Sunday, October 28, 2012

Hoja za Wanazuoni kuhusu Maadui wa Waislamu


Baadhi ya Hoja Zilizoibuliwa na Wanazuoni Kutokana na Makala ya Mohammed Mtoi Kuhusu Maadui wa Waislamu na Uislamu

---
Hoja za wanaodai kuwa TZ kuna mfumo kristo ziko wazi na sehemu ambazo unaweza kusikiliza kwa undani ni misikiti kadhaa ya kariakoo na msikiti wa mwenge, among others. Pia kuna CDs nyingi zimetengenezwa na hoja zimechambuliwa kwa kina. Ukipata fursa nenda ktk moja ya misikiti hiyo na uweze kujadiliana nao. Binafsi ktk kutaka kujifahamisha kuhusu hili nimehudhuria misikiti kadhaa (tangu mwaka 2008 mahsusi kwa jambo hili) ukiwemo wa Mwenge ambao ni kinara wa mambo haya. Baada ya Sala za Ijumaa na miezi ya Ramadhani kwenye Darsa za jioni nimejitahidi sana kufanya mijadala na waumini wenzangu kuhusu swala hili ili kujifunza zaidi. Na Allah ndie mwenye kujua zaidi.

Baadhi ya siku nilihisi Ijumaa yangu imepotea kwani sikufurahishwa na hutba zilizotolewa kwa kuwa ktk jazba zilikiuka sheria za Ijumaa. Pale (mwenge na kwingineko) uwe makini maana kuna wenye jazba sana. Namshukuru Allah kuwa nilijifanya mjinga ili nieleweshwe na sikwenda kwa lengo la kubishana. Sitochukua jukumu la kuziwasilisha hoja zao hapa kwa kuwa wenyewe wapo na wanaweza kuzizungumzia. 

Nadhani itapendeza sana ukizipata na kisha kujibu moja baada ya nyingine na kuonesha ni kwa kiasi gani hazina mashiko badala ya kufanya majumuisho kana kwamba sote tuna uelewa mmoja/sawa kuhusu hoja hizo.

Binafsi nazifahamu lakini sishawishiki kuanza kuzijadili kwani ni nyingi. Na pia sidhani kama wale Waislam wenye kudai kuwa kuna mfumo kristo wamo humu wanazuoni. I am engaging in dialogue with them in various forums (fora) and i have been an active participant in that (neither a supporter nor an opposer, just a curious learner, as always).

Naamini siwezi kutendea haki hoja zao kwa kuwa mimi si mfuasi wa madai kuwa kuna mfumo kristo. Kama wamo humu wanazuoni basi tujadiliane. Kwa uchache ktk uliyoungumzia, wao wangeweza kujibu ifuatavyo (kwa mtazamo wangu mimi):

1. Nina uhakika wangependa sana hoja yako kuhusu CCM ambayo binafsi sikubaliani nayo. Na huu ni mtazamo wangu si lazima ukubaliane nao na wala mimi si mfuasi wa chama chochote cha siasa TZ.

2. Nina uhakika wangependa sana hoja yako kuhusu Bakwata kuwa ni chombo kilichoundwa ili kuhakikisha serikali yenye mfumo kristo imewatia mikononi waislam. Waislam wanaodai kuwa TZ kuna mfumo kristo wanaipinga sana Bakwata. Lakini nadhani watapingana nawe ktk swala la vigezo vya nani awe kiongozi wa Bakwata. Hata MUM [Muslim University of Morogoro] haina sifa hizo za kubobea ktk elimu zote mbili. Nafahamu some prominent muslims with PhDs walioacha kazi MUM kwa kuwa wanaona imejikita zaidi ktk elimu akhera na kupunja maslahi ya wahadhiri.

3. Pia sio kila mtu mwenye jina lenye asili ya uarabuni au ambae ni muislam anasimamia maslahi ya waislam siku zote. Kwa hivyo hoja ya kutumia majina ya watu wenye vyeo mbalimbali kuthibitisha kuwa waislam wamo serikalini wao wanaipinga kwa kudai kuwa hao wamo kwa majina tu na wanatumika kutekeleza maslah ya mfumo kristo unaodhibitiwa na kanisa katoliki.
I usually look at this issue from a structural violence framework in analysing state-people relations of power in producing subjects and subjectivities and not in producing citizens. 

...

[Tusisahau kuwa kuna mapambano yanaendelea dhidi ya "mfumo dume", Tujifunze toka mapambano hayo ktk kuchanganua mapambano haya dhidi ya "mfumo kristo"]

- Baruani
---
 Mimi ni Mchungaji (japo sina kundi la kuchunga) siamini kwamba tatizo la hapa Tanzania ni Ukristo dhidi ya Uislam au kinyume chake. Bali kushindwa kutambua kwamba kusudi la Imani either ya Kikristo au Kiisilamu si kuishi baada ya kufa bali kutupatia matumaini ya maisha ya sasa. Kudhania kwamba matumani ya maisha ya sasa yanatoweka kwa sababu ya dini moja au nyingine ni kushindwa kutathmini dini as tour de force na driver ya maendeleo.  Dini inatakiwa kuleta maendeleo with certainty ya maisha ya hapa na sasa (here and now (etiology)).  Kadhalika, kuifanya dini kuwapa watu matumaini ya maisha ya baadaye (hope for future life (teleology). Kushindwa kugundua kwamba religion is for our common good, some have shifted the burden of our common enemy- poverty - to religion to which they have missed the mark. 


- Chaggama
---
Dear Mchungaji, with all due respect, the origins of these two religions, history of their expansion over the centuries, modern realities in many Asian, Middle-Eastern, North and West African nations, and now add in the list KENYA AND TANZANIA, will contradict that PC, and, I am sorry to say, timid, opinion.


WIKENDI HII huko Zanzibar kuna mkutano kati ya wazee wa mabaraza na viongozi wa chuo kimoja chenye campus yake Zanzibar kwa kuwa 'wenyeji' wamekasirika kwamba wanafunzi wa chuo hicho 'wanavaa vibaya'. So what, kwani wamewakalia kwenye mapaja?! (Hausikii vituko hivi huko Ulaya na Marekani kwa sasa - lakini, kama population growth trends za sasa zikiendelea, tutayaona tu...)

Tatizo ni DINI: lack of tolerance kwa imani, mitazamo au lifestyles nyingine; kwa ufupi - political ideology yenye msingi katika imani yenye nia ya kutawala, hata kwa kutumia nguvu, sekta zote za kitaifa. Kwa ideology hii, the end justifies the means na malipo ni akhera. So, no ethical considerations here.

Kwa nini yule Imamu wa Kipakistani aliamua kumtoa kafara mtoto mdogo wa Kikristo? Sio kwa sababu ya chuki binafsi, sio hata kwa sababu ya UMASKINI Mchungaji, (ambao upo kila sehemu lakini watu hawachomeani nyumba za ibada!), kwa maneno yake: 'hii ni njia rahisi ya kuwafukuza Wakristo katika kijiji hiki'. Matatizo ya Wazanzibari kwa muungano, 'wabara', wageni, makobe, n.k. yote yana hii religious element.

Coming to a village near you shortly...

- Charles
---
Charles, nakushukuru kwa kunielimisha zaidi. Ngoja nijaribu kuandika kwa njia pana kidogo. Deo alipendekeza kwamba pawepo na moderators ili kutafuta suluhisho la amani yetu. Nilikubaliana na Deo kwamba, moderators wawepo. Labda tusiwaite moderators towaite 'Peace Builders' watakaojihusisha na conflict resolution na post conflict solutions. Hivyo basi, Nilijaribu kuelezea kwamba tatizo letu hapa ni kushindwa kuisoma dini katika muktadha wake sahihi (tour de force). Kama wakiwepo peace builders wawasaidie rioters kugundua kwamba tatizo ni Ubeberu sio Dini. 

Ndio maana nikasema wakristo na waislam wa Tanzania adui yetu wa pamoja ni umasikini. Hivyo solution yake sio kulumbana au kupambana kwa kuchoma makanisa au kuua watu, bali kuitumia dini kuutokomeza umasikini. Wakristo wa Ulaya walipigana sana wao kwa wao (Inqusition). Wale waliohamia Marekani wakasema vita basi. Ila dini ya Puritan ikawa ni driver ya accountability ili kujenga uchumi na taifa lenye amani. Hoja yangu ilikuwa ina precedent ya historia ya dini Ulaya na mustakabali wake kimaendeleo. Hadi leo, Wamarekani wameshikamana pamoja na kuwa kila dini imewakilishwa katika nchi hiyo. Wamarekani kisiasa na kiuchumi hawana permanent friend, ila wana permanent American interest. Hiki ndicho tunachotakiwa kuwa nacho hapa Tanzania. Wakati fulani Waislam wamarekani walimuona Mchungaji Dr Martin Luther King Jr, kama Spiritual leader wao. That means that adui yao wa kweli alikuwa (still yet) ni umasikini na unyanyaswaji na Wazungu. 

Hivyo Charles, nilikuwa napendekeza tu kwamba huyo moderator ambaye tumemuita peace builder alenge kwenye tatizo halisi. Mfano, Biblia na Quran zote zina mafungu ya kisasa 'lex talionis' kama waitavyo wanasheria. Ila within the right context, when these texts are correctly interpreted can change vengeance into peace building necessary for economic growth. Tafasiri zikikosewa zinaweza leta maangamizi na zikipatiwa zinaweza leta amani.

- Chaggama
---
All of those are a product of capitalism lifestyle and in particlar neoliberalism; not the so called "Mfumo Kristo"

- Madaha
---
Hatuwezi kupata suluhisho la tatizo lililopo Tanzania bila kufahamu nini hasa kinapelekea hali tuliyonayo. Na sikubaliani na hoja yako ya kusema hili swala halituhusu. Jaribu kwenda mitaani kunako vurumai sasa hivi ukawaambie kuwa halituhusu uone kama utasikilizwa. Hata kama ingekuwa ni ugomvi kati ya uarabu na neoliberalism, tayari sisi tumeingia humo katikati na tunapigana. Hatuwezi kujitoa by simply saying si ugomvi wetu. Sana sana tutazima moto sasa lakini bado vuguvugu linafukuta na moto utaibuka tena. Tutaendelea kupayuka na kujibizana kama wanazuoni lakini mchango wetu utakuwa ni insignificant ktk kupata suluhisho.


Vijana na wazee wa kitanzania wameshajimilikisha mapambano haya na wanaendelea kujipanga. Hoja wanazozitumia kumobilize watu bado hazijapanguliwa. They have articulated and appropriated a local and global history of struggles between Muslims and the state and contend that the state received support from western countries to suppress Islam in Tanzania and in the region since 1960s.  Mfano ni hoja ya kufa kwa juhudi za kuwa na East African Muslim Association badala yake kuwa na BAKWATA, na mengineyo.


Malumbano ya jazba, kejeli, dharau na mbwembwe nyingi hayatasaidia kutatua tatizo, bali yataharibu mawasiliano baina ya watu na kuharibu uwezekano wa kuwa na mdahalo wa kistaarabu.

- Baruani
---
Nikirudi kwa Mchungaji wetu, nakubaliana kabisa kwamba tatizo si DINI, na Adui yetu ni UMASKINI, lakini tusisahau 'inequality', 'inequity', 'exclusion' n.k. ni factors zinachangia umaskini.  Na umaskini wetu uko lopsided, yaani wengine (wachache) wananeemeka na wengine wako katika dhiki kali (kwa sababu ya kuwa excluded katika mainstream-economics and social services) wakingojea trickle down amabayo haijasaidia.  Ndiyo maana kuna 'Discontents', ambazo baadhi ya mwanazuoni alisema kwamba kuna struggle ya Waislam kama kweli ni 'Waislam' kujiondoa katika kile kinaitwa kukandamizwa kwa muda mrefu na mfumo wanaouita 'MFUMO KRISTO.  Ndgu Baruani aliandika hivi "Vijana na wazee wa kitanzania wameshajimilikisha mapambano haya na wanaendelea kujipanga". 


Maswali ambayo tujiulize, 

1. Je, kuchoma makanisa ni sehemu ya hayo mapambano dhidi ya dhana ya mfumo wanaouita Mfumo KRISTO?  Je, hawa vijana na wazee wa kitanzania waliojipanga  katika 'statement' ya Baruani ni kina nani, je ni Waislam au ni Magaidi au RELIGIOUS Extremist ambao wameteka nyara DINI ya Uislam, na wanatumia kivuli cha Uislam, kama BOKO Haram kule Nigeria, kufikia malengo yao ya kisiasa n.k.?


Nashawishika kwamba Ndugu Madaha, amekuwa 'critical' na akaja na dhana ya Mfumo Arab-Islam, kuonyesha kwamba DINI ya Uislam inahujumiwa na ndiyo maana tunatakiwa kuwa makini sana hapa, vinginevyo hatuwezi kufikia muafaka, maana leo Makanisa yanachomwa moto, kuna siku yatachomwa na watu watapoteza maisha.  Ni vizuri kupambanua DINI na Ugaidi/Religious extremist tusichanganye masomo hapa, hasa katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa sasa haya matatizo yanaendelea kukua, angalia hapo Kenya, nadhani nimeleweka.

Pia nakubaliana kwa upande mwingine kwamba ni lazima utafiti ufanywe kuelewa kiini cha tatizo, na hii inawezekana na ninashauri kutumia ACTION Research, au research design yeyote ambayo itatoa matokeo yasiyoegemea upande mmoja.  Baada ya hapo tutaona pa kuanzia, meanwhile ni vizuri serikali ifanye wajibu wake na wale wanaovunja sheria kwa visingizio vyovyote vile, sheria ichukue mkondo wake. 

Ni muhimu hapa KIONGOZI wa NCHI yetu yaani RAIS wetu wa Jamhuri aonyeshe true leadership bila kuegemea upande mmoja, maana yeye ni kiongozi wa Watanzania, si wa Waislam au Wakristo, au wasio na dini peke yao, ni kiongozi wetu, kwa hiyo ana wajibu wa kuhakikisha anakemea haya mambo kwa nguvu zote alizopewa na KATIBA na kwa mujibu wa KATIBA, na kulinda kisiwa chetu cha amani TANZANIA yetu tunachojivunia.

- Masabuda
---
Swali ambalo huwa ninajiuliza ni kwamba, Hivi bila hizi imani za "kikoloni" kusingekuwa na Maisha?


- Gabriel
---
natamani ingekuwa rahisi watu kutoka nje ya mifumo fikra yao ili waweze kusikilizana na wenzao wenye mifumo fikra tofauti. huu ndio haswa msingi wa kusikilizana. najaribu kumsikia baruani. amejaribu tena na tena kusema hao waliojimilikisha hayo mapambano hawamo humu mtandaoni lakini wapo. kama tunataka kuelewa hoja zao (na hasemi anaziafiki wala sisi tuziafiki) ni bora kujifunza kutoka kwao; ndipo tupembue chuya na safi ili tujue tulipo na jinsi gani tunaweza kuzuia tufani ambayo dalili za mawingu inayokusanya tunaishuhudia hivi sasa. haitoshi kuwaita hawa jamaa kuwa ni magaidi n.k. kwa kuwa wawe wawavyo, wapo na hoja yao inauzika kwa walio pembezoni--na wenye kuitikia itikadi wanayoitumia kuuza sera zao. hivi ndivyo tafrani nyingine duniani zilivyotokea--watu walio pembezoni, walio wengi hawaridhishwi na hali ilivyo, anatokea 'masia' anasema kisa ni wale... anaweza kuwaita 'magabacholi' au 'makwerekwere' au 'semites/mayahudi' au 'shiites' au 'wakristu/to' au 'watutsi' chochote kile lakini moto ukiwaka ni maelfu na maelfu ya mauaji. haikumzuia hitler kuua wayahudi kwa kumuita nazi; wala intarahamwe kufanya mauaji ya kimbari kwa kuitwa hivyo--tumejiita wanazuoni, basi tumejitwika dhamana ya kutafakari mitafaruku ya kijamii kwa kina na kihistoria ili  kuitafutia suluhu madhubuti hata kabla waliopewa dhamana rasmi wakikawia kubaini ukubwa wa tatizo. huu ni wajibu wa kila msomi wa jamii kutumia elimu yake kuinusuru jamii na kizazi chake kutoka kwenye zahama za aina hii--na hili ni anga lililo wazi mbele ya macho yetu, haifai kulifanyia mzaha.

- Demere
---
VYANZO

MJADALA:


PICHA:1 comments:

Anonymous October 29, 2012 at 8:33 AM  

Asante Chambi kwa mazungumzo ya muhimu sana na yenye maudhui ya kisiasa na kiutawala. Na pia nimefurahishwa sana na picha ulizotoa za hayati Mwalimu Nyerere na mashekhe kwenye nyakati za uhuru.

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP