Monday, December 3, 2012

Mbona Wanafunzi Wanafeli Kiswahili Pia?

KITILA MKUMBO:
Narudia tena kusema kwamba mpaka sasa hivi hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kwamba kushuka kwa elimu yetu, kunakoonekana zaidi kutokana na wahitimu wengi kufeli mitihani ya mwisho, kunatokana na matumizi ya lugha ya Kiingereza katika elimu. Ingekuwa tatizo ni lugha ya Kiingereza, wahitimu wa shule za msingi wangekuwa wanafanya vizuri kwa sababu lugha inayotumika huko ni Kiswahili. Lakini sivyo hali ilivyo. Ngoja niwape mfano. Matokeo ya mwaka jana (2011) asilimia 43 ya wahitimu wa elimu ya msingi (darasa la saba au LY) walifeli (sifuri). Katika mwaka huo wa 2011 asilimia 46 ya wahitimu wa elimu ya sekondari (Kidato cha Nne) walifeli (division 0), ambayo kitakwimu haina tofauti na hiyo ya elimu ya msingi. Na hali ipo hivyo hivyo katika miaka mingine. Sasa naombeni mnieleze kama tatizo ni Kiingereza kwa nini darasa la saba wanafeli kiasi hicho wakati wanatumia lugha yetu pendwa ya Kiswahili? Ndio ninarudia kusema kwamba tatizo la elimu yetu ni kubwa mno na ni urahisishaji wa mambo kukitupia lawama Kiingereza. Sababu kubwa inayotolewa mara kwa mara ya kutaka tuachane na Kiingereza ni kwa sababu watu wengi hawakimudu-wanafunzi kwa walimu. Hii ni sababu dhaifu kwa sababu inatoa taswira kwamba sisi watanzania hatufundishiki lugha hii, kitu ambacho sio kweli. Watu wengi hawakimudu kwa sababu hatujawekeza katika kuhakikisha kwamba tunajifunza lugha hizi mbili vizuri. Ndivyo itakavyokuwa kwa Kiswahili. Watu wanadhani itakuwa rahisi na mteremko tukianza kutumia Kiswahili. Ukweli ni kwamba tusipowekeza kujifunza Kiswahili cha kitaaluma tutajikuta tunayazunguka matatizo yetu badala ya kuyatatua. Tunahitaji kuwa makini sana, na kupunguza uanaharakati katika jambo kubwa kama hili la elimu na lugha. 

KUNDA STEPHEN:
Kwanza tukubaliane kuanguka kwa kishindo kwa elimu Tanzania (msingi na sekondari) kuna sababu nyingi ambazo ziko kwenye mipango mibovu na ya ubabaishaji iliyo kwenye sekta hiyo na siyo lugha pekee. Msingi kuna sababu zake na sekondari kuna sababu zake. Hata kama interventions zitawekwa haziwezi kuwa similar. These levels are beyond compare, huku ni watoto ambao ndiyo wanajifunza both lugha na facts za masomo, na huku watoto ni more matured ambao wanatakiwa kujua zaidi vile walivyojifunza. Hivyo si sahihi kusema kwamba kama sababu ni lugha ya kiingereza basi msingi wangefaulu zaidi kwa sababu wanatumia kiswahili. Huyu mtoto ambaye ametoka msingi ambako anafundishwa kwa kutumia lugha yake akaingia sekondari na kufundishwa kwa kiingereza kisicho sahihi anapata nini kama ile medium of communication ni poor na pia yeye hana msingi mzuri wa lugha hiyo? Sanasana tunafundisha watoto kiingereza kibovu kisichokubalika popote na contents (facts za masomo) hawazipati, that is my hypothesis. Kama tunataka kutumia kiingereza, tunahitaji maandalizi ya muda ambayo ni pamoja na walimu watakaowaandaa watoto vizuri msingi ili waweza kufundishwa kwa kiingereza sekondari na vyuoni, kitu ambacho kwa sasa hatuna. Kwa hili naweza kusema kwa sekondari kufeli kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na lugha (among other reasons). Kiswahili kiendelee kutumiwa up until tutakuwa tumejenga msingi mzuri wa kufundishia kiingereza, tusiparamie tu kufundisha watoto kiingereza sasa hivi.

SABATHO NYAMSENDA:
Je, kufaulu kwa wanafunzi katika mitihani ni kipimo cha elimu bora? Hoja ni kueneza maarifa kwa binadamu, maarifa hayo yakamkomboe katika maisha yake na ya jamii inayomzunguka. Kiingereza, imetajwa, ni moja ya vikwazo vinavyowanyima wanafunzi wetu maarifa. Hili halihitaji tafiti za kisayansi, hata kama zipo na zinafanyika. Kwa bahati nzuri wewe [Kitila] ni mwalimu wa Chuo Kikuu, unaweza kutumegea uzoefu wako uwapo darasani. Nakumbuka nikiwa mwaka wa pili, Prof. Mukandala, ambaye ni makamu mkuu wa Chuo, alikuwa akitufundisha somo liitwalo Utawala wa Umma (au kwa ‘kitaalamu’ Public Administration). Kila akianza kuzungumza wanafunzi wanajikunyata, wanakosa raha. Profesa naye, mwalimu kweli kweli. Anajua tatizo la wanafunzi wake, hataki awanyime maarifa. Anatwanga Kiswahili. Wanafunzi wanatabasamu na kushangilia: Tumeelewa! Nikiwa mwanafunzi, niliwahi kumtafuta bila mafanikio [kutokana na urasimu wa ofisi zetu za umma] ili nimtake aanzishe mchakato wa kubadili lugha ya kufundishia CKD. Sikutegemea kuwa angefanya hivyo lakini labda angesaidia katika kuibua mjadala.

IMMA DOMINIC:
Kutokimudu Kiingereza/ lugha nyingine yoyote ile inachangiwa sana na ubora wa mfundishaji, kama mwanafunzi yupo vizuri kiakili na vifaa vya kufundishia vipo. Hiyo kauli ya kutofundishika...inashusha hadhi ya mtanzania chini ya mnyama/paka maana hata yeye ukimfundisha with time ataelewa mahali pake pa kulala, n.k (sidhani kama hii ni hoja ya wanaounga mkono kiswahili, au yamkini imeeleweka visivyo...Kiswahili ni lugha inayoeleweka kwa walimu na wanafunzi wengi Tz, na hutumika sana ktk mazingira na shughuli zetu za kawaida hivyo inakidhi vigezo vya kuwa lugha ya kufundishia...Pamoja na hiyo, hakuna aliyepinga kwamba lazima kiswahili kiboreshwe au tujifunze kiswahili fasaha...sababu ukweli ni kwamba lugha kwa kuongea kawaida haina masharti mengi ila katika nyanja ya utaalam...kuna kanuni zake, misamiati yake na uandishi wake. Hivyo maandalizi bora yakifanywa na tukianza kukitumia Kiswahili hayo ya lugha na ufasaha 
wake yatakuwa hayaepukiki.

CHANZO CHA MJADALA:

CHANZO CHA PICHA:

0 comments:

Karibu kwenye ulingo wa kutafakari kuhusu tunapotoka,tulipo,tuendako na namna ambavyo tutafika huko tuendako/Welcome to a platform for reflecting on where we are coming from, where we are, where we are going and how we will get there

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP