Monday, November 5, 2012

Kideo: Makulilo Ajibu Maswali Kuhusu Skolashipu

Da Subi, Chambi na Mwangomile,

Nimeandaa majibu ya yale maswali ya scholarships ya ndugu Mwangomile. 

VIDEO YENYE MAJIBU HII HAPA 


Swahili la mwisho la TOEFL/IELTS ntalijibu kwenye video ya pekee kwani lina maelezo marefu kidogo.

MUHIMU:

Maelezo zaidi pamoja na video ya Recommendation Letter hii hapa http://www.makulilofoundation.org/2010/11/recommendation-letters.html

Hii ni video nyingine, nimetengeneza leo...hii ni kuhusu TOEFL/IELTS and here is the link:


Mtihani wa kupima uwezo wa lugha ya Kiingereza (English Proficiency Test). Katika makala moja niligusia kuhusu mtihani huu. Kwa ufupi ni kwamba, kwa kuwa Tanzania lugha ya Taifa ni Kiswahili (si Kiingereza) japokuwa elimu ya juu hutumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia, mwombaji lazima aoneshe vyeti kuwa anajua lugha ya Kiingereza kwa ufasaha na ana uwezo wa kusoma shahada anayoomba. Hakuna mtihani wowote ule au cheti chochote kile kinachotakiwa isipokuwa kimoja kati yah ii mitihani miwili: International English Language Testing System (IELTS) au Test of English as Foreign Language (TOEFL). Huu IELTS ni wa Waingereza na unafanyikia pale British Council, na TOEFL ni wa Wamarekani unafanyikia University Computing Center – UCC tawi la University of Dar es Salaam, Mlimani.
Ni mara chache sana kupewa ruhusa ya kutuma maombi yako bila kuwa na cheti cha mtihani mmoja wa lugha kati ya hiyo. Udhamini wa Norway (Quota Scheme) wao huruhusu waombaji ambao wamesoma masomo ya sekondari na chuo (elimu ya juu) ambapo lugha ya Kiingereza ilitumika kama lugha ya kufundishia, kutowasilisha cheti cha aidha TOEFL au IELTS. Kwa vyuo vingine ni lazima uoneshe cheti cha lugha ya Kiingereza.
Ushauri wangu: Usisibirie mambo ya bahati ya mtende kuota jangwani kwa kutofanya mtihani huo wa lugha ya Kiingereza. Watu wengi hawafanyi mtihani huu, na wakiomba vyuo wakikosa wanaanza kulaumu, mara kuna upendeleo nk. Wanasahau kuwa VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA inapokuja suala zima la udahili na udhamini wa elimu ughaibuni. Ni vyema ufanye mtihani huu uwe katika nafasi nzuri ya kuwa mshindani mkubwa kuondokana na kuwa mshiriki au msindikizaji. Japokuwa ni gharama kulipia na kujiandaa kufanya mtihani huo, ni uwekezaji mzuri kwani unalipa, na faida yake ni kupata udhamini na kutimiza ndoto yako ya kielimu ughaibuni.

MAKULILO
CALIFORNIA, USA
----------------- 
Ernest Boniface Makulilo
Fulbright Scholar 2008-09 (Marshall University, WV)
Rotary Ambassadorial Scholar 2009-10
MA Peace and Justice Studies, May 2010 (University of San Diego, CA)


1 comments:

Anonymous November 10, 2012 at 10:17 PM  

Wapi In kigamboni unafanya TOEFL?

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP