Hivi sasa wafugaji waliopewa vijiji 8 Kilosa-wanalima mashamba humo, baadhi ya mifugo ipo nje kidogo ya Mikumi National Park porini huko wameficha. Kama ni uongo peleka askari utawaona wanatokea huko. Nani asiyewaona. Ila, mfugo unaoga DIP. Unapoogelea ktk mito ambayo watu ndio chanzo chao cha maji, na wakulima watumiao madawa hovyo na kunywa maji hayo-ndio tunaongeza Cancer katika vizazi na miili yetu na vilewa vya uzawa. Bado hayo madawa ya mkororo yasiyo bora tunayouziwa duka za dawa/kupewa zahanati na kutumia.

-Watu wanaposema wao wafugaji wanahitaji ardhi, lakini semi-arid area ng'ombe mmoja kamilifu (Livestock unit) anatakiwa kutumia ekari 5 hapa TZ. Je kila Boma au Kaya ya mfugaji maeneo hayo ataweza kuzipata ekari hizo, kisha kijiji kizima? Ni wazi ufugaji endelevu muhimu ama tutatiana vilema na kuuana daima. Pia Kilimo endelevu sio cha kuhama hama. Mbuga na misitu kuwepo ni muhimu hakuna ujinga ama sivyo nchi ingekuwa kipara kama Somalia na majangwa mengine. Misitu ya Mkuranga, Rufiji na Lindi, Kilosa, Kilombero, Ulanga kuwepo si Ujinga. Tuyaangalie haya kabla ya Vita isiyoisha.

Tabia ya kuongeza Miji kuingia vijijini na [fasheni] ya miji midogo ya kisasa, itamaliza maeneo ya watu kulima, itameza mashamba kuwa maeneo ya majengo, vizee na watoto wataathirika sana, ukimwi utaongezeka. Si vibaya kuwa na 'City' ambayo [ina] misitu na mashamba ya mifugo na ya kilimo cha mazao. City sio lazima majengo tu-na mashamba ya kilimo na ufugaji wa Kisasa. Mbona Ulaya kuna cities ambazo ukitoka kilometa chache tu unaona ming'ombe minene, kondoo na farasi? Cities zina miti mingi na kivuli? Kuwaje sisi tusiwe na mbuga, misitu na miti tuzagaze mifugo na majumba? Watawachomea Nyumba mahakimu, Polisi na watawala na itakuwa vurugu hasa watu wamechoka kuteswa solution hakuna. hayo ya Rufiji yatazagaa hata upeleke maji ya kuwasha-watakuvizia wewe na watoto wako. Tuyaangalie haya yasifike huko. Tutumie utawala wa sheria na kilimo/ufugaji endelevu. Kuhamahama makazi kwa kilimo na mifugo -Kuishe"

- Mwanabidii HK

"Kusema kweli ni uonevu. Serikali ichunge sana huu uhuru wa kutembea na kuhamahama. Katiba ibadilike ikataze uhamaji hamaji karne hii si ya shifting cultivation wala transhumance katika mifugo. Hata walao matunda pori-miti imeingia fungus matunda hakuna na miti inakufa. Climate change inaleta mabadiliko mpaka ya mfumo wa uchumi. Ulaya wana mifugo mingi ya thamani na mashamba makubwa bali hufuga kisasa. Bima ya mifugo imeanzishwa pia kuna Saccos tubadilike wafugaji. Kuboresha mbegu bora vituo vipo na mbuzi wa maziwa na mapacha kulikoni? 

Hata wakati wa machief watu waliingia maeneo ya wengine kwa makubaliano. Ukienda kwa wafugaji-Arusha, Simanjiro, Monduli au Usukumani, ukuryani hukuti mfugaji analishia mazao ya shamba au mfano mahindi mifugo. Utakuta wamezungusha miti ya miiba (Mkizingo-Acacia Nilotika) na miti ya miba mingineyo kuzuia mifugo isiingie shambani. Huko wanakogombea ardhi na wenzao (Loiboisirret-near Tarangine and Terrat) wanalima kwa matrekta, wanafuga pia ardhi yao imekuwa nyeupe kipara mpaka mto sirret ulikauka, mto terrat umekauka kama wameufufua ni kipindi cha sasa. Hata mradi wa maji wa mto terrat kwa wafugaji umekuwa hautoi maji [ya] matumizi na ulinzi. Ikafika watu wanapiga mkuki mabomba mifugo inywe lakini hayatoki.

Mifugo inalimbikizwa sasa kutokana na hela/mali inayopatikana Mererani na hapo Loboisirret kijijini kwa mfano kuna machimbo pia. Akitoka Simanjiro anaingiza mashamba ya Wapare Ruvu analisha. Mkulima Maasai wa Ruvu halishii shamba lake analolima. Ukiwa na silaha ya mkuki na mbio za kukimbia utaumiza wengine tu. Ila kiboko ya wote ni Waikoma wa Ikoma Robanda huko wanakuogopa hawaingii hovyo labda kuiba mifugo tu. Akiwa Naberera, Kitwai etc analishia katika shamba la mtu ambaye ni wa-kuja (Sio Maa). Kilimo siku hizi hata wafugaji ambao wamekuwa agropastoral wanalima ili wapate chakula wasiuze mifugo ili kununua mahindi. nani ambae haoni mashamba ya mahindi Ngwara, maharage, Monduli, Manyara etc. hata ndani ya ngorongoro ugonmvi kilimo kuongereza.

Kilimo cha mpunga katika majaruba na cha mahindi, kunde Bunda, Geita, Nyanza etc huko Usukumani asiyekiona nani? lakini wanapotaka utajiri kwa kulimbikiza mifugo kuiondoa makwao wakafuge kwingine hulishia mashamba ya wanyonge. Wengine watembeao na mifugo ni vibarua analipwa mfugo kwa miezi ya kuchunga. Mfugaji wa Kisukuma akifika Kigamboni, Rufiji, Mkuranga, Kilwa, Lindi anaona misitu ilivyoshona ni kufyeka miti, kuchuma na kuuza mkaa ili apate chakula na matumizi, akipata fedha nyingi anapeleka kwao kununua mifugo kupata jina la utajiri bila ya kuangalia carrying capacity. Si anajua TZ unahanja na kuharibu popote kisha unahama unakwenda kuharibu kwingine?

Hata siku moja hutoona mfugaji akilishia mifugo shambani kwake lakini kwa mkulima au mtu si wa kabila lake atafanya calculated humiliation na ethnocentrism zao na kutesa wengine. Hata hapa DSM wenye mifugo hawalishii mashambani mwao. Ifike sasa kufuga na kulima sustainably iwe sheria; kuhifadhi ardhi na misitu iwe sheria; watu kuhama hama hovyo nje ya maeneo yao kwa kibali na mifugo isitembee kwa miguu inaleta matatizo; mifugo inayowekwa kwa siri na viongozi wa kata, vijiji kuruhusu wafugaji kukaa katika mapori kwa siri, kupitisha mifugo usiku mashambani wawajibishwe. Kwani wafugaji wanalishia mashamba ya watu usiku wa manane mtu anakosa food security. Kutoka Geita hadi Kilosa au Manyara hadi Mikumi National Park ni ufisadi na rushwa zinazoleta mauaji ya watu wasio na hatia. Vibibi haviruhusiwi kuokota kuni maeneo yao ya zamani eti sasa ni maeneo ya wafugaji waliohamia-kisiri. Kibibi kikienda kinabakwa.

Hayo mauaji ya Rufiji huko Kilwa na Lindi watakuwa wameshajiandaa hao wafugaji hawatopita kama ndio wameua na wanaelekea huko. Hiyo Rice bread basket area imekwisha hakuna kulima tena mipunga ni mifugo mashambani. Hata Uvuvi-wanaingia kuvua kwa mabomu kutoka maeneo yao ya mbali kwenda maeneo ambapo wavuvi wa huko wanalinda mikoko na masalia ya samaki. Kisha wavuvi wenyeji wakichoma vibanda ya wavuvi wahamiaji waharibifu wa mazingira ili waondoke-serikali inawakamata na kuwafunga (Kilwa Kisiwani).

Wanapoharibu mazingira yao kisha ni kuvamia maeneo na mashamba ya wawekezaji kwa visingizio wadhibitiwe. Tunapogawiwa maeneo ya mashamba ya serikali ya zamani tulime-lakini tunauza kwa wengine ambao wanajenga majumba za biashara badala ya sisi kulima kisha tunahamia barabarani ambako tunabomolewa.Ifike wakati kuwa, ukipewa ardhi marufuku kuiua mpaka miaka kadhaa ipite na usibadili matumizi bila kibali. Hii itaepusha watu kuuza ardhi na kulewea pombe hela kwa kisingizio cha kuhamia kwingine mapori yapo.

Uhamaji hamaji, ujambazi na mauaji, usalama mdogo vijijini inakera. watu hawatalima, hawatasoma, hawatakwenda hospitali, watachomeana nyumba haya mambo yatokomezwe.
Inakera. 

- Mwanabidii HK
  
CHANZO: 

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP